Rushwa na biashara vinarudi Tanzania

Rushwa na biashara vinarudi Tanzania

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,284
Reaction score
13,943
Nimetoka Tanzania juzi na mara ya mwisho kwenda Tanzania ilikuwa 2019.

Kwa maono yangu.

1. Biashara zinaanza kurudi kwa kasi na watalii wameongezeka sana.

2. Rushwa inarudi kwa kasi sana hasa NIDA na Police traffic.

Mfano NIDA kuna watu wanasubiri miaka miwili card bila kuwaambiwa sababu wakati kuna watu wakito pesa wanapata card zao mapema sana. Sasa tatizo la ucheleweshaji wa card ni nini hasa.

Kwenye traffic hasa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha rushwa imezidi mfano barabara ya bypass ya Arusha imefika kiwango hata watu hawataki kutumia hiyo njia kwasababu ya usumbufu wa polisi.

Raisi shughulikia rushwa na muwe wakali maana tunarudi wakati wa Kikwete.
 
Mwandiko tu unaonekana bonge la bosi,a lafu umerelax huna haraka.

Mama head of state yupo humu ajustfy your opinion
 
Watalii au biashara na rushwa havikuathiriwa kubadilika uongozi. Hata kabla ya huu, rushwa uhamiaji, NIDA, tra ilikuwa pale pale.
 
Kipindi Cha mpito hiki.
Baada ya 2025 ndio tutakua na uelekeo. Kwa Sasa watu wanaziba magape kulingana na urefu Wa Kamba ZAO.
Dunia ya sasa Nje ya Demokrasia na utawala Bora basi ni Lazima pawe na Kiongozi mkali.
CCM imetengeneza mianya ya Rushwa Chini ya Katiba Hii. Ukisikia Katibu au wizara Fulani wameiba hakuna MTU Wa kuwafanya chchote Bila idhini au kuwajibishwa na aliyemteua

CCM ni chama cha Mapinduzi. CCM walitumia ujanja Mwingi sana kuweka mifumo na Katiba inayoendana na Tawala za kijeshi. Ndio MAANA chama cha kina Makada wengi Ndani ya majeshi hasa wale Wa zamani ambao wengi Wanapewa vyeo na madaraka Ili kuwatumia kwenye Siasa na utawala lakini pia kufikisha maelekezo ya chama kuwa ni Amri ya kijeshi Ndani ya majeshi . Hivyo ni nchi inayotawaliwa kijeshi chini ya ya mapinduzi ya CCM.

Ubaya Wa mfumo Huu Wa CCM kutawala kijeshi ni kuwa kuna kuwa na raia wanaotumia Majeshi kulinda uhalifu wao kwenye Mali za umma. Leo hii Kuna watu walitakiwa SIO tu kufungwa Bali kunyongwa Lakini Bado wanapewa madaraka na wao wanageuka kuwa mabosi Wa Polisi. Unakuta RC ,DC au Waziri Ana tuhuma nyingi za ubadhirifu Wa Mali za umma lakini MTU huyo huyo anaweza kumpa RPC maelekezo Hata kama SIO halali na Kwa Sababu ni kundi la raia wachache waliojimilikisha nchi kijeshi Kwa kuwatumia makada wachache Ndani ya majeshi basi wanaendelea kutawala kijeshi na kurithisha Watoto wao nafasi KUBWA KUBWA na kuendelea kujificha Ndani ya Chama kilichojificha nyuma ya vyombo vya Dola.

Katiba Mpya ni Lazima na muhimu sana Ili kuirudisha nchi Kwa wananchi. Ama itawaliwe kijeshi kabisa na Amri ifuatwe na wote.

Hii nchi Haina dirá maalumu.
 
Biashara ni kweli inarudi kwa kasi mkoa wa Arusha, utalii upo juu na dec hii nitakuwepo huko. Serena, KIBO inasemekana imesheheni. Arusha walipitia kipindi kigumu sana awamu ya 5, ukijumlisha na covid ule mkoa ulikuwa kwenye hali mbaya sana.

Barabara ya EAC haina trafic wengi ukilinganisha na barabara za katikati ya mji, Naitumia sana nikiwa Arusha na waliopo si wapenzi wa magari madogo labda kama ww ni dreva wa gari kubwa inawezekana.

Kiualisia Haya magari ya watanzania hasa mikoani kama Arusha Trafic wakiamua kusimamia maadili yao watakusanya pesa nyingi sana, wakati mwingine kuchukua hizo tsh 2000-5000 wanawabeba tu raia.

Zama za JK zimerudi ndio na nadhani itachukua muda kurudi kwenye mfumo unaofanana na ule wa awamu ya 5.
 
Ama itawaliwe kijeshi kabisa na Amri ifuatwe na wote.
Yaani nchi itawaliwe na jeshi tufate amri tu? Watabaki wanyonge na jeshi wakiuza madini na kilimo cha mkono, wafanyabiashara wote wenye mitaji wataiondoa mitaji yao kuilinda, Kenya utalii utapanda sana sababu mshindani wake akili kakosa, kariakoo vyumba vitawa chini ya 50,000 kwa mwezi, Bandari ya mombasa itaneemeka, misaada itakuwa chini sana. Katiba mpya ni muhimu na itapatikana ila haitakua mwarubaini wa matatizo yote, bado tutakuwa na mambo ya kutatua. Huko Ulaya panapoitwa nchi zilizoendelea wana matatizo wanatatua.
 
Yaani nchi itawaliwe na jeshi tufate amri tu? Watabaki wanyonge na jeshi wakiuza madini na kilimo cha mkono, wafanyabiashara wote wenye mitaji wataiondoa mitaji yao kuilinda, Kenya utalii utapanda sana sababu mshindani wake akili kakosa, kariakoo vyumba vitawa chini ya 50,000 kwa mwezi, Bandari ya mombasa itaneemeka, misaada itakuwa chini sana. Katiba mpya ni muhimu na itapatikana ila haitakua mwarubaini wa matatizo yote, bado tutakuwa na mambo ya kutatua. Huko Ulaya panapoitwa nchi zilizoendelea wana matatizo wanatatua.
Hizi ni dhana tu. Tanzania ibatawaliwa kijeshi Kwa mgongo Wa raia.
Raia kutawala kijeshi ni tatizo sana mana matapeli Wa Nje wanashirikiana na watu wasio na uzalendo kupora Mali zote na mikopo wanachukua kutapeli nchi inabaki na madeni.
Wawekezaji ni matapeli ,Wezi na wanyanganyi.

Unategemea vipi wawekezaji Wa kulika para hicho, mihogo, manabasi, vanilla, ni upumbavu mkubwa.

Tuna wasomi wanauwezo wakutumiawa.
Tutfanya biashara na wao. Nani ataacha Kununua dhahabu Kwa sababu ya Haki za Binadamu, mbona Congo Wanakwenda Kununua ,nani ataacha Kununua almasi . Madaraja tutajenga wenyewe, mabarabara wenyewe.
Tutaimarisha usalama na kufuta dhulma.
Tutawakaribisha watalii na kuwapa ulinzi mkubwa .
Leo Rwanda wanahost wakimbizi Toka Ulaya Kwa sababu ya utawala makini wa Kijeshi .
Wazungu ni wanafiki.
Wakati wa JPM walikubali kuwa nchi yetu uchumi unapaa. Na walimhofia kuwa Ataleta mabadiliko ya kisiasa Afrika nzima Ndio maana wakamfanyia figisu kushirikiana na wanasiasa raia ndani na nje ya Chama chake.

Raia wakiwa juu bila katiba inayowabana ujue wanawaza kuwa mabilionea na kuyatumia Majeshi kama mbwa wao wa kulinda hujuma zao . Wanachofanya ni kuwatuma hao hao wanajeshi na Polisi kutawala Kwa amri. Hata hivyo amri zao zijakaa unafiki na kukosa tija kwenye maendeleo. Iddi amini angeachwa atawale nchi yake Kijeshi Leo Uganda ingekua ni nchi Tajiri sana Duniani. Hofu ya Nyerere kuwa Hali ya Uganda ingeleta pia mapinduzi Kwa nchi jirani ikasababisha awasaidie waasi wa Uganda na kuingia kwenye vita.
Zanzibar inatawaliwa Kijeshi, Tanganyika inatawaliwa Kijeshi. Ndio maana hakuna kura itakayompata Rais Tanzania ndani ya CCM na nje ya CCM.
Kwa hiyo hakuna katiba mpya ni ama kila uchaguzi Jeshi liisaidie CCM kupindua Nchi na kuwarudishia nchi au wapinzani wabaki wasindikizaji wa matapeli waliojipenyeza na wawekezaji wezi.
 
Back
Top Bottom