Rushwa kitengo cha Pasipoti haitibiki

Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Kitengo cha Pasipoti kinakwenda kinyume kabisa na agizo la JPM la kupiga rushwa vita. Kitendo cha kuchelewesha pasipoti na kuomba rushwa hakikubaliki. Mtu ameomba pasipoti kuanzia mwezi wa nne mpaka leo akienda anaambia kuna matatizo ya pasipoti akienda kwenye kaunta anakuta wengi wa mwezi watano wamepatia pasipoti. Kuliuliza wametoa kitu kidogo ili wapatiwe. Mambo ya ndani rushwa ni kansa. Badilikeni.
 
Mkoa gani huo ? Honestly mie sikuwahi kujua mtu hapo... All I did is to follow the process... Na nikapata passport yangu ontime kuliko nilivyotegemea. Hiyo ni hapo makao makuu Dsm
 
Watanzania hutaka short cut hivyo hutanguliza mlungula. Wacha waipate
 
Kama ulienda umevaa kama yule Masai Nyotambofu itakuwa wamekuchukulia poa....mbona Watu wanapata Passport tu bila hata mizengwe.
 
Hapo kweli pana rushwa ya ajabu. Kuba jamaa yangu nae alihangaika sana tu.
Halafu kuna hili ambalo nimegundua, kwa mfano wasomali, basi hapo ndipo rushwa inapotoka hasa. Kuna msomali aliyezaliwa hapo TZ, Mzazi kazaliwa hapo TZ lakini ile akifika tu na maobi yake jibu la kwanza AAA WE NI MSOMALI HII NI NGUMU SANA TENA SANA. Inamaana tayarisha rushwa ya kutosha. Sasa cha ajabu pammoja na huo ugumu jama akisha pokea rushwa yake passi inatoka hata kama mtu hajui kiswahili.
Yaani hapo palitakiwa paangaliwe haswa. Aliye timiza kila kitu apewe haki yaki.
Passi ni haki ya raia si mpaka aulizwe unaitakia ya nini.
Mbona huku ulaya huulizwi hilo suali, tena hujazi miform nyingi, ukionyesha kitambulisho tu hapo polisi basi wao wana information zako zote, kinacho fanyika wanakuonyesha hapo kwenye screan na kama ziko sawa sawa unatia saini. within a week unapata passi yako
 
Imenikumbusha mama moja anaitwa Tyetyetye Feb. 2015 na wenzake, wakati na-renew passport, walizungusha na kunipatia saa 12 jioni.
Matendo yalionesha kudai rushwa. Walipoona hatutoi wazitoa past kwa hasira.
 
Kitengo cha Pasipoti kinakwenda kinyume kabisa na agizo la JPM la kupiga rushwa vita. Kitendo cha kuchelewesha pasipoti na kuomba rushwa hakikubaliki. Mtu ameomba pasipoti kuanzia mwezi wa nne mpaka leo akienda anaambia kuna matatizo ya pasipoti akienda kwenye kaunta anakuta wengi wa mwezi watano wamepatia pasipoti. Kuliuliza wametoa kitu kidogo ili wapatiwe. Mambo ya ndani rushwa ni kansa. Badilikeni.
Halafu kwanini wanahoji unaitaka pasisport ya nini? Kwani siyo haki kupewa? Yaaani hadi nipate mwaliko ulaya? Hili ni jipu tena limeoza, mguu ukatwe.
 
Uhamiaji wameshatoa maelekezo kuhusu msongamano kwa kipindi hiki! Miaka 10 iliyopita walibadilisha passport na zinakaa kwa miaka 10 sasa msongamano ni sawa na wakati ule walipobadilisha! Wameshauri waend kuomba wanasafiri karibuni sio kila mwenye passport akiona imeisha anaenda tu! Kuepus msongamano!!
 
Back
Top Bottom