kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,310
- 12,606
Kinachohalalisha kosa kufanyika ni kosa lenyewe na dhamira wakati wa kulitenda kosa. Kuna wakati rushwa inaombwa kwa nia njema ili mtumishi apate nguvu na moyo wa kutoa huduma.
Rushwa inapofusha macho na masikio ya wanaoidai, na wakati mwingine rushwa inafunga midomo ya wanaoipokea. Lakini kuna wakati rushwa inasababisha matokeo chanya kwenye utoaji huduma hasa pale inapoombwa ili mtu apate chunywa chai, apate nauli na kujia kazini , kulipa ada ya mtoto na kulipa pango la chumba.
Wakati mwingine mtumishi atalazimika kuomba na kupokea rushwa sio kwa kupenda wala hiari yake ila kama njia halali ya kupata chakula, ada ya mtoto, kodi ya pango, nauli ya kutokoa na kurudi kazini, kuhudumia gari, kurejesha deni la benk lenye riba kubwa, adhabu za road traffic, kufua uniform, nk.
Waziri husika sio mjinga hata kidogo, anahafamu viwango vya mishahara vya watumishi wake wote. Waziri hajui watumishi wake wanaishi wapi, umbali gani kutoka kazini na kwenye nyumba za kodi kiasi gani maana hakuna nyumba za watumishi, lakini anataka watumishi wanaowahi kazini, nadhifu na wanaochangamkia wateja wao.
Waziri hataki kufahamu mtumishi amekula nini (maana hata canteen hakuna), anakujaje na kuondokaje kazini maana hana usafiri kwa watumishi, hataki kujua kama mtumishi ana watoto wangapi na wanasoma wapi anachohubiri ni huduma safi iliyotukuka, ubaya wa kula rushwa na wizi wa vitendea kazi.
Mhudumu kwa hali hiyo lazima atafanya mambo yafuatayo wakati akisubiri siku ya kustaafu ya kustaafu kwake.
1. Atatoa huduma mbovu kwa wateja wake kutokana na njaa au msongo wa mawazo
2. Atadai au kupokea rushwa hata kama hataki
3. Ataiba vitendea kazi vya mwajiri wake
4. Ataiba muda wa mwajiri akifanyakazi binafsi za kujalizia upungufu.
5. Atajaa madeni mwili mzima kutoka kwa watu binafsi, taasisi za kukopesha, gengeni, shuleni, vyuoni, kwenye bucha, nk
6. Atajiuza mwili wake au kuingia kwenye biashara haramu
7. Ataacha kazi
Je, mtumishi afanye nini kama kipato cha ajira hakimtoshi kugharamia mahitaji yake ya msingi kabisa?
Ukiona mtumishi anapata mshahara mdogo lakini bado anafanyakazi hapohapo kazima mtumishi huyo ama anakula rushwa, mwizi wa mali za mwajili, mwizi wa muda wa mwajiri au anafanya vitu haramu.