Baadhi ya Viongozi wa Kamati za siasa za Mikoa zenye dhamana ya kusimamia maamuzi hasa wakati wa uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama ama zile za Kiserikali kama Ubunge na Udiwani wamekumbatia rushwa kiasi kwamba wamekuwa Vipofu wa kuziona kanuni nzuri zilizopaswa kutumika katika kufanya maamuzi. Jambo hili limesababisha baadhi ya watu bila kujali kama ni wana CCM ama si wana CCM almuradi wana taka mambo yao kimaslahi yafanyike wamekuwa na nguvu ya kutawala maamuzi ya Chama katika kuteua nani wachukue nafasi gani zenye maslahi kwao badala ya kufuata kanuni hata kama ni wasaliti wa chama.Hili limedhihirika huko Mkoani Kigoma ambako maamuzi ya haki toka kwa wana CCM wenye mapenzi na Chama chao kuonesha hadharani kuchoshwa na vitendo vya wakubwa walafi hao waliopewa rushwa nono ili kulazimisha mgombea maslahi wao kupita katika kugombea nafasi hiyo.Kitendo cha Mgombea uenyekiti wa Halmashauri ya Buhigwe kukosa kura za kutosha ni fundisho kwa Wala rushwa hawa sijui huko kibondo ambako wasaliti wa Chama waliopaswa kushughulikiwa wameshughulikiwaje lakini nako nadhani kwa vile kanuni hazina maana tena na wasaliti hao walishajihakikishia mamlaka kwenye kamati ya si Hasa kwa kuungana na upinzani wataendelea kupeta tu. Kiama kikuu chaja bila kusafisha Chama kwa kuwang'oa walafi hawa mtayaona makubwa upinzani halisi ulikuwa na Mizizi yake KIGOMA baadaye tukadhani adabu ingerudi lakini mliposhindwa kujirekebisha tukawapa kiboko kidogo kwa kuwapunguzia majimbo sasa mnataka tuwanyime yote? Shauri yenu msipojirekebisha na kuzingatia kanuni badala ya RUSHWA:A S 2152:.