Rushwa wizara ya maji na umwagiliaji

mabambase

New Member
Feb 24, 2016
2
0
Kwa masikitiko makubwa naandika ujumbe huu nikiwa kama kijana niliyejiajiri lakini ndoto zangu za kujiajiri zinaonekana kuzimwa na serikali yetu eidha ni kwa makusudi au kimfumo lakini sioni mwanga tena zaidi ya giza.

Mimi ni kijana, baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka 2008 kwenye fani ya uhandisi niliamua kujiajiri kwa kufungua kampuni yangu ya ujenzi ili niweze kufungua mwanya wa kuajiri na vijana wengine pia.

Nilianza kuendesha kampuni kwa shida na hii ni kutokana na kutokuwa na mtaji wa kutosha na miaka 4 baadae mambo yalikaa sawa nikaanza kwenda vizuri kwa kupata miradi mingi sehemu tofauti tofauti hasa MIRADI YA MAJI VIJIJINI chini ya ufadhili wa Bank ya Dunia na serikali ya Tanzania.

Mwaka 2014 kampuni yangu ilipata takribani miradi mine ya maji vijijini yenye thamani ya Zaidi ya Tsh 2.8 bilioni.

Tulianza kazi vizuri huku tukilipwa kwa wakati, tatizo lilianza mwishoni mwa mwaka 2014 baada ya Sakata la Escrow kuibuliwa bungeni na hivyo wafadhili wa miradi hii walisitisha ufadhili wao kwenye miradi hii ya maji vijijini ambayo kwa kiasi kikubwa ilkuwa kwa ufadhili wa bank ya dunia na serikali yetu kwa kiasi kidogo.

Mateso yalianzia hapo tangu Januari 2015 hadi leo serikali haikuweza tena kutulipa madeni yetu na hivyo kupelekea miradi yetu yote kusimama huku tukiwa na madeni kwenye taasisi mbalimbali za fedha.

Kampuni yangu imeajiri wahandisi wenye shahada watano, mafundi wenye ujuzi mbalimbali kumi na mbili, madereva sita, watu wasio na ujuzi ambao walikuwa wanafanya kazi za kutumia nguvu kama kuchimba mitaro, kubeba zege, tofali au mchanga kama 200 kwa site zote.

Hali yetu kimaisha imekuwa ngumu sana tangu kipindi hicho hadi hivi leo ninavyoandika ujumbe huu.

Mimi kama mkurugenzi wa kampuni nimeishi kwa stress kubwa, kuna wakati huko Shinyanga nimefikishwa kwa mkuu wa wilaya na mahakama ya mwanzo kwa wale wanaonidai lakini tulijitahidi kwa kadiri tulivyoweza kupunguza madeni.

Kilichonifanya kuandika uzi huu ni RUSHWA ya waziwazi inayoendelea wizara ya maji kwa sisi wakandarasi tuliofanya miradi ya maji ambao hatujalipwa pesa zetu na miradi yetu imesimama hadi leo.

Wakati wa kufunga bunge, waziri wa maji alijigamba wanakwenda kulipa makandarasi wa miradi ya maji ili kazi zilizosimama zimalizike nchi nzima. Cha kusikitisha hakuna kilichofanyika na si waziri, naibu wala katibu wa wizara aliyewahi kulitolea ufafanuzi suala hili ili tujue tutalipwa lini.

Mchezo uliopo kwa sasa ni kwamba wizara ya maji ina fedha ambazo zinatakiwa kutumwa halmashauri kulipa wakandarasi wanaodai, na ili pesa itumwe kwenye halmashauri unayodai wewe mkandarasi ukipata mtu kati wa kukuunganisha na wakubwa pale wizarani wakubwa watakuuliza UNATUACHA ACHAJE?

Ukiweza kuwahahakikishia kwamba kwenye hayo malipo kuna chao pesa inatumwa kwenye halmashauri unayodai ikiwa na barua ya maelekezo ulipwe wewe muhusika uliyeelewana nao, tofauti na ilivyokuwa awali pesa inayotumwa ilikuwa ikigawanywa kwa wote mnaodai.

Hii imetuvunja moyo sana sisi vijana wadogo tuliojiajiri na kuzalisha ajira kwa vijana wenzetu na hatuna namna ya kufanya maana hatuna ndugu zetu IKULU wala WIZARA YA MAJI.

Ila tunachosema ni kwamba Biblia inasema haki huinua Taifa, kama kwenye taifa hakuna haki hata ustawi wake ni mdogo sisi tusio na ndugu ikulu au wizarani wa kutuandikia memo ili tulipwe tutaendelea KUPIGA MAGOTI NA KUMLILIA MUNGU maana yeye hapokei rushwa,yeye ni wa haki na yeye atatutetea ili haki itendeke na tunaamini machozi yetu hayatakwenda bure.

Raisi Magufuli amefanya ubaguzi kwa kulipa makandarasi wa barabara madeni yote na kusahau kwamba hata sisi ni makandarasi pia.

Nadhani bado anahisi yuko wizara ya ujenzi kumbe si hivyo kwa sasa yeye ni baba wa wote.

Sambaza ujumbe huu kwenye mitandao ya kijamii labda utawafikia wahusika maaana sisi wanyonge hatuna namna ya kufikisha ujumbe kwa wakubwa hawa Zaidi ya mitandao yetu hii ya kinyonge.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!
 
Mikataba mingi ya kibongo ni sawa na kucheza kamali. Kwasababu kila kiongozi anayekuja anakuja na utalatibu wake Ila lakini haitakiwi ukate tamaa hata maisha yetu yakibongo ndivyo ya yalivyo yana changamoto nyingi sana na hii ni kwasababu tanzanania ni moja ya nchi zinazo endelea
Kwasababu hiyo ni kazi kama zilivyo kazi zingine inabidi ufike sehemu husika na uwaeleze matatizo yako bila kuogopa chochote ili ujue mwisho wake ni nini na kama itashindikana utafanya mishe nyingine huo hautakuwa mwisho wa maisha. Na ukisema ulazimisheshe lazima utakutana na tatizo mbeleni siku zote ukiona unafanya kitu kinakataa achana nacho huwezi jua utakuna na nini mbeleni.
 
Lipo tatizo kubwa sana ktk mfumo wa manunuzi na ulipaji wa stahili za wazabuni hasa kwa sekta ya umma.Kupata tenda/order/kazi ni shida {rushwa nje nje},kulipwa pia ni shida..Twapataje mutual benefits value for money ?
 
Back
Top Bottom