Rushwa nchini imeota mizizi-Dr Kafumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rushwa nchini imeota mizizi-Dr Kafumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by masopakyindi, Oct 10, 2012.

 1. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Dr. Dalaly Kafumu  Kana kwamba kukomelea msumari kwenye suala la kukithiri kwa rushwa mchini, Dr Kafumu, mbunge wa CCM aliyenguliwa kiti cha Igunga, ameandika kitabu juu ya kukithiri kwa rushwa nchini Tanzania.

  Kulingana na gazeti la Nipashe la leo 10/10/2012, Dr Peter Dalali Kafumu katika kitabu chake "Sauti Inayolia" ameelezea jinsi rushwa ilivyo kithiri nchini , pengine kuliko wakati mwingine wowote ule.

  Dibaji ya kitabu cha Dr Kafumu imeandikwa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.

  Dr Kafumu ameelezea kuwa ,
  "baadhi ya wanasiasawanapata nyadhifa mbali mbali kwenye vyama na hata ubunge kwa kutoa rushwa",

  Ameendelea,
  "Maamuzi ya wapiga kura na mamlaka za uteuzi yanashawishiwa na rushwa,mameneja katika taasisi na idara za serikali wanakula rushwa ili wawe matajiri".

  My Take

  Kwa hakika sasa suala la rushwa ni la kisiasa na limepita uwezo wa utendaji wa TAKUKURU.
  Tatizo limeota mizizi na halijakemewa na kuchukuliwa hatua kiasi cha kutosha kisiasa.

  Inaelekea wanaolipihia kelele majukwaani nao vile vile wanafaidika na rushwa katika kificho, hata hivyo matokeo yake yako peupe na wananchi wanaona.
   
 2. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ameyajua leo baada ya kung'olewa ubunge
   
 3. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,746
  Likes Received: 12,827
  Trophy Points: 280
  Kwani kafumu ana shangaa nini?
  Mimi namshangaa yeye kushangaa swala rushwa wakati kwenye campaign zake alitoa rushwa ya "wali maharage!"

  sijui kafumukia wapi?
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Aliyeandika dibaji ni nani? Na aliyelea rushwa iliyoota mizizi nchini ni nani vile?
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Hata maindi na mchele waliogawa ccm kwenye uchaguzi mdogo igunga ni rushwa na imedhibitishwa na mahakama kuu kupitia hukumu ya kesi yake ya kupingwa ubunge.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 6. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Mkapa ,Sumaye na Dr Kafumu wanapinga rushwa!
   
 7. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  rostam amemzindua usingizini ee?
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Hii vita ni kali sana na kubwa mno...sijui JK ana jipya gani au ndio jiii kama kawaida nao ni upepo utapita??
   
 9. Munambefu

  Munambefu JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 895
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Ati Dibaji Mkapa,mwandishi Kafumu?kutupiga watupige wao halafu kulia walie wao!yani wanafisidi mpaka haki yetu ya kulia
   
 10. T

  Tewe JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Anacheza huyo huwezitenganisha ccm na rushwa
   
 11. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  iundwe tume kuchunguza kama ni kweli tanzania kuna rushwa, hili jambo ni geni sana.
  Ila takukuru ndio mizizi yenyewe ya rushwa chini ya awamu ya ukapa.
   
 12. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  kwenye kitabu chake kaorozesha na ule mpunga wa kampeini au ile ilikuwa TAKRIMA na si mdudu RUSHWA?na kwanini aseme RUSHWA IMEOTA MIZIZI NCHINI,kwanini asiseme RUSHWA IMEOTA MIZIZI NDANI YA CCM? na wetaja nikitengo gani kinaongoza kwa kuathirika na mdudu rushwa?
   
 13. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ameandika ni kiasi cha rushwa alichotoa wakati anawania ubunge.

  Huwezi kuwa gamba bila kutoa au kupokea rushwa, karibu wanaiweka kwenye katiba ya chama lao gambas.
   
 14. Kiwalani

  Kiwalani Senior Member

  #14
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hicho kitabu alikiandika na kilitoka KABLA ya Kafumu kugombea ubunge Igunga.
   
 15. mirisho pm

  mirisho pm JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 2,483
  Likes Received: 3,303
  Trophy Points: 280
  tusimhukumu MH.KAFUMU na MH.MKAPA au MH.SUMAYE, tukubaliane kwanza kwamba ni kweli, pia tuwaache waseme yote mpaka wamalize.. cn b a gud source of in4mation by any how, freedom of expression is gud! alafu tuwaulize, wakati walikuwa kwenye nafasi nzuri kulisemea jambo hilo pengine kuliko mtu mwingine yeyote kwa kipindi chao Walifanya nini? au ukitoka ndo unaona rushwa, ufisadi... au ni muendelezo wa zile siasa za wachumia tumbo? muhimu sana ni kwa nini sasa? em fikiria kama hao jamaa wanalia kuwa rushwa imewaumiza.. na wana karibu kila ki2 anachohitaji binadamu wa dunia yeyote chini ya jua.. itakuwa kina cie huku matombo? kuanzia mwenyekit wa kjj mpaka kwa mkuu wa wilaya unatoaje jasho? lakini pia iwe funzo kwa wanasiasa walio kwenye nyadhifa, watekeleze wajibu wao, wakitoka wasituletee ngonjera tuuu.. watanzania makabwela tumechoka hizo stori at!
   
 16. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu, umejitofautisha na small time thinkers kwa kupasua mada na kuingia ndani ya kiini cha tatizo.

  Ni jambo la kushangaza kuwa WALIOMO MADARAKANI hawaoni kwamba rushwa ipo.
  Ila wakitoka ndio inpowaumiza na wao wenyewe.

  Lakini tumpe haki yake Dr Kafumu kwa sababu aliandika kitabu hiki KABLA ya kuenguliwa ubunge.

  Kwamba sasa kilio cha rushwa kinaanzia NDANI ya CCM basi mambo inaelekea inaanza kuwa mbaya sana.
  Hata hivyo wananchi wa kawaida wameliona hilo muda mrefu sana wasijue la kufanya.
   
 17. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Still kwa nini aliingia kwenye chama ambacho kimeleta mfumo uliojaa rushwa
   
Loading...