Russian-African Forum 2016: Tanzania & Zimbabwe

Russian-African Forum 2016: Tanzania & Zimbabwe

Urusi haitegemei mafuta na gesi tu; kuna teknolojia, viwanda vya uzalishaji pamoja na madini. Ndio nchi inayoongoza kuwa na hifadhi ya madini ya almasi duniani, pamoja na madini ya vito aina ya alexandrite ambayo kwa mara ya kwanza yalipatikana Urusi. Jaribu kupitia taarifa mbali mbali, utafahamu mengi kuhusu taifa hili.
mkuu cjui kama ulifatilia ile world econonomic forum ya davos 2016,utaona kwamba among mataifa makubwa russia ipo mbali sana katika zile inovative economies,pia hata rais putin huwa daily anawambia wananchi wake russia needs to diversify uchumi wake ili waweze ku compete na west,pia jaribu kuangalia kwann uchumi wa uchumi wa russia uko na misukosuko sasa hivi? utaona ni kwasababu ya sanctions,lakin la pili kubwa ni kuporomoka kwa bei ya gas na mafuta...lakin pia kuhusu madini ya natural resources zngne c russia tu alie nazo,hata marekan wana mafuta mengi na gas nyingi sana,lakini wao huwa wananunua mafuta kutoka nchi nyingne kwa sababu kiktiba walizuia kuuza mafuta yao nje mpk kufkia mwaka jana....
 
Urusi haitegemei mafuta na gesi tu; kuna teknolojia, viwanda vya uzalishaji pamoja na madini. Ndio nchi inayoongoza kuwa na hifadhi ya madini ya almasi duniani, pamoja na madini ya vito aina ya alexandrite ambayo kwa mara ya kwanza yalipatikana Urusi. Jaribu kupitia taarifa mbali mbali, utafahamu mengi kuhusu taifa hili.
hivi we unafikiri marekani wao hawana hizo gas na mafuta?? wanazo lakini wanafanya biashara nyingn nying sana.yaan uchumi wao haupo umeelemea sekta flan flan tu...usikatae kuhusu uchumi wa russia kutegemea sana mafuta na gas we kaangalie kwe total GDP yao mafuta na gas yanachangia asilimia ngapi mkuu utaona.......pili muu wala usibishe sana mbona uchumi wa russia ni mdogo sana hata kwa uchumi wa ufaransa tu....labda tu kwakuwa hata muasis wa taifa letu aliegemea upande huo wa mashariki lakini kwenye swala la kujenga partnership ya kiuchumi nchi kama japan can give us more than russia can do..uwezo wa uchumi au wa biashara wa nchi unaupima hata kwa idadi ya makampuni yake yanayofanya biashara kwenye nchi zingine..idadi ya kampuni za japan,german,china,USA,UK, hata india zilizopo nchini kwetu ni nyingi mno huwez kulinganisha na kampuni za urusi zilizopo huku tanzania ambazo hata hatujazizoea kabisa hili linaonyesha mzunguko wa biashara wa kampuni za nchi hii ni mdogo kuliko nchi hizo nlizozitaja,kwahio mkuu hio patnership na russia ni kweli itatusaidia lakini ni kidogo sana ukilinganisha na ushirkiano na nchi hizo nlizozitaja.hasahasa USA,JAPAN na CHINA,russia inafanya vizuri kwenye oil,gas na arms industry ila kwingneko still iko far ukilinganisha na na nchi hizo
 
mkuu cjui kama ulifatilia ile world econonomic forum ya davos 2016,utaona kwamba among mataifa makubwa russia ipo mbali sana katika zile inovative economies,
Unapozungumzia innovative economies ni uwezekano wa nchi kupiga hatua za kimaendeleo baada ya muda fulani kutokana na ubunifu wa sera, teknolojia na kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji. Hii tunaweza kusema ni makisio ya kiuchumi baada ya kipindi fulani. Mimi nasema wakati uliopo, Urusi iko katika nasafi gani kiuchumi.?? Jaribu kupitia taarifa za IMF na world bank..
pia hata rais putin huwa daily anawambia wananchi wake russia needs to diversify uchumi wake ili waweze ku compete na west,
Hizo ni sera za kiuchumi jinsi ya kuendana na kasi ya dunia. Ili kuhimiri ushindani wa kibiashara na mageuzi ya kisayansi ni lazima sera ziendane na wakati uliopo.
pia jaribu kuangalia kwann uchumi wa uchumi wa russia uko na misukosuko sasa hivi? utaona ni kwasababu ya sanctions,lakin la pili kubwa ni kuporomoka kwa bei ya gas na mafuta...
Kweli, mafuta na gesi bei zake zimeshuka na mapato yatakashuka vile vile lakini sio kuporomoka. Katika sekta ya uchimbaji, huwa tunaangalia ni jinsi gani shughuli ya uchimbaji imesaidia kuendeleza sekta nyingine kiuchumi. Ndio maana leo Urusi ni wabunifu katika teknolojia, viwanda na nishati kutokana na fedha ya uwekezaji kupatikana kutoka kwenye machimbo ya madini, gesi na mafuta.
lakin pia kuhusu madini ya natural resources zngne c russia tu alie nazo,hata marekan wana mafuta mengi na gas nyingi sana,lakini wao huwa wananunua mafuta kutoka nchi nyingne kwa sababu kiktiba walizuia kuuza mafuta yao nje mpk kufkia mwaka jana....
Mkuu, huwa tunaangalia ubora na sio uwingi. Aina ya mafuta yanayopatikana Amerika ni Oil Shale, ubora wake ni mdogo. Kwa hiyo inahitajika gharama na hatua nyingi za uchenjuaji ili kupata bidhaa iliyokamilika. Higher production costs tend to lower profit ratio. Ndio maana serikali na makampuni mengi ya Amerika yanajihusisha zaidi kutafuta malighafi ya mafuta nje ya nchi.
 
hivi we unafikiri marekani wao hawana hizo gas na mafuta??
Wanazo, sema aina ya machimbo waliyonayo ni Oil Shale. Yaani hata gesi iliyopatikana Tanzania ina ubora zaidi ya Amerika. Kampuni nyingi zinashindwa kuchimba huko sababu ya uwekezaji wake kuwa mkubwa katika kuzalisha.
wanazo lakini wanafanya biashara nyingn nying sana.yaan uchumi wao haupo umeelemea sekta flan flan tu...
Biashara kubwa halali wanayotegemea na inayoendelea kuwalipa ni uuzaji wa silaha, ubunifu wa intaneti na mitandao. Sekta nyingine zimeshikiliwa na mataifa mbali mbali. Kingine kinachowalipa zaidi ni vita wanayopigana kwenye nchi tofauti tofauti.
usikatae kuhusu uchumi wa russia kutegemea sana mafuta na gas we kaangalie kwe total GDP yao mafuta na gas yanachangia asilimia ngapi mkuu utaona.......
Sijakataa, lakini tofauti na gesi Urusi pia ina madini mengi. Madini ya vito kama Alexandrite, ndio madini yenye gharama kubwa duniani. Leo hawa jamaa hawajaanza hata kuchimba hifadhi yao ya almasi..
pili muu wala usibishe sana mbona uchumi wa russia ni mdogo sana hata kwa uchumi wa ufaransa tu....
Uchumi wa Ufaransa sio wa kubeza kiasi hicho, nimekwambia jaribu kupitia taarifa za IMF na WB utazame Urusi iko nafasi ya ngapi kiuchumi duniani.
labda tu kwakuwa hata muasis wa taifa letu aliegemea upande huo wa mashariki lakini kwenye swala la kujenga partnership ya kiuchumi nchi kama japan can give us more than russia can do..
Hapana, maamuzi ya leo hayafanani na miaka 50 iliyopita. Dunia imebadilika kwa kila kitu kuanzia siasa hadi teknolojia. Kinachotizamwa zaidi ni sera ya uwekezaji na uwezo katika sekta husika. Tazama hapo juu, sekta walizozianisha katika mkutano ujao. Halafu linganisha na uwezo wa Japani katika sekta hizo.
uwezo wa uchumi au wa biashara wa nchi unaupima hata kwa idadi ya makampuni yake yanayofanya biashara kwenye nchi zingine..idadi ya kampuni za japan,german,china,USA,UK, hata india zilizopo nchini kwetu ni nyingi mno huwez kulinganisha na kampuni za urusi zilizopo huku tanzania ambazo hata hatujazizoea kabisa
Mkuu mazoea yana nafasi gani katika sera za uwekezaji.?? Tofauti na kuwa na biashara za silaha na ukachelo wa kisiasa kipindi cha ujamaa na ukomunisti. Urusi haikuwahi kufanya biashara nyingine na nchi za kiafrika.
hili linaonyesha mzunguko wa biashara wa kampuni za nchi hii ni mdogo kuliko nchi hizo nlizozitaja,kwahio mkuu hio patnership na russia ni kweli itatusaidia lakini ni kidogo sana ukilinganisha na ushirkiano na nchi hizo nlizozitaja.hasahasa USA,JAPAN na CHINA,
Jaribu kufafanua zaidi mzunguko wa biashara katika uwekezaji unakuwaje.?? Na mchango wa Urusi utakuwaje mdogo ukilinganisha na nchi ulizozitaja.?? Kwa sababu hiyo miradi itakayozungumziwa ni larger scale na itakuwa multinationals ikuhusisha na nchi nyingine kama nishati na uchimabji wa gesi. Leo Urusi wanajenga gas plant nchini Uganda, wanafungua mgodi wa nickel nchini Burundi, wanaendesha miradi mingi nchini Namibia na nchi nyingi za kiafrika.
russia inafanya vizuri kwenye oil,gas na arms industry ila kwingneko still iko far ukilinganisha na na nchi hizo
Ndio maana watakuja na vipaumbele vya kwenye gesi, mafuta, madini na nishati. Hauwezi kuwekeza kwenye viwanda bila ya kuwa na nishati ya uhakika. Na jambo jingine umeona nchi za magharibi zilivyojaribu kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu, kwa kigezo cha misaada.!! Urusi hawana utaratibu huo.
 
Unapozungumzia innovative economies ni uwezekano wa nchi kupiga hatua za kimaendeleo baada ya muda fulani kutokana na ubunifu wa sera, teknolojia na kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji. Hii tunaweza kusema ni makisio ya kiuchumi baada ya kipindi fulani. Mimi nasema wakati uliopo, Urusi iko katika nasafi gani kiuchumi.?? Jaribu kupitia taarifa za IMF na world bank..

Hizo ni sera za kiuchumi jinsi ya kuendana na kasi ya dunia. Ili kuhimiri ushindani wa kibiashara na mageuzi ya kisayansi ni lazima sera ziendane na wakati uliopo.

Kweli, mafuta na gesi bei zake zimeshuka na mapato yatakashuka vile vile lakini sio kuporomoka. Katika sekta ya uchimbaji, huwa tunaangalia ni jinsi gani shughuli ya uchimbaji imesaidia kuendeleza sekta nyingine kiuchumi. Ndio maana leo Urusi ni wabunifu katika teknolojia, viwanda na nishati kutokana na fedha ya uwekezaji kupatikana kwenye machimbo ya madini, gesi na mafuta.

Mkuu, katika sekta ya madini, gesi na mafuta huwa tunaangalia ubora na sio uwingi. Aina ya mafuta yanayopatikana Amerika ni Oil Shale, ubora wake ni mdogo. Kwa hiyo inahitajika gharama na hatua nyingi za uchenjuaji ili kupata bidhaa iliyokamilika. Higher production costs tend to lower profit ratio. Ndio maana serikali na makampuni ya Amerika yanajihusisha zaidi kutafuta malighafi ya mafuta nje ya nchi.
sawasawa mkuu,so katika USA,china,japan,german,france,UK .........RUSSIA unaiweka katika position gani kwa nguvu ya uchumi wake......maana mi sifikiri km russia can be of help more than these countries..hio ndo point yangu.......maana siamini kama kiuchumi russia inaizidi hata nchi moja hapo juu nafikiri ina rank ya tisa ama ya kumi hivi duniani..mi naona tukiwa na patnership nao tutafaidika sawa tu na patnership na nchi kama south korea
 
it sounds okay, but we must do it with caution, as we all know when the Russians enter your house by the door the US enter through the windows. the consequences are beyond repair.
 
sawasawa mkuu,so katika USA,china,japan,german,france,UK .........RUSSIA unaiweka katika position gani kwa nguvu ya uchumi wake......
Narudia tena jaribu kutazama orodha za nchi kiuchumi kupitia data za world bank na IMF.
maana mi sifikiri km russia can be of help more than these countries..hio ndo point yangu.......
Huwezi kufikiria tofauti wakati data zinapatikana.
maana siamini kama kiuchumi russia inaizidi hata nchi moja hapo juu nafikiri ina rank ya tisa ama ya kumi hivi duniani..
teh teh teh utaamini vipi wakati huna data sahihi kutoka kwenye vyanzo sahihi.?? Umetumia vigezo gani hadi kufikia hitimisho lako.??
mi naona tukiwa na patnership nao tutafaidika sawa tu na patnership na nchi kama south korea
Sio kweli, kwa sababu mafanikio ya uhusiano wa kimaendeleo hayapimwi kwa uwezo wa nchi moja wapo. Kinachoangaliwa ni sera za maendeleo baina ya nchi mbili. Ndio maana China imefanya mambo makubwa sana katika kipindi cha miaka 20 tu, kuliko Uingereza iliyokuwepo zaidi ya miaka 50.
 
it sounds okay, but we must do it with caution, as we all know when the Russians enter your house by the door the US enter through the windows. the consequences are beyond repair.
Of course, we must be aware from both sides. This will be an ideal place to start in educating children in hopefully near future classrooms of the history not told in current history books. As we all know, history is told by victors and until we are taught and learned the true history.
 
Of course, we must be aware from both sides. This will be an ideal place to start in educating children in hopefully near future classrooms of the history not told in current history books. As we all know, history is told by victors and until we are taught and learned the true history.
exactly and the tide is turning into Africa, where the three world giants are converging to harness the untapped resources with all means,
I remember two statements from French government and British crown in 1880s over the fashoda to their generals respectively.
1. The crown to Lord kitchner. "We are claiming for the Sudan by way of conquest because it is the easiest and the most simplest way."
2. French to General Machand " You are going to fire pistol shot at Fashoda, we are agree all the consequences"

we too must be aware of this.
 
Narudia tena jaribu kutazama orodha za nchi kiuchumi kupitia data za world bank na IMF.

Huwezi kufikiria tofauti wakati data zinapatikana.

teh teh teh utaamini vipi wakati huna data sahihi kutoka kwenye vyanzo sahihi.?? Umetumia vigezo gani hadi kufikia hitimisho lako.??
Sio kweli, kwa sababu mafanikio ya uhusiano wa kimaendeleo hayapimwi kwa uwezo wa nchi moja wapo. Kinachoangaliwa ni sera za maendeleo baina ya nchi mbili. Ndio maana China imefanya mambo makubwa sana katika kipindi cha miaka 20 tu, kuliko Uingereza iliyokuwepo zaidi ya miaka 50.
orodha ya kiuchumi ndo hio ambayo russia haipo hata top 7 ya nchi zenye uchumi mkubwa au we unataka data gani?? nambie basi hio source ambayo russia ipo below number 5 kwa ukubwa wa uchumi nami nkaisome...mi najua iko nyuma kwa wenzie na ndo mana hata hizo conference na huku africa anakumbuka now.....
 
orodha ya kiuchumi ndo hio ambayo russia haipo hata top 7 ya nchi zenye uchumi mkubwa au we unataka data gani?? nambie basi hio source ambayo russia ipo below number 5 kwa ukubwa wa uchumi nami nkaisome...
Rank Country GDP (Millions of Int$) Year (2014)

World 108,777,213

23px-Flag_of_Europe.svg.png
European Union
[n 1] 18,640,411
1
23px-Flag_of_the_People%27s_Republic_of_China.svg.png
China 18,088,054
2
23px-Flag_of_the_United_States.svg.png
United States 17,348,075
3
23px-Flag_of_India.svg.png
India 7,411,093
4
23px-Flag_of_Japan.svg.png
Japan 4,767,157
5
23px-Flag_of_Germany.svg.png
Germany 3,748,094
6
23px-Flag_of_Russia.svg.png
Russia 3,576,841
7
22px-Flag_of_Brazil.svg.png
Brazil 3,275,799
source: http://data.imf.org/?sk=7CB6619C-CF87-48DC-9443-2973E161ABEB

Rank Country GDP (Billions of Int$) Year (2014)

World 108,464

23px-Flag_of_Europe.svg.png
European Union
[n 1] 18,423
1
23px-Flag_of_the_People%27s_Republic_of_China.svg.png
China 18,031
2
23px-Flag_of_the_United_States.svg.png
United States 17,419
3
23px-Flag_of_India.svg.png
India 7,393
4
23px-Flag_of_Japan.svg.png
Japan 4,631
5
23px-Flag_of_Russia.svg.png
Russia 3,745
6
23px-Flag_of_Germany.svg.png
Germany 3,690
7
22px-Flag_of_Brazil.svg.png
Brazil 3,264
source: Data | The World Bank
Kila kitu ni maamuzi, miaka ya 2000 nafasi ya India kiuchumi ilikuwa haipo. Lakini sasa hivi ni taifa linalozalisha "stainless steel" chuma cha pua kwa wingi duniani. Nafasi iliyokaliwa na Ujerumani kwa kipindi kirefu. Kwa hiyo hata Urusi ana nafasi kubwa, hasa ukizingatia alishawahi kuwa dola kuu duniani.
mi najua iko nyuma kwa wenzie na ndo mana hata hizo conference na huku africa anakumbuka now.....
Urusi ni nchi kubwa na yenye rasirimali nyingi. Na sera za nje za Urusi zimeegemea zaidi katika kutafuta ushawishi wa kisiasa kuliko malighafi. Afrika ni turufu, hauwezi kuwa dola kuu duniani bila ya kuwa na ushawishi kutoka bara la Afrika. Ndio maana Amerika na China walishatangulia kufanya hivyo hapo mwanzo.

Tazama orodha ya nchi zilizoorodheshwa hapo juu, utangundua nchi nyingi kupitia vyama vyao vya ukombozi vilikuwa na malengo ya kijamaa na kikomunisti, sera ambayo ni ya mataifa ya mashariki. Hata Afrika ya Kusini ilipata uhuru wake kwa msaada wa Urusi kupitia serikali ya Tanzania. Kwa hiyo Urusi anapojaribu kurudi, anarudi kwa mara ya pili.
 


+7 (495) 268-07-87


© 2016 Russian-African Forum (RAF)












BUSINESS FORUM PROGRAM
Russian-African Forum, Tanzania
April 27-28, 2016


April 27
(Wednesday)

Options:
• Business meetings – Russian companies with Tanzanian Ministries
• Business meetings - Russian companies with Tanzanian companies
• Visit to EPZA
• Visit to Ubungo II plant (TANESCO)
• Visit organized by TRL and TPA


April 28
(Thursday) : 10.00 - 19.00 Welcome remarks by Permanent Secretary, Ministry of Industry, Trade and Investment – Tanzania
Remarks by Executive Director of Tanzania Private Sector Foundation
Moderator: Raymond Mbilinyi. Executive Secretary, Tanzania National Business Council (TNBC)

Arrival and registration

Welcome tea/coffee

Round table – Transportation Engineering
«Infrastructure projects and localization of transport engineering products"

We would like to open a discussion on product localization and the launching of dealerships and service centres for transport engineering. Due to it’s good geographical location and economy development Tanzania might become the centre for servicing the EAC market (5 countries) and the SADC market (15 countries), as Tanzania is a member of both Communities and actively developing port infrastructure supporting import and further distribution of goods to African countries

Moderator: Ekaterina Dyachenko, Founder of B2B-Export Group

Venue: Julius Nyerere Convention Center

Language: English

Russian Participants:

Sukhoj Civil Aircraft

Irkut

United Wagon Company

Kamaz

Tanzanian participants:

Tanzania Ports Authority (TPA)

Railways Asset Holding (RAHCO)

TANROADS

Tanzania Railway Limited

Tanzania Civil Aviation Authority (TAA)

Motisun Group of Companies

Comafric Group of Companies

Turky's Group of Companies

Quality Group


Round Table - Agriculture "Green revolution in Africa - agriculture development projects"
Agriculture remains the mainstay of the Tanzanian economy, employing the majority of the workforce. Given the rapidly growing world population and the fact that the African continent has the largest share of the world’s uncultivated land, there is a room for agriculture to expand in a sustainable way to meet the growing world demand.This session is to present an overview of the agricultural situation and projects in Tanzania to the participants, to create an opportunity to meet Russian producers and to promote international cooperation.

Russian participants:

Rostselmash

Chelyabinsk Tractor Plant

Melinvest

Avgust

Edagum

Tanzanian participants:

The National Food Reserve Agency (NFRA)

Center for Agricultural and Rural Technology

Plenary session «Russia and Tanzania - it takes two to tango»
The Russian-African Forum is to open to discussions on the cooperation of Tanzanian and Russian companies, to provide an opportunity for Russian companies, financial and government authorities to get a better understanding of the Tanzanian economy and to create mutual collaboration.
Moderator: Ekaterina Dyachenko, Founder of b2b-export.com
  • Welcoming Remarks: Hon. Charles Mwijage (MP), Minister for Industry, Trade and Investments, United Republic of Tanzania

  • Welcoming Remarks by Hon. Denis Manturov, Minister for Industry and Trade, Russian Federation

  • Remarks by Alexander Ruchyov, President of Morton Group, Russian Federation

  • Remarks by Nehemiah Kyando Mchechu, Director General of National Housing Corporation, United Republic of Tanzania

  • Remarks by Raffaele Tomaino, Vice President of Sales of JSC "Sukhoi Civil Aircraft", Russian Federation

  • Remarks by Marina Neronova, Overseas Sales Director of OJSC "Power Machines", Russian Federation

  • Remarks by Eng. Felichesmi Mramba, Managing Director of Tanzania Electric Supply Company (TANESCO), United Republic of Tanzania

Briefing for mass media

Round table – “Investment opportunities for Russian companies in Tanzania”
The roundtable is devoted to a practical discussion on investment opportunities and climate in Tanzania, financial instruments available for African companies working with Russian companies on power, transport and other types of infrastructure development.

Moderator: Juliet Kairuki, Executive Director, Tanzania Investment Centre (TIC)

Tanzanian participants:
TANESCO

STAMICO

TPDC (Tanzania Petroleum Development Corporation)

Tanzania Geothermal Development Company Ltd

Rural Energy Agency (REA)

Drilling and Dam Construction Agency

Motisun Group of Companies

Edenville International (Tanzania) Ltd.

Simba Oil Company Ltd.

Russian participants:

Power Machines

Rotek

Inter RAO

Metprom

Round Table – Energy «Powering Tanzania – development in the energy sector»
Russia is the world's leading natural gas exporter. Besides Russia is the world's fourth largest electricity producer after the USA, China, and Japan. Roughly 63% of Russia's electricity is generated by thermal plants, 21% by hydropower and 16% comes from nuclear reactors.The round table is aimed to drive forward the industry and to provide detailed insights into valuable partnerships between Tanzanian and Russian power sector companies.

Moderator: Ekaterina Dyachenko, Founder of B2B-Export Group

Russian participants:

Morton

Veya Investments

VEB

Farexpo

Tanzanian participants:

Export Processing Zones Authority (EPZA)

National Development Cooperation (NDC)

National Housing Corporation (NHC)

Tanzania Buildings Agency

Edenville International (Tanzania) Ltd.

Simba Oil Limited

Turky's Group of Companies

Sea View Development Ltd.

Motisun Group of Companies

Quality Group

Business meetings and networking

Sukhoi Superjet 100 presentation (by invitation only)
 
Hapa wasaidie Energy Sector, mining and Revamping our obsolete industries.
Baada ya kufanikisha hili then waje tuzungumzie Sukhoi, MiG , Armata na S300.
😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀
Gu-Nyani Ngabu gukiona hii lazima ni gutamani kufa.

CC: Dotworld
 
Back
Top Bottom