Rushwa ya ngono vyuoni

Vitalis Konga

Senior Member
Sep 22, 2018
127
231
Bila shaka wana JF mtakuwa hamjambo,naomba nisipoteze muda niende moja kwa moja kwenye....

Tangu siku ya tarehe 28 Novemba 2018 ambapo Rais wa JMT Dr. John Magufuli alizindua maktaba mpya katika Chuo Kikuu cha Dar Es Saalam (UDSM), mjadala wa tangu siku hiyo si Maktaba iliyozinduliwa bali ni tuhuma alizoibua mmoja ya wahadhiri wa UDSM, Mwanamama Dr. Vicensia Shule akidai kuwa UDSM kuna rushwa ya ngono iliyokithiri, hivyo yeye alibeba bango kufikisha ujumbe kwa ndugu Rais lakini aliogopa walinzi wake (hata miye kwakweli waliniogopesha Novemba 1, nilipohudhuria Kongamano la Uchumi pale Nkurumah Hall-UDSM) hivyo alishindwa!

Mama, Dr. Vicencia Shule aliibua hoja ya ukatili wa kijinsia wanaofanyiwa wanafunzi wa kike chuoni hapo, aliibua madai ya wahadhiri kudai rushwa ya ngono kwa wanafunzi ili kuwasaidia katika masomo hususani kuwapa alama za juu kwenye mitihani yao, ikumbukwe Chuo Kikuu Mwalimu wa somo husika ndiye msahihishaji wa majaribio yote mawili (Test 1 and Test 2), Kazi za Darasani (Assignments) na mtihani wa Mwisho (Final or UE) hivyo ana Mamlaka makubwa na akiamua usifaulu haufalu na akiamua ufaulu hata kama huna uwezo wa kufaulu utafaulu tu, kwasasa yeye ndiyo mtu wa mwisho katika kila alama zako za somo!

Tuhuma hizo za Dr. Vicensia Shule zimepokelewa kwa hisia tofauti kutoka makundi mawili (kwa mtizamo wangu), kuna kundi la kwanza linalounga mkono na na kumpongeza na kundi la pili ni lile linalopinga kwa madai kuwa hicho kitu hakipo. Kiongozi mmoja wa serikali alifika mbali kwa kuandika ujumbe kwenye mtandao wa twitter akisema 'kuna mtu ametumwa kukichafua chuo kikuu UDSM. Hatafanikiwa' --- hapo ni dhahiri alimlenga Dr. Vicensia Shule si mwingine!

Kwanza jamii ni lazima itambue historoa kidogo ya Mhadhiri huyu, Dr. Vincensia Shule, kwanza kabisa Mhadhiri wa UDSM tangu mwaka 2000, alipochaguliwa kuwa baada ya kuhitimu shahada yake ya kwanza (Bachelor Degree) chuoni hapo. Baadae alisoma shahada ya uzamili (Masters) hapo hapo UDSM na kuhitimu mwaka 2004. Kwa kifupi Dr. Vicensia Shule yupo UDSM tangu mwaka 1997 alipojiunga akiwa Mwaka wa Kwanza. Hivyo mpaka sasa ana miaka 21 UDSM!

Mwaka 2007 alijiunga na Chuo Kikuu cha Johannes Gutenberg Mainz, nchini Ujerumani, kusoma shahada ya uzamivu ya Sanaa na Uandaaji wa filamu (PhD in Theatre and Film). Na baada ya PhD yake ameendelea kuwa Mhadhiri wa UDSM hadi leo, hivyo kutoka mwanafunzi wa mwaka kwanza 1997 hadi sasa kuwa Mhadhiri Mwandamizi, Dr. Vicensia Shule ameona na kusikia mengi pale UDSM, na mpaka imefikia amesema basi ujue imekithiri Kweli kweli, sasa inapotokea anakejeliwa, anatukanwa matusi mazito hii ni kuonesha jamii yetu imekuwa ya kupuuza mambo ya msingi, Dada zetu, Shangazi zetu, wadogo zetu na watoto wetu wananyanyaswa na mtu ambaye yupo Kwenye hivyo viunga kwa miongo miwili anatusaidia kupaza sauti tunampinga kwa kumtusi na lugha zisizo!

Nimekaa nakitafakari 'Kama Mhadhiri Mwandamizi anapingwa hivi, anaonekana mwongo, mzushi na mchonganishi vipi kwa Binti wa mwaka wa kwanza?" Binti ambaye anasoma kwa wasiwasi asijue kama atapata ada ili amalizie masomo yake! Jamii yetu imekuwa ikiongozwa na mihemko.

Jamii yetu inaangalia nani kasema, siyo kasema nini? Vipi kana hilo lingeibuliwa na Gavana wa Dar, aseme 'Nimekuwa nikifuatwa na Wanafunzi wa UDSM wakidai kuombwa rushwa y ngono na walimu' Je, tusingemshangilia na kumsifu ni mchapa kazi?

Wengi twaweza kupuuza leo lakini tutambue ipo siku watoto wetu wa kuwazaa (kama hao Dad zetu hatuna uchungu nao) watasoma vyuo vikuu na watafanyiwa hayo hayo tunayoyapuuza. Tusipokemea leo tusitegemee tabia hiyo ya itakufa pindi watoto wetu watakapojiunga. Mabinti kuombwa rushwa ya ngono ipo katika vyuo vyote iwe vya umma ama vya binafsi. Mwaka huu huu kuna Mwalimu wa UDOM alikamatwa na TAKUKURU kwa kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wa kike aliyefeli ili ampe alama za kumfaulisha katika mtihani wa marudio!

Hivyo baada ya sisi kushambulia hoja tuneamua kumshambulia mtoa hoja, waswahili wana msemo 'Mjumbe hauwawi' ila sisi tunataka kuamua wakati ametupa ujumbe. Kwa kizazi hiki kilichojaa uoga sitegemei kuona kikipaza sauti, Mabinti wengi vyuoni wanapitia maswahibu makubwa na hawezi kusema kwasababu ya uoga wa kufelishwa.

Bado nafikiria uamuzi ambao utachukuliwa na UDSM baada ya kumwita na kumhoji Dr. Vicensia Shule juu ya tuhuma alizoibua, nitashangaa sana kuona/kusikia amesimamishwa ama amfukuzwa kazi kutoka na hili, kitu nachotegemea ukisikia na kukiona ni UDSM kumpongeza Mhadhiri huyu kwa ushujaa wake wa kupaza sauti kwa niaba ya Wanafunzi wake. Ikubukwe Dr. Shule ni mlezi wa Wanafunzi wake japo siyo kwamba ni 'Dean of Students' lakini Mwalimu yoyote yule awe wa Dini ama shuleni, ni mlezi 'automatically' kila Mwanafunzi aliyepo katika mazingira yake

Tuungane kukomesha ukatili wa kinjisia vyuoni, mafiosini, shuleni, migodini, hospitalini, vyama vya siasa na hata mitaani kwetu.

Wewe kama mdau wa Elimu Unasemaje?
 
Dr. V.S anastahili pongezi kwani kusimamia kitu kama hiki kwenye mfumo dume bila kujali madhara yanayoweza kumpata ni kazi kweli kweli. Kuna wafia vyuo ambao vyuo vyao vikitajwa kwa vitu hasi basi wanakimbilia kusema mtu anachafua chuo. Wengi tunajua hayo mambo hutokea swali ni ana ushahidi kiasi gani. Lakini pili na cha msingi zaidi hatua gani zinastahili kuchukuliwa. Kama tukikubali dalili zipo kitu kimoja ni kufanya iwe vigumu kwa lecture mmoja kuwa na maamuzi ya mwisho kwenye somo-kuna system ya ku appeal vyuoni kama huridhiki na matokeo yako hivyo ikifanyiwa kazi kumkata mwanafunzi marks kwa uonevu ni kitu kinaweza kupunguzwa. Kwa upande wa post graduate si vibaya kuwa na supervisory team ya at least watu wawili-hadi watatu hii itapunguza mwalimu mmoja kuwa na sauti kubwa. Wanafunzi pia wapewe uelewa wa kutosha wa jinsi ya kujikinga na wahadhiri wa aina hiyo pamoja na system za kuweza kuwanasa.
Shida kubwa itakuwa pale mwanafunzi anapojilengesha kwa mhadhiri kwani yeye mwenyewe yuko tayari kuuza utu wake. Hapa elimu kwa wote wanafunzi na wahadhiri labda inaweza saidia hasa kwa upande wa wahadhiri. Nilisha wahi kuwa introduced kwa wahadhiri waliokuwa wanakwenda disko na wanafunzi wao mabinti wa post graduate chuo fulani hapa nchini-haihitaji kufikiria sana kujua nini kina endelea. Ukisikia darasa linamuita mwalimu shemeji basi ujue hapo darasa zima linahusika. Yote kwa yote sio ethical kwa mwalimu kutembea na mwanafunzi wake bahati mbaya unaweza ukakuta wenye madaraka ndio wanafanya hivyo bila aibu.
 
Mkuu hili taifa limezama kwenye uzinzi na wanaongoza kwa uzinzi ni wasomi sijui huwa na pepo gani mchafu wa ngono

Kwaiyo hao jamaa lazima wayatetee mambo yao mm binafsi nimeshuhudia Mara kadhaa vyuoni Lecturer akishakiwa kwa tuhuma ya ngono unakuta uongozi wa chuo haumfuatilii na kupuuza hizo taarifa

Lakini ikitokea lecturer amefumaniwa sehemu ndio utakuta uongozi wa chuo unamchukulia Action kujisafisha
 
Vitalis Konga, Jinai kama jinai haiwezi kushughulikiwa kwa njia ya vipost vya kwenye mitandao ya kijamii.Kama aliona hayo yanatendeka kwanini asiende kuripoti polisi kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa kesi za jina ya 1967,kifungu cha 7? JE, aliwahi kulifikisha kwenye uongozi wa chuo ? Kwa PHD na miaka 21 UDSM na alichokifanya hakika,Elimu yake haijamsaidia.Labda tuseme na yeye alitoa rushwa ya ngono ndo akafika hapo alipofika,tukasema anawaonea gere wadogo zake wasiwe kama yeye tutakuwa tumekosea?Halafu eti,anamuomba rais achukue hatua,rais achukue hatua zipi hapo? Kwa kiwango cha Phd bado anaamini katika hilo rais anaweza kuchukua hatua gani HAPO? Nashawishika kumuunga mkono faizafoxy asemapo,"HUKO SHULE MLIENDA KUSOMEA UJINGA".HUYU CHUO KIMCHUKULIE HATUA KALI SANA.[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom