Rushwa ya ngono maofisini

Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
180
Jamani maofisini kuna mambo ambayo yanasikitisha sana.
Tuna wataalamu wengi tu ambao utaalamu wao wameupata kimashaka hasa kwa rushwa ya ngono.
Mbaya zaidi wanaendeleza tabia hii hata wanapokuwa maofisini au katika sehemu zao za kazi.
Utashangaa wanapanda vyeo kila kukicha. Kisa tu kamridhisha boss usiku uliopita.
Kasi ya utendaji wao si mzuri hata kidogo zaidi ya kususbiri kuelekezwa kila kitu.
Wamekuwa ni watu wa kubebwabebwa tu katika ofisi husika na wenye dhamana nao.
Kuna wengi tu hawana hata huo ujuzi wanao fanyia kazi hata chembe.
Au wengine wanao lakini kwa kiasi cha chini mno. Hii ni katika ofisi zote za umma na binafsi
Kweli tumeamua hata sisi binadamu kujibinafsisha wenyewe kiasi hiki?
Hivi jamani tunaelekea wapi?
 

mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
18,923
23,793
hii kali! kujibinafsisha wenyewe lol
ni kweli husemayo na wapo wanawake ambao kweli wao dili lao ndio hilo....kutoa uroda ili aweze kupanda ngazi na hamna aibu kabisa.
sasa unajua ni rahisi sana kuonyesha kidole kwa wanaume/mabosi kwa udhaifu wao lakini pia lazima tujue kwamba kuna wanawake ambao wao hii ndio kazi yao na wanakutia majaribuni mpaka basi tuu
 

smati

Senior Member
Dec 24, 2010
149
5
Inaniuma sana hii kitu, hakuna sehemu ambayo nimefanya kazi sijakutana nalo hili. Itabidi iwepo kozi pale udsm ya wavua chupi;
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
45,184
75,662
Natumai Nyote Hamjambo Na Mnaendelea Vyema Na Utafutaji Wa Tonge Japo Tutaishia Tu Kuwa Chini Ya Dola Moja Wakati Wana ESCROW Na Majizi Yanapeta! JAMANI KWANZA KABISA NAPENDA KUPONGEZA WAANZILISHI WA PLATFORM HII YA JF na Wana MEMBERS Wote Humu KWANI KWA UTAFITI Wangu AMBAO NINA UHAKIKA Nao Ni Kwamba JF Ni KIBOKO YA KUREKEBISHA MAMBO YA KIPOPOMA Yanayoendelea Hapa Nchini Kwetu NA IMEKUWA NI CHACHU YA MAPINDUZI Ya KIFIKRA, KIUNGOZI Na KIUTENDAJI Na Kwa ASILIMIA 75 Hadi 90 JF IMEFANIKIWA MNO KUWEKA MAMBO SAWA KWANI MEMBERS HUMU NI WATU WENYE UELEWA WAO MKUBWA TU NA VIONA MBALI...HONGERENI KWA HILO NA POPOTE ULIPO JIPIGIE MAKOFI Ya Ki ESCROW ESCROW.

Jamani Leo Nimekuja Na SUALA MOJA Ambalo Kwa BAHATI MBAYA SANA HATUJA WAHI KULIZUNGUMZIA Na KAMA TUMEWAHI KULIZUNGUMZIA Basi HATUJALISHUPALIA SANA KAMA ESCROW NA TEZI DUME! Ndugu Zanguni KILIO CHANGU KIKUBWA NI SUALA LA RUSHWA YA NGONO MAKAZINI, MASHULENI Na ktk TAASISI ZINGINEZO. DADA ZETU, MADEMU Zetu NA PENGINE WALIOTUZAA WANANYANYASIKA SANA NA SUALA HILI LA RUSHWA YA NGONO.

Kupitia Kwenu HEBU NAWAOMBENI JAMANI TUJADILIANE Na TULIPIGIE VITA HILI SUALA ILI MAMA, DADA NA MADEMU ZETU WAWE SALAMA KWANI HALI NI MBAYA Na INASIKITISHA. TAFADHALI TUSHAURIANE NINI KIFANYIKE Na KAMA WANAUME WENZANGU AMBAO MPO HUMU NDANI ( JF ) NA MNA TABIA HIYO YA KUOMBA RUSHWA YA NGONO JAMANI TUACHE HIYO TABIA NA TUMWOGOPE MWENYEZI MUNGU.

Leo NATAKA NIPIGANIE SANA HAKI ZA AKINA MAMA, DADA NA MADEMU ZETU HIVYO MADUME WENZANGU MTANISAMEHE Kidoooooooooogo. Karibuni Tuliendeleze!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom