Rungu kakabidhiwa kichaa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rungu kakabidhiwa kichaa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mangaline, Jun 1, 2012.

 1. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli usiopingika, kuwa nchi yetu sasa inakabiliwa na matatizo mengi. Moja ya tatizo kubwa, ikiwa ni ubadhilifu wa fedha za umma, kuanzia serikali kuu hadi serikali za mitaa. Tatizo hili limeachwa kwa miaka mingi sasa, hadi kufikia kuonekana kama ndiyo staili ya maisha.
  Kutokana na mbinyo uliojitokeza ndani ya Bunge, hadi kupelekea kuaingusha serikali, sasa serikali mpya imeshtuka. Ofisi ya waziri mkuu, tawala za mikoa na serikali za mitaa, iliitisha semina kwa madiwani wote nchi nzima, na kuwapa majukumu ambayo sasa yamezua wimbi la mabalaza ya madiwani katika halmashauri mbalimbali kuanza kuwakataa wakuu wa idara, wakurugenzi wa halmashauri na hata wakuu wa wilaya.
  Hali hii inazua hali ambayo, sasa yawezekana wananchi wakaipenda sasa serikali yao, au chuki ikaongezeka.

  WAZO LANGU
  Unapo taka kutatua tatizo. litatue kwa busara ili tatizo lisije likakuletea matatizo.
   
 2. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Nimepita hapa!
   
 3. m

  mbalapala Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Naungana na wewe mkuu maana madiwani walivochaluka ni hatari.Huku kwetu wanapiga kura ya kutokuwa na imani na Mwenyekiti.Mambo si mambo.Acha tusubiri bana though vita haina macho
   
 4. D

  Davie Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni ujinga pale ambapo wanashindwa kujua sasa hili wimbi la maiwani kupewa nguvu hii sasa tushuhudie wataalam wakishindwa kufanya kazi zao kwa kuhofia kukosea na kukumbana na madiwani.
   
Loading...