Russia leo ndio deadline ya nchi adui kulipia kwa Dola na Yuro

Malaika Mkuu

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
901
907
Mwisho leo

Leo Alhamis ya tarehe 31 Machi 2022 ndio mwisho uliotangazwa kwa nchi maadui wa Russia kulipia gesi, mafuta na bidhaa zake kwa pesa za Dola na Yuro Au pesa nyengine yeyote isipokuwa Rubo. Rubo ni pesa za Urusi na kuwa Rais Putin anasema kutokana na hatua za kiadui za nchi hizo sasa ni lazima wanaotaka gesi na mafuta yake walipe kwa fedha zake.

Huko Ulaya matumbo joto. Waziri wa Uchumi wa Ungereza amepatwa na tumbo la kuhara. Waziri wa Uchumi wa Ujerumani ameripotiwa akiwataka wananchi kuanza kufunga mkanda na kupunguza matumizi haraka. Ameitisha kikao cha dharula cha kujadili janga hilo. Euro News Now wanaripoti kuwa “German economy minister urges consumers and businesses to cut back: ‘every kilowatt hour counts’

Wakati hayo yakitokea hali halisi ya mapigano haiwekwi hewani kisawia na vyombo vya magharibi. Endapo majeshi ya Urusi wangeua raia kama inavyodaiwa wananchi (pichani) wangeogopa na kukimbia. Lakini inaonekana wazi kuwa wanaokimbizwa ni wanajeshi wa Ukraine. Pia nchini Uturuki majadiliano ya kusitisha vita kati ya Urusi na Ukraini yamefikia muafaka wa kuifanya Ukraini nchi huru isiyofungamana na upande wowote (kwa maana kuwa haitojiunga NATO wala kushirikiana na Marekani kijeshi) huku ikikubali pia matakwa ya kuitambua Crimea kuwa sehemu ya Urusi na Majimbo ya Donetsk na Luhansk kama nchi huru. Taarifa zinazotifikia watetezi wa haki duniani zinathibitisha makubaliano haya yanayolenga kuokoa mamilioni ya raia wa Ukraine kutokana na Kipigo cha Urusi.

Miji iliyozingirwa na ile isiyozingirwa haina tofauti kutokana na Urusi kutumia makombora yake ya masafa ya kati kuangamiza maeneo lengwa yenye maslahi ya kijeshi ya Ukraini na nchi za magharibi. Wakati taarifa za magharibi zikisema makombora ya Urusi yamepiga hospitali mjini Meruipol taarifa za kijeshi za Urusi zinaonesha waliouawa ni askari wa mataifa ya kigeni waliokuwa kwenye mafunzo toka kwa wakufunzi wa nchi maadui.

Zaidi ya askari mamluki 300 wameuawa kwenye shambulio hilo. Jana askari wengine 200 na ushee wameuawa kwenye shambulizi kama hilo mjini Kharkiv ambako imethibitishwa n Urusi kuwa walikuwa mgambo mamluki waliokuwa wanafundishwa na Ungereza.

Wakati hayo yakiendelea Spika wa Bunge la Urusi (Duma) ametaka hata biashara za Mazao na Mbolea toka Urusi kwenda mataifa adui zifanyike kwa Rubo.

“Russia’s top lawmaker suggests fertiliser, grain and other commodities should also be paid for in roubles” Jambo hilo ghafla limezua taharuki na kuoanda kwa bei sio tu za mafuta na gesi huko Ulaya bali pia za ngano na mbolea. Nchini Ujerumani pekee ongezeko la jumla la bei limepanda kwa kiwango kisichowahi kushuhidiwa kwa zaidi ya miaka 41 hadi kufikia 7.3%

Ungereza imeitisha kikao cha dharula cha nchi za Ulaya kujadili ongezeko la bei za mbolea.

Endapo Urusi itatekeleza sharti lake la kuzuia mauzo kwa nchi hizo bila malipo ya Rubo huenda ikaleta maafa sana haswa kipindi hiki chenye baridi bara Ulaya.

Kitabu cha Bunge la Tanzania kitazinduliwa hivi punde kitakupa pia historia inayofichwa ya mahusiano ya kiutawala na uchumi kwa nchi za Tanzania Kenya na Uganda tangu tawala za asili za Kilwa, Baganda na Mlima Kenya hadi kufikia hali iliyopo sasa Bungeni Tanzania. Hakikisha unaweka oda yako sasa kupitia +255712417307.

Dr. Albanie Marcossy.
 
Putin hatoweza salia madarakani one man must be eliminated for safety of world. Stay tune.
 
Pro USA 🇺🇸 tumejificha muda huu, matumbo yanaunguruma kama tumemeza vyura, wapi wanauza Andrews tukanunue?

1648714646927.png
 
Avatar Yako Haifanani na ulichokiandika mkuu
Sifanani kivipi mkuu?
Inamaana unaona ni utani niliyoandika au huamini!
Ngoja nikuletee links .
Siko hivyo!

Europe — for now​

PUBLISHED THU, MAR 31 20223:37 AM EDT
thumbnail

Sam Meredith@SMEREDITH19
WATCH LIVE
KEY POINTS
  • In a call with German Chancellor Olaf Scholz on Wednesday, Russia’s Vladimir Putin said European companies could continue paying for gas supplies in euros or dollars.
  • Meanwhile, Kremlin spokesman Dmitry Peskov on Wednesday confirmed Russia would not be seeking gas payments in rubles immediately, saying instead that this switch is likely to be a “gradual process.”
  • Germany, alongside the G-7 nations, has signaled gas supply agreements cannot be unilaterally modified and European buyers of Russian gas say the Kremlin is not entitled to redraw long-term contracts.
 
Russia amekubali malipo kwa kutumia EURO ..nakuhabarisha!
Mkuu jana Kansera wa Ujerumani alimpigia simu Putin na kumwambia ya kwamba tangazo hilo ni la ghafla mno lina hitaji muda kulitekeleza ndio maana Putin akaruhusu mfumo wa kwanza kuendelea wakati waki tafuta ufumbuzi.
 
Mwisho leo

Leo Alhamis ya tarehe 31 Machi 2022 ndio mwisho uliotangazwa kwa nchi maadui wa Russia kulipia gesi, mafuta na bidhaa zake kwa pesa za Dola na Yuro Au pesa nyengine yeyote isipokuwa Rubo...
Kipindi Cha barid kimeshaisha sahivi ni spring, alafu pia urussi ata loose sababu asilimia 30 ya revenue vya urusi inatokana na gesi na mafuta
 
Avatar Yako Haifanani na ulichokiandika mkuu

Europe — for now​

PUBLISHED THU, MAR 31 20223:37 AM EDT

thumbnail

Sam Meredith@SMEREDITH19
WATCH LIVE
KEY POINTS
  • In a call with German Chancellor Olaf Scholz on Wednesday, Russia’s Vladimir Putin said European companies could continue paying for gas supplies in euros or dollars.
  • Meanwhile, Kremlin spokesman Dmitry Peskov on Wednesday confirmed Russia would not be seeking gas payments in rubles immediately, saying instead that this switch is likely to be a “gradual process.”
  • Germany, alongside the G-7 nations, has signaled gas supply agreements cannot be unilaterally modified and European buyers of Russian gas say the Kremlin is not entitled to redraw long-term contracts.
 
Vizuri ila Luna m
Mkuu jana Kansera wa Ujerumani alimpigia simu Putin na kumwambia ya kwamba tangazo hilo ni la ghafla mno lina hitaji muda kulitekeleza ndio maana Putin akaruhusu mfumo wa kwanza kuendelea wakati waki tafuta ufumbuzi
Ahsante! Kuna mdau hapo ambaye naamini hafuatilii alikuwa haamini hii taarifa .afadhali ya wewe unafuatilia na upo updated!
Vizuri kwa usahihisho.
 
Sifanani kivipi mkuu?
Inamaana unaona ni utani niliyoandika au huamini!
Ngoja nikuletee links .
Siko hivyo!

Europe — for now​

PUBLISHED THU, MAR 31 20223:37 AM EDT
thumbnail

Sam Meredith@SMEREDITH19
WATCH LIVE
KEY POINTS
  • In a call with German Chancellor Olaf Scholz on Wednesday, Russia’s Vladimir Putin said European companies could continue paying for gas supplies in euros or dollars.
  • Meanwhile, Kremlin spokesman Dmitry Peskov on Wednesday confirmed Russia would not be seeking gas payments in rubles immediately, saying instead that this switch is likely to be a “gradual process.”
  • Germany, alongside the G-7 nations, has signaled gas supply agreements cannot be unilaterally modified and European buyers of Russian gas say the Kremlin is not entitled to redraw long-term contracts.
Hizi ni habari mbaya kwa Warusi wa Tabata Kisukuru.
 
Back
Top Bottom