Rusumo, Ngara: Watu 8 wanashikkiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kuiba mafuta baada ya lori la mafuta kuanguka

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Jana kuna picha wa wananchi wa wilaya Ngara wakichota mafuta baada ya gari la mafuta kuanguka. Mkuu wa mkoa amemuagiza kamanda wa polisi mkoa Kagera kuwakamata wote waliochota mafuta na kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria.

***
Watu nane Wilayani Ngara wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za wizi wa mafuta katika gari lililopata ajali Kijiji cha Mshikamano maarufu Machinjioni, na kusababisha kifo cha dereva wa gari hilo

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema licha ya kukamatwa watu hao pia wamefanikiwa kukamata lita 300 za mafuta zilizokuwa zimeibwa katika tukio hilo

Kamanda amesema kuwa shughuli za ufaulishaji mafuta zinaendelea chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Police katika eneo la ajali hiyo lililopo njiani kabla ya kufika mpaka wa Rusumo

Pia soma
 
FB_IMG_15668331326901715.jpeg
 
Ingewekwa sheria na adhabu kali kwa wote watakao husika kuiba kwenye ajali na pia wakuu wa wilaya na mikoa wangekua wanawajibishwa, huu upuuzi usingekua unatokea.
 
Wapigwe anagalau mvua miezi 6 jela wakirudi akili iwakaye sawa.
Mtawalaumu sana watu na kuwafunga sana ila tatizo umasikini umekithiri. Mtu anaishi maisha ya kuunga unga leo amepata kesho hajapata halafu utegemee gari la mafuta lianguke asiende kuchota mafuta? Hiyo haiwezekani.
Awamu hii imejikita katika kuendeleza vitu na siyo watu. AJIRA MWENYEKITI WA CCM AMEZIFUTA UNATEGEMEA WATU WAISHIJE? LAZIMA WATU WACHOTE MAFUTA TU
 
Tatizo bindamu wa siku hizi ni wabishi sana...
Cc: mahondaw
Tatizo ni umasikini ndugu. Umasikini umewafanya watu wawe wabishi na sugu. Kuna watu wanaishi na wengine wanapambania maisha. Huyu anayepambania maisha, gari la mafuta likidondoka lazima akachote mafuta.
 
Back
Top Bottom