Rushwa na UVCCM mkoa wa Tanga

stuartkifua

Member
Apr 19, 2014
62
5
Ni dhahiri ule msemo wa asali hailambwi mara mbili hauwezi kupingwa kokote na hii ni baada ya kamati ya utekelezaji UVCCM mkoa wa Tanga kuingiwa na tamaa ya visenti kutoka kwa baadhi ya wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti Mkoa na hivyo kupelekea makosa matatu ya msingi
1.Kuteua wagombea wote watatu wakitokea Tanga mjini na Mkinga

2.Kupokea rushwa kabla na baada ya kikao cha kamati ya utekelezaji kilichokaa 02/10/2017 ushahidi upo

3.Kuingiza watu ambao si wajumbe wa Kamati ya utekelezaji kwenye kikao na hii dhahiri ni kwa sababu ya kuweza kufanikisha adhma yao


Kwanini Rushwa?Kumekuwa na mtandao mkubwa wa kuomba rushwa ukiongozwa na mmoja wa kiongozi mkubwa wa jumuiya akishirikiana sambamba na makatibu wa wilaya na ambapo baadhi ya makatibu walitumwa kwenda kuwaomba rushwa baadhi ya wagombea wakijinasibu watoe pesa ili jina lirudi na hapa ndo tulipoanza kuona sasa nguvu ya rushwa ukilinganisha na na demokrasia na vigezo vya uongozi kuwekwa pembeni na hatimaye rushwa au mlungula kushika nafasi

Na kudhihirisha kuwa rushwa imefanya kazi basi wajumbe wa kamati ya utekelezaji wamependekeza majina matatu ambayo mawili kati ya hayo ni ambayo yalishapigiwa kelele kwa kuendekeza vitendo vya rushwa kwa kuwapa wajumbe wa kamati ya utekelezaji ili majina yao yarudi na kwa vile ushahidi upo basi sina budi kuyaweka hapa majina ya hao wagombea na kama ni ubishi basi wakanushe juu ya hili

1.SAAMUMY ALLY
2.YUNUS KASOMO
3.OMARY SAID

Kupendekeza majina kwa kuhusudu rushwa ni sawa na kuiuza jumuiya kwa watu tena bila aibu

HIVYO SISI KAMA WAPENZI WA CHAMA NA JUMUIYA TUNAIOMBA KAMATI YA UTEKELEZAJI TAIFA IWEZE KUPITIA UPYA MJAINA YA NAFASI YA MWENYEKITI UVCCM MKOA WA TANGA NA HATIMAYE KUTENDA HAKI KWA KUWAPATA WAGOMBEA WENYE UWEZO NA VIGEZO KWA KUFUATA MISINGI YA HAKI NA SI RUSHWA

SHIME MWENYEKITI,MAKAMU MWENYEKITI NA KATIBU MKUU TULIFANYIE KAZI HILI LA SIVYO JUMUIYA INAENDA KUUZWA NA KUFA KWA MKOA WETU WA TANGA
 
Back
Top Bottom