Mimi huwa nasema siku zote huwezi kuendelea na kuheshimika kama utakuwa
na mtazamo tegemezi. Hii ni katika kila kitu... tekinolojia, uchumi, elimu n.k.
Sasa Russia ili kuonyesha mabavu na ushashawishi katika eneo la ulaya mashariki
na baadae dunia nzima nilazina wasiwe tegemezi.
Ingeshangaza kama wao wanataka kuwa taifa kubwa wakati software wanazo
tumia katika nyanja za kitaifa ni za kampuni ya microsoft. Sasa kama microsoft
watashinikizwa na uncle Sam kutouza Russia si watakuwa wameliwa?
Huyu jamaa anamkakati wa nguvu kujenga nchi yake na we ngoja tuu muda wa
medvedev uishe ili mwenyewe aingie uone.