Hapo kweli pana rushwa ya ajabu. Kuba jamaa yangu nae alihangaika sana tu.
Halafu kuna hili ambalo nimegundua, kwa mfano wasomali, basi hapo ndipo rushwa inapotoka hasa. Kuna msomali aliyezaliwa hapo TZ, Mzazi kazaliwa hapo TZ lakini ile akifika tu na maobi yake jibu la kwanza AAA WE NI MSOMALI HII NI NGUMU SANA TENA SANA. Inamaana tayarisha rushwa ya kutosha. Sasa cha ajabu pammoja na huo ugumu jama akisha pokea rushwa yake passi inatoka hata kama mtu hajui kiswahili.
Yaani hapo palitakiwa paangaliwe haswa. Aliye timiza kila kitu apewe haki yaki.
Passi ni haki ya raia si mpaka aulizwe unaitakia ya nini.
Mbona huku ulaya huulizwi hilo suali, tena hujazi miform nyingi, ukionyesha kitambulisho tu hapo polisi basi wao wana information zako zote, kinacho fanyika wanakuonyesha hapo kwenye screan na kama ziko sawa sawa unatia saini. within a week unapata passi yako