Me nimeuliza tu kwa 7bu nimesikia kuna watu wanazinunua kwa bei mzuri sana ila kabla sijaiuza hii yangu naomba kujua wanazihitaji kwa madhumuni gani
Hakuna soko lake.
Sarafu zilizokuwa na thamani pekee ni rupia ya Mjerumani iliyotengenezwa kwa dhahabu ghafi.
Sarafu hiyo iliitwa Tabora, lakini haikuenea sana kwa kuwa wakati inatolewa ndiyo kipindi cha vita kuu ya1 ya dunia alipofurushwa Mjerumani kutawala Tanganyika.
Hizo coins Wajerumani wazilificha kwa kuchimbia maeneo mbalimbali nchini kutokana na kutokuwa na muda tena wa kufanya transaction pamoja na usafirishaji.
Walichokifanya waliweka mark za gps wanazozijua wao maeneo hayo kisha wakasepa.
Baadaye likaibuka kundi la matapeli.
Mbinu wanayoitumia ni kwamba, anazuka mtu mmoja na kuanza kueneza uvumi kama unavyoeneza wewe hapa na anakuwa kajikasimia pesa ya kupoteza kama mtaji.
Let say, anaandaa Laki 1 kwa ajili ya kuhalalisha uvumi wake huo na kuanza kununua coins alizoamua akidai kwamba zinatafutwa sana na zina thamani kubwa.
Kweli mtu atakapozikusanya na kumpelekea, anatazinunua hadi hapo atakapofikisha kiwango cha thamani ya fedha alizoamua kupoteza kama mtaji wake.
Uongo huo utaendelea kuzunguka kwa kasi na watafutaji wataongezeka na kumfikia yeye.
Ndipo atakapo wapiga kwa kuringa kabisa kwamba anazo na anajua kuwa zinatafutwa sana, kwa hiyo anawapigiza bei anayoitaka kwa kuwa watafutaji watakuwa na kitete cha kupata na hapo ndiyo unakuwa mwisho wa mzunguko.
Huyu mnunuzi wa mwisho aliyenunua kwa tapeli anaweza akabahatika kuziuza kutokana na uvumi utakavyokuwa umeimarika na kuenea.
Lakini baadaye zitabakia mikinoni mwa watu na wasijue pa kuzipeleka, kila mmoja akidai anasikia tu, lakini specific market anakuwa haelewi.
Ndugu yangu huo ni utapeli wa kawaida, huvumishwa na wavumishi wakiisha tengeneza faida yao ya kitapeli husizi na baadaye kuanza tena.
Kwa hiyo kama umepata soko, ziuze bila ya kujadili bei, vikuondokee mikononi mwako, sababu vitu hivyo havina thamani.
Labda kama wanaovitafuta ni watu wa malikale kwa ajili ya kuviweka makumbusho, hapo tunaweza kujadili vingine.