Ruvu Shooting, sikilizeni 'sauti ya ndani' ili kuepuka dhahama toka kwa Simba SC

ninosi

Senior Member
Jun 30, 2022
151
333
Tangu Ruvu Shooting apande ligi kuu katika msimu wa 2016/17, amekutana na Simba SC mara 13 mpaka sasa. Rekodi za timu hizo mbili katika ligi kuu in kama ifuatavyo:-

Ushindi: Simba SC 11-1 Ruvu Shooting
Sare: Simba SC 1-1 Ruvu Shooting
Idadi ya Magoli ya kufunga: Simba SC 36-5 Ruvu Shooting
Ushindi Mkubwa: Simba SC 7-0 Ruvu Shooting

Kwenu Ruvu Shooting:
1. Kwa takwimu hizo chache, Ruvu Shooting mnapataje ujasiri wa kutaka kuingiza timu leo uwanjani? Ndugu zangu Ruvu Shooting sikilizeni 'sauti ya ndani'.

2. Ukiangalia mechi 3 zilizopita, Ruvu Shooting kapoteza 2, draw 1 huku Simba SC akishinda 2, draw 1.. Ruvu Shooting hamuogopi jinaminizi linalowaandama sasa? Ndugu zangu Ruvu Shooting sikilizeni 'sauti ya ndani'.

3. Triple C leo kaamka salama kabisa, na sasa anaelekea kupata kifungua kinywa.. Masau Bwire hamuogopi jinsi Triple C atakavyokua aklisambaza boli Taifa? Ndugu zangu Ruvu Shooting sikilizeni 'sauti ya ndani'.

NB: Wenzenu tuliwaonya wakakaidi, kilichowakuta walitamani kukimbia uwanja.
 
Kwa 'Matomaso'...
Screenshot_2022-11-19-06-58-20~2.jpg
 
Kama Chama anarudi leo naamini Simba itaanza kucheza mpira mzuri, jamaa amekuwa mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Simba SC.
 
Kama Chama anarudi leo naamini Simba itaanza kucheza mpira mzuri, jamaa amekuwa mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Simba SC.

Leo atakua dimbani baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya mechi 3.
 
Wakishinda Yanga, bahasha tena huku nanyie mnafungwa na Yanga, mkishinda nyie mnajua..!! Kweli NGADA ni mbaya

Mkuu ungekaa kimya, tusingeelewa ni kiasi gani wewe ni JUHA. Hapa tunazungumzia mechi kubwa ya leo, baina ya Ruvu Shooting na Simba SC. Hayo masuala ya Yanga, bahasha yanatoka wapi?! l
 
Mkuu ungekaa kimya, tusingeelewa ni kiasi gani wewe ni JUHA. Hapa tunazungumzia mechi kubwa ya leo, baina ya Ruvu Shooting na Simba SC. Hayo masuala ya Yanga, bahasha yanatoka wapi?! l
Ahahahahahaaa Masuala ya Yanga yanatoka kwa Simba. Kwamba Yanga wakishinda mnasema ni bahasha
 
Sawa..!!! Ila usisahau Chama kutokuwepo kwake kwenye mechi za Simba athari yake ni kubwa kuliko huyo jamaa mwingine kwenye timu yake..!! Nyie bila Chama hamchomoki, mnalambwa tu

Japo Chama anaumuhimu wake lakini katila mechi 3 zilizopita ambazo Chama hakuwepo, Simba ilishinda 2 ikadroo 1. Sasa leo Triple C yupo dimbani, kila napowafikiria Ruvu kitakachowakuta naogopa.
 
Japo Chama anaumuhimu wake lakini katila mechi 3 zilizopita ambazo Chama hakuwepo, Simba ilishinda 2 ikadroo 1. Sasa leo Triple C yupo dimbani, kila napowafikiria Ruvu kitakachowakuta naogopa.
Kisa Chama, maana yake umekubali kuwa Chama asipokuwepo mambo yanaharika
 
Ni kweli Ruvu ni wabovu Kwa Simba ila utofauti wao Si mkubwa sana kwa Sasa, Nawashauri Simba Kwa Hali ya timu Yao ilivyo sasa wasitarajie makubwa na baada ya mechi wakavunjika Moyo.

Mkuu kweli unaifananisha Simba SC na Ruvu Shooting?!

Katika mechi 7 zilizopita, Ruvu kadroo 2 na kafungwa 5... Halafu unasema kwa recent form hawana tofauti, kweli?!

Katika msimamo wa ligi unajua Simba SC yupo wapi na Ruvu yupo wapi, alafu unakuja unasema wanafanana, kweli?!

Nikifiria kauli ya Msemaji wenu aliyekolokoloni kuhusu mashabiki na wanachama wa Yanga SC, naomba niishie hapa.
 
Back
Top Bottom