Rushwa na uraia wa Siyoi, CCM watafutana uchawi badala ya kujibu HOJA

chachana

Member
Aug 4, 2011
57
92
Rufaa iliyokatwa na chadema kuhusu utata wa uraia wa sioi sumari mgombea wa ccm umeleta mkanganyiko mkubwa kwa viongozi wa ccm.

Inasemekana kwenye vikao nape alionya sana kuwa utata wa uraia wa sioi unaweza kuwaingiza matatani. Idara ua uhamiaji ilishakiri kwa barua kuwa sioi hakuwahi popote kukana uraia wa kenya na mbaya zaidi inasemekana pia kuwa hati mbili za kusafiria zenye kuonyesha uraia wa nchi mbili tofauti.

Mpaka usiku huu mkurugenzi na wanasheria wa serikali walikuwa kwenye kikao kuhusiana na suala hilo. Hata hivyo inasemekana kuna uwezekano mkubwa sioi akatolewa kwenye kugombea kwa sababu kinyume na hapo ni kuamsha balaa kubwa.
IGP saidi mwema inasemekana usiku huu amefika usa river kwa ajili ya suala hili

Update: by Joseph Peter
 

Siyo rufaa, bali ni PINGAMIZI. Iwapo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo [Bwana Kagenzi] atalitupa, ndipo Nasari anaweza kukata Rufaa kwa Tume ya Uchaguzi Makao Makuu Dar es Salaam na hiyo ndio itaitwa ni Rufaa.

Swala la Uraia halimhusu IGP Said Mwema, kama kweli ameenda hapo ni kwamba anaingilia kazi za Idara ambazo sio za kwake. Maswala ya Uraia yanahusu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Uhamiaji ambaye yuko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kama CHADEMA wana barua ya kutoka ofisi ya Uhamiaji mkoani Arusha, basi hapo kuna utata mkubwa. Kwa kuwa kuna baadhi ya wana CCM hawakutaka Siyoi apite, watahujumiana wao kwa wao na huo ndo utakuwa mwisho wa mchezo.
 

Nilidhani CCM wanapiga kelele juu ya ukoo ndani ya Chadema tu kumbe hata wao wana endeleza ? Kuna nini hadi huyu mtoto apiganiwe hivi kuwa Mbunge ?
 
Hii ni shida nyingine ya kugangamalia jambo bila kufikiria madhara yake. Si kila saa Nape ni Mropokaji wakati mwingine huwa mkweli asilimia mia moja. Oneni sasa.
 
Kazi imeanza na hata watakayemweka kama wataamua kumtoa asiyeoa naye watamtafutia sababu tu. Chadema Chama Makini chanjeni mbuga mwenzetu ana msiba kwake
 
Mwanzoni nilidhani ni mizengwe ya ccm jama alivokatwa Bashe kumbe pana weza kuwa madai ya mashiko.
 
Mliambiwa Barua ya UHAMIAJI ilika bidhiwa CHADEMA na vigogo wa CCM mkabisha sasa yako wapi,kazi yenu kupinga bila kutafakari,hata wama CCM hawamtaki siyoi
 
Mwanzoni nilidhani ni mizengwe ya ccm jama alivokatwa Bashe kumbe pana weza kuwa madai ya mashiko.

Kwa mujibu wa Bashe mwenyewe, anasema alizaliwa Tanzania na kwa kujua mizengwe ya sihasa za Tanzania akaukana na uraia wa Somalia kabla ya uchaguzi. Uhamiaji walithibitisha haya lakini Magamba wasipokutaka, hata nyeusi itaitwa nyeupe.
 
Sheria gani inayomfanya Sioi asiwe raia wa Tanzania?.... sheria namba na kifungu plz.
 

Imekwenda shule! Imetulia!
 

kwa hiyo hata baba yake hakuw raia wa tanzania?
 
CCM mercenary politician:
rage
kinana
rostam
and bunch of them are there...

Mkuu inasikitisha sana kuona kuwa watu wengi sana wana uraia wenye utata, lakini serikali iko kimya tu. Utata wa urais wao unaonekana pale wanapokuja kugombea nafasi za uongozi. Kama ni kweli mgombea ana pasi mbili za kusafiria, anakuwa amevunja sheria za nchi, na anatakiwa kuchukuliwa hatua, na kama ana uraia wa nchi mbili moja ikiwa ni Tanzania pia anatakiwa kuchukuliwa hatua, na kama ni mgeni inatakiwa ithibitishwe kuwa amelipia hati zake zote za ukazi na kuwa taratibu zote zinazohusiana na uhamiaji zimefuatwa.

Inaonesha kuwa kuna udhaifu mkubwa sana Uhamiaji. Ni Jambo la aibu kama kweli IGP amekwenda USA RIVER kwa sababu ya utata wam uraia wa mtu mmoja anayeeonekana kuwa mgombea wa CCM, wakati Dar es salaam makao makuu kuna mamia ya mambo muhimu yanayitakiwa kushughulikiwa. Still inaonekana hata ndani ya jeshi letu la Polisi usalama wa raia uko chini ya maslahi ya CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…