FT: Ligi Kuu Bara | Ruvu Shooting 0-4 Simba SC | Stade de Benjamin Mkapa 19/11/2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
FULL TIME
90+3 Dakika tatu za nyongeza kuelekea kumalizika kwa mchezo
90' Phiri anapata nafasi anashindwa, shuti lake linapaa juu ya lango
77' Simba wanafanya mabadiliko, anaingia Kibu anatoka Bocco, anaingia Kennedy anatoka Onyango
Bocco anafunga goli la nne kwa Simba na la tatu kwake katika mchezo huu
68' Goooooooooooooooooooaaal
Onyango anapewa kadi ya njano kwa utovu wa niadhamu
52' Timu zote zinafunguka, huku Ruvu walijitoa mhanga kushambulia
50' Ruvu wamerejea na nguvu, wamefanya mashamulizi mawili makali
Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza

MAPUMZIKO

45' Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza
38' Mabadiliko kwa Simba, Akpan anaingia anatoka Kanoute ambaye ameumia
Shomari Kapombe anafunga kwa shuti akimalizia pasi ya Chama
36’ Goooooooooooooooooaaal
34’ Salum Kipaga wa Ruvu anapewa kadi ya njano
29’ Bocco anakosa nafasi ya wazi, shuti lake linapanguliwa na kipa
25’ Simba wanafanya mashambulizi mfululizo
22' Shambulizi kali langoni mwa Ruvu, shuti la Phiri linatoka nje
18' Goooooooooooooooooaaal
Bocco anafunga goli la pili akimalizia pasi ya Chama
13' Simba wanamiliki mpira, wanafika langoni mwa Ruvu lakini wanakosa umakini
03' Bocco Goooooooooooooaaal gooal John Bocco anatupia kambani bao la kwanza akimalizia kazi nzuri ya Chama
00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa Benjamin Mkapa

================

Vumbi la Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kutimka leo Novemba 19, 2022 ambapo Maafande wa Ruvu Shooting wanakiwasha dhidi ya Mnyama Mkali Mwituni Simba SC kwenye Uwanja wa Stade de Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Hii mechi huenda ikawa ya moto sana na ushindani wa kutosha ndani ya dimba kutokana na timu zote mbili kuwa na Makocha Malegendari wa Vilabu nchini Tanzania, Charles Mkwasa na Juma Mgunda.

Kocha Msaidizi wa Ruvu Shooting amesema haya kuelekea mchezo huo. "Tumetoka Uwanja wa mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo, Simba ni timu kubwa na bora tunawaheshimu lakini tutaingia kwa kushindana ili kupata matokeo chanya". Amesema Kocha Msaidizi wa Ruvu.

Naye Kocha wa Simba SC amesema haya kuelekea mchezo huo. "Maandalizi yanakwenda vizuri tuna mechi muhimu na ngumu na utakuwa mchezo wa ushindani, kuhusu Chama amerudi kundini anaendelea vizuri na kwa mapenzi ya mungu kesho (leo) atakuwa kwenye kikosi". Amesema Kocha wa Simba.

Ruvu Shooting Je, wapo tayari kuzuia malengo ya Simba na wao kupata ushindi au Boli Litatembea na wao Simba kupata ushindi.!? Dakika 90 za jasho na damu kuamua.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku. Usikose Ukaadithiwa Yaani.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
 
Siku ya kuendelea kuwakimbiza waleee na speed ya 5G.. Simba SC Mnyama Mkali Mwituni Nguvu Moja
 
Vumbi la Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Novemba 19,2022 ambapo Maafande wa Ruvu Shooting wanakiwasha dhidi ya Mnyama Mkali Mwituni Simba SC kwenye Uwanja wa Stade de Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Hii mechi huenda ikawa ya moto sana na ushindani wa kutosha ndani ya dimba kutokana na timu zote mbili kuwa na Makocha Malegendari wa Vilabu nchini Tanzania, Charles Mkwasa na Juma Mgunda.

Kocha Msaidizi wa Ruvu Shooting amesema haya kuelekea mchezo huo. "Tumetoka Uwanja wa mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo, Simba ni timu kubwa na bora tunawaheshimu lakini tutaingia kwa kushindana ili kupata matokeo chanya". Amesema Kocha Msaidizi wa Ruvu.

Naye Kocha wa Simba SC amesema haya kuelekea mchezo huo. "Maandalizi yanakwenda vizuri tuna mechi muhimu na ngumu na utakuwa mchezo wa ushindani, kuhusu Chama amerudi kundini anaendelea vizuri na kwa mapenzi ya mungu kesho (leo) atakuwa kwenye kikosi". Amesema Kocha wa Simba.

Ruvu Shooting wapo tayari kuzuia malengo ya Simba SC na kupata ushindi au Boli Litatembea na Simba SC kupata ushindi.!? Dakika 90 za jasho na damu kuamua.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku. Usikose Ukaadithiwa Yaani.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

Wewe Si Ndiye Uliyesemaga Mayele Hawezi Kufikisha Hata Goli 9 Msimu Huu, Sasa Ngojaa…
 
Mnyama mkali Simba Sc tafuna hao watoto wa Masau Bwire Ruvu Shooting.

SIMBA NGUVU MOJA
SIMBA BINGWA NBCPL 2022/2023
 
Wachezaji wanacheza kama walilazimishwa aisee, na leo utaona tofauti nyingine jinsi hizi timu zinavyocheza zinapokutana na Simba ila wakikutana na Yanga sasa oohh asalaleee
Huu si ushabiki ni ufala, mtu mwenye akili timamu na anayejua mpira atakuwa anajua aina ya mpira anaocheza Yanga, Aina ya wachezaji wake, mfumo wake na hata kujituma na umakini wa wachezaji wenyewe, Kocha wao na uzoefu walionao hasa ukizingatia wamekaa pamoja kwa muda mrefu.

Yanga huwezi linganisha na timu yoyote ile hapa Tanzania, hata pale wanapocheza viwanja vigumu huwa wanajilinda kwa ufasaha mf. Kagera Sugar.

Ni ujinga kuamini kuwa timu zinapocheza na Yanga hazijitumi, Last season Simba alifungwa na Yanga kwenye Ngao ya Jamii na alipigiwa pasi nyingi mno, na sio kwamba Simba hawajui mpira hapana, ila Yanga wana uwezo mkubwa kuliko Simba.

Huu ushabiki wa Kijinga haufai.
 
Sawa mkuu, lakini kweli ile mechi ya juzi na Singida uliwatazama vizuri wachezaji wa SBS na kisha pitia mechi zao zilizopita...
 
Back
Top Bottom