Ruhusa ya wajawazito kurudi shule inavyowatesa Malawi.

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Wakuu natumai mmeaka salama.!

Malawi ni Moja ya Nchi ambazo zimelazimika kuwarudisha shule mabinti ambao walipata ujauzito wakiwa bado wanafunzi.
Mabinti hawa baada ya kujifungua wanarudi na kuendelea na masomo kama kawaida sambamba na hilo ni marufuku kwa mwalimu kumuadhibu mtoto kwa fimbo. Popote katika eneo la shule.

Nimepita karibu katika shule zote za Nchi hii toka Kalonga mpaka Sanje. Kusini kabisa Mwa Malawi. Pamoja na faida za misaada ya kiuchumi wanazopata kutoka wa wafadhiri kama kujengewa majengo mazuri ya shule na kuletewa vitendea kazi kama vitabu na madaftari.

Waalimu wengi wananung'unika kushuka kwa nidhamu, kwa watoto wa kizazi hiki mwanafunzi hana tena nidhamu kama iliyokuwepo hapo awali. Kwa shule za msingi na sekondari.

Pia athari za uzinzi na uasherati kwa sasa ni kama zimefunguliwa mlango zinaa imekuwa kitu cha kawaida sana katika jamii ambapo watoto wadogo sana unawakuta kwenye madanguro au sehemu za kuendesha biashara ya ngono!

Walimu wanaofundisha mabinti walio acha watoto nyumbani wanasema ni kama darasa zima linakuwa na wamama badala ya mabinti.

Sisi kama Tanzani ni vema tukawa makini kabla ya kuruhusu huu upuuzi kutoka kwa wajiitao wafadhiri..
 
Wameyapalilia wenyewe
 
Usijifiche nyuma ya hiyo habari, Ujumbe wako ni kuwa na wewe hukubaliani hawa mabint kurudi shule!

Hebu jiweke katika hali ya Uwewe ndio umepata mimba umejifungua na umri wako bado ni mdogo unakuruhusu kuendelea na shule lakini jamii yako haitaki urudi shule UTAJISIKIAJE?

Mnapozungumzia haya mambo muwe mnajivika "nafsi zenu" kwanza. (Ningelikuwa mimi)
 
Dunia imebadilika, watoto wanajifunza tabia za ajabu kupitia tekinolojia. Shuleni kwenyewe wanafundishwa jinsi ya kufanya scientific research kupata information zitakazowasaidia katika mijadala yao. Usiseme matumiza ya simu na iPad.

Adhabu ya viboko ikitolewa mashuleni, kuwa na adhabu mbadala ambazo ni kali kama
1. Kumuweka mtoto afanye reflection kwa kosa lake, na akubali kwa maandishi akilirudia wazazi wake wanafahamishwa.

Akirudia mtoto apewe suspension.

Baada ya suspension asupobadilika apelekwe jela ya watoto.

Hivi vinahitaji resources ndiyo matatizo.

Watoto ambao wako hatarini kupata mimba nurse wa shule awape ushauri wa contraceptives. Kuna sheria kuwa binti wa miaka 16 mwenye uelewa anaweza kufanya maamuzi pasi kuwafahamisha wazazi.
 
Wameyapalilia wenyewe
Wanadai ni.Nchi maskini wanahitaji Msaada kiukweli inatia hasira.
Hebu fikiri mama aliye na mtoto nyumbani amekaa dawati moja na binti yako kisha wana umri unaofanana.! Unategemea watakuwa na mazungumzo gani ya ziada.?
Je hayo mazungumzo yatakuwa na athari gani kwa huyu binti ambaye huenda alikuwa anajizuia asipate mimba au asiwe na mahusiano?! Hivi hili darasa kama lina vijana wa kiume je., mtazamo wao kwa mabinti walio bado fresh..unakuwaje.!
Leo hii ukipta huku Malawi
Sio ajabu kukuta binti kwenye mkoba wake wa shule ana powder na lipstick ana wanja na nk. Sabbu sheria za shule wala wizara hazikatazi, na binti ana uhuru. Wa kufanya hivyo.
 
Wazazi wawe karibu na watoto wao, umasikini usiwafanye kuwatoa kafara watoto!
 
Nakari
Dunia imebadilika, watoto wanajufunza tabia za ajabu kupitia tekinolojia. Shuleni kwenyewe wanafundishwa jinsi ya kufanya scientific research kupata information zitakazowasaidia katika mijadala yao. Usiseme matumiza ya simu na iPad.
Nakaribisha mdau tuungane kuanzisha 'Tanzania Young Mothers Schools'(TAYOMOS). Pamoja na masomo ya kawaida, tunawafundisha Ujasiriamali, ufundi, lishe, mazingira n.k. naamini tutapata ufadhili na kuendesha hizo shule kila kanda.
 
Ok so hii umeandika ili kusapoti CCM na kutoruhusu mjamzito kurudi darasani?

Kwanini nyinyi CCM msiwe mnaoutsource kazi ya kutetea blunder zikitokea?

Umesema Malawi nidhamu hakuna. Ila hujasema kama sababu ni kukosekana hivyo viboko au ni mtu kupata mimba na kurudi darasani.

Tufanye sababu ni kutokuepo adhabu ya viboko. Malawi ni nchi pekee ambayo haitekelezi hiyo adhabu? Zipo nyingine? Hizo nchi nyingine nidhamu imeshuka pia?

Kipimo chako ni kipi cha nidhamu?

Tanzania tuliwahi kupunguza idadi ya viboko, nidhamu ilishuka? Imeshuka?

Unasema watoto wanaenda na wanakutwa kwenye madanguro...

Mbona mtu kua kwenye danguro na uwepo wa sera ya kumruhusu kurudi darasani baada ya ujauzito ni vitu ambavyo havisababishani? Mtoto haendi danguroni kwakua kuna hiyo sera, mtoto huenda huko kwakua nyumbani chakula hakuna na ana mahitaji.

Kama hoja yako ni kulaumu uwepo wa sera. Tanzania tumeipindua hiyo sera, wale watoto waliokuepo Kimboka, Sokota, A, wamepungua? Hawajapungua?

Articles nyingi huiterm Malawi kama eneo ambalo mtoto wa kike huanza kufundwa mapema mno kiasi kwamba rate yao ya UKIMWI na kuvunjika ndoa ni kubwa. Hii haiwezi kua sababu ya watoto kujianika kwenye danguro kuliko hiyo ya uwepo wa sera?

Ok unajua kama kusoma ni haki ya binadamu? Sawasawa na kuishi? Ndiyo maana adhabu ya kunyongwa haitekelezwi siku hizi, si unajua?

Na unajua kama nchi yetu imesaini makubaliano mbalimbali ya kimataifa ya haki za binadamu? Kwa hiyo hata hii haki ya kusoma inabidi waitoe?

Anayekugomea msaada hakugomei kwakua umeiondoa hiyo sera, anakugomea kwa kua unavunja haki ya binadamu kupata elimu.
 
Hiyo mimba alipataje? Hakujua kuwa kupata mimba ni kosa kisheria.. ?
Mnasingizia kubakwa wangapi walio bakwa na wangapi wamepata kwa hiyari yao wenyewe?..
Umeme ni hatari mbona hatuoni watu wakifa kila siku kwa kushika waya za umeme.? Lets teach our young nidham na heshima ya maisha badala ya kutafuta shortcut. Binti ajue kuwa akipata mimba ndio basi story ya maisha yake imebadirika sio binti tena na mama na majukumu yake yamebadirika ni kulea sio kusoma!

Akitaka kusoma ajue kuwa hilo ni jukumu lake kwa wakati wake sio kwa wakati ule ambao alipaswa kusoma sabbu bila shaka hakuzingatia alilopaswa kulifanya "fullstop."
Hayo mengine tunajitakia matatizo ambayl baadae yatatengeneza kilio kingine.
Usijifiche nyuma ya hiyo habari, Ujumbe wako ni kuwa na wewe hukubaliani hawa mabint kurudi shule!

Hebu jiweke katika hali ya Uwewe ndio umepata mimba umejifungua na umri wako bado ni mdogo unakuruhusu kuendelea na shule lakini jamii yako haitaki urudi shule UTAJISIKIAJE?

Mnapozungumzia haya mambo muwe mnajivika "nafsi zenu" kwanza. (Ningelikuwa mimi)
 
Hiyo mimba alipataje? Hakujua kuwa kupata mimba ni kosa kisheria.. ?
Mnasingizia kubakwa wangapi walio bakwa na wangapi wamepata kwa hiyari yao wenyewe?..
Umeme ni hatari mbona hatuoni watu wakifa kila siku kwa kushika waya za umeme.? Lets teach our young nidham na heshima ya maisha badala ya kutafuta shortcut. Binti ajue kuwa akipata mimba ndio basi story ya maisha yake imebadirika sio binti tena na mama na majukumu yake yamebadirika ni kulea sio kusoma!

Akitaka kusoma ajue kuwa hilo ni jukumu lake kwa wakati wake sio kwa wakati ule ambao alipaswa kusoma sabbu bila shaka hakuzingatia alilopaswa kulifanya "fullstop."
Hayo mengine tunajitakia matatizo ambayl baadae yatatengeneza kilio kingine.

SWALI KWA HERUFI KUBWA, UNAUNGA MKONO HAWA MABINT KURUDI SHULE AU NDIO IWE MWISHO WA KUPATA ELIMU?

Tuanzie hapo nisije nikawa nabishana bure tu nawewe.
 
Una matatizo na Neno "CCM" inawezekana kwako ni kama jinamizi kila ukisikia CCM unaweweseka.
Sio kila haki za binadamu ni haki sahihi kwa maendeleo na Afya ya Jamii yako kuna wakati misingi imara ya kijamii inapuuza hizo mnazoita haki za binadamu.

Kuna mikataba ya ajabu Taifa limesainishwa na watu wapuuzi walafi ambao nyinyi leo "Upinzani" mnawatetea kwa misingi ya mnachoita haki za binadamu. Nchi inaingia kwenye matatizo sabbu ya wale Mchwa na vyeti vya kubumba waliokuwa wamejazwa na mabwana zenu kwenye mifumo ya serikali leo
Rais anajaribu kuitoa Nchi kwenye makucha na uozo ule mnamwita dikteta. Na wale waliofanya ule upumbavu kwenu ni mashujaa wanaopaswa kutetewa.

Mtoto wa kike ana haki na heshima yake katika jamii yetu anaheshimiwa na kutunzwa lakini akipata mimba hilo akiwa shule hilo halina msamaha. Sehemu yake sahihi ni Nje ya shule.
Hilo liko wazi hata nyumbani kwenu binti akipata mimba kabla ya ndoa na kuzalia pale nyumbani je heshima yake inaongezeka? Au inapungua na kuondoka kabisa katika jamii yake?
Ok so hii umeandika ili kusapoti CCM na kutoruhusu mjamzito kurudi darasani?

Kwanini nyinyi CCM msiwe mnaoutsource kazi ya kutetea blunder zikitokea?

Umesema Malawi nidhamu hakuna. Ila hujasema kama sababu ni kukosekana hivyo viboko au ni mtu kupata mimba na kurudi darasani.

Tufanye sababu ni kutokuepo adhabu ya viboko. Malawi ni nchi pekee ambayo haitekelezi hiyo adhabu? Zipo nyingine? Hizo nchi nyingine nidhamu imeshuka pia?

Kipimo chako ni kipi cha nidhamu?

Tanzania tuliwahi kupunguza idadi ya viboko, nidhamu ilishuka? Imeshuka?

Unasema watoto wanaenda na wanakutwa kwenye madanguro...

Mbona mtu kua kwenye danguro na uwepo wa sera ya kumruhusu kurudi darasani baada ya ujauzito ni vitu ambavyo havisababishani? Mtoto haendi danguroni kwakua kuna hiyo sera, mtoto huenda huko kwakua nyumbani chakula hakuna na ana mahitaji.

Kama hoja yako ni kulaumu uwepo wa sera. Tanzania tumeipindua hiyo sera, wale watoto waliokuepo Kimboka, Sokota, A, wamepungua? Hawajapungua?

Articles nyingi huiterm Malawi kama eneo ambalo mtoto wa kike huanza kufundwa mapema mno kiasi kwamba rate yao ya UKIMWI na kuvunjika ndoa ni kubwa. Hii haiwezi kua sababu ya watoto kujianika kwenye danguro kuliko hiyo ya uwepo wa sera?

Ok unajua kama kusoma ni haki ya binadamu? Sawasawa na kuishi? Ndiyo maana adhabu ya kunyongwa haitekelezwi siku hizi, si unajua?

Na unajua kama nchi yetu imesaini makubaliano mbalimbali ya kimataifa ya haki za binadamu? Kwa hiyo hata hii haki ya kusoma inabidi waitoe?

Anayekugomea msaada hakugomei kwakua umeiondoa hiyo sera, anakugomea kwa kua unavunja haki ya binadamu kupata elimu.
 
"SIUNGI MKONO HAO MABINTI KURUDI SHULE"
elimu aitakayo aweza kuipata kwa mazingira mengine sahihi kwake kwa wakati wake na sio kwa nafasi ya shule aliyo ipoteza.
SWALI KWA HERUFI KUBWA, UNAUNGA MKONO HAWA MABINT KURUDI SHULE AU NDIO IWE MWISHO WA KUPATA ELIMU?

Tuanzie hapo nisije nikawa nabishana bure tu nawewe.
 
Wakuu natumai mmeaka salama.!
Malawi ni Moja ya Nchi ambazo zimelazimika kuwarudisha shule mabinti ambao walipata ujauzito wakiwa bado wanafunzi.
Mabinti hawa baada ya kujifungua wanarudi na kuendelea na masomo kama kawaida sambamba na hilo ni marufuku kwa mwalimu kumuadhibu mtoto kwa fimbo. Popote katika eneo la shule.

Nimepita karibu katika shule zote za Nchi hii toka Kalonga mpaka Sanje. Kusini kabisa Mwa Malawi. Pamoja na faida za misaada ya kiuchumi wanazopata kutoka wa wafadhiri kama kujengewa majengo mazuri ya shule na kuletewa vitendea kazi kama vitabu na madaftari.
Waalimu wengi wananung'unika kushuka kwa nidhamu, kwa watoto wa kizazi hiki mwanafunzi hana tena nidhamu kama iliyokuwepo hapo awali. Kwa shule za msingi na sekondari.
Pia athari za uzinzi na uasherati kwa sasa ni kama zimefunguliwa mlango zinaa imekuwa kitu cha kawaida sana katika jamii ambapo watoto wadogo sana unawakuta kwenye madanguro au sehemu za kuendesha biashara ya ngono!
Walimu wanaofundisha mabinti walio acha watoto nyumbani wanasema ni kama darasa zima linakuwa na wamama badala ya mabinti.

Sisi kama Tanzani ni vema tukawa makini kabla ya kuruhusu huu upuuzi kutoka kwa wajiitao wafadhiri..
Hili jambo sometiems siyo sometimes ndiyo,
Kuna mdada flani wakati tuko kidato cha nne kumbe akawa amepigwa mimba akashindwa fanya paper akakaa nyumbani akajifungua, kumbe baadae alienda shule private bila kusema kuwa ana mtoto akarudia kidato cha nne akafaulu, akenda pcm form six akapiga one moja kali akena UDSM ninapozungumza kwa sasa ni mhandisi mmoja matata sana anakula maisha wakati sisi tuliomtangulia katupga bonge la gap.
SOmetimes mtu akipata second chance anafanya poa sana ila pia ina matatizo yake maana wengi wanaogopa jihusisha na mapenzi wakihofia kupoteza masomo za hiyo hofu ikiondoka pia ni tabu
 
Wakuu natumai mmeaka salama.!
Malawi ni Moja ya Nchi ambazo zimelazimika kuwarudisha shule mabinti ambao walipata ujauzito wakiwa bado wanafunzi.
Mabinti hawa baada ya kujifungua wanarudi na kuendelea na masomo kama kawaida sambamba na hilo ni marufuku kwa mwalimu kumuadhibu mtoto kwa fimbo. Popote katika eneo la shule.

Nimepita karibu katika shule zote za Nchi hii toka Kalonga mpaka Sanje. Kusini kabisa Mwa Malawi. Pamoja na faida za misaada ya kiuchumi wanazopata kutoka wa wafadhiri kama kujengewa majengo mazuri ya shule na kuletewa vitendea kazi kama vitabu na madaftari.
Waalimu wengi wananung'unika kushuka kwa nidhamu, kwa watoto wa kizazi hiki mwanafunzi hana tena nidhamu kama iliyokuwepo hapo awali. Kwa shule za msingi na sekondari.
Pia athari za uzinzi na uasherati kwa sasa ni kama zimefunguliwa mlango zinaa imekuwa kitu cha kawaida sana katika jamii ambapo watoto wadogo sana unawakuta kwenye madanguro au sehemu za kuendesha biashara ya ngono!
Walimu wanaofundisha mabinti walio acha watoto nyumbani wanasema ni kama darasa zima linakuwa na wamama badala ya mabinti.

Sisi kama Tanzani ni vema tukawa makini kabla ya kuruhusu huu upuuzi kutoka kwa wajiitao wafadhiri..
Na Zanzibar je inahusika?
 
"SIUNGI MKONO HAO MABINTI KURUDI SHULE"

Point yako ilikuwa ni hiyo na ndio maana nilisema usijifiche kwenye kichaka cha hiyo habari ili kuhalalisha hoja yako.

Nachoweza kusema tu "Jifanye ndio wewe umepata mimba au ni mzazi wa bint aliyepata mimba" Utapenda uendelee/aendelee kukaa nyumbani?
 
Tatizo kuna kiongozi anapayuka majukwaani huku akijifanya kuwatunishia misuri wajomba. Kwani wakati wa kikwete wanafunzi wajawazito waliendelea na masomo?? Ukweli ni kwamba walikuwa wanaondolewa kimya kimya wakibahatika sana waliokuwa kidato cha mtihani wa taifa hasa form four walikuja fanya tu mitihani
 
Kwani mtoto aliyejifungua mtoto akirudi shule watanzania mnapungukiwa Nini!? Amalize tuu elimu yake ya secondary akifauru aendelee na masomo...

Mimi sioni tatizo lolote... Ugumu ukowapi kama sio roho mbaya za koroshow... Watoto wa kike wana haki ya kupata elimu sawa na mtoto wa kiume alompa mimba mtoto mwenzake wa kike...

ELIMU NI HAKI YA KILA RAIA KWA HIARI KAMA ANAPENDA
 
Kila jambo lina wakati wake. Ni vizuri watoto wetu wakawekewa mipaka na kujua kuwa kuna gharama (consequences) kwa kufanya mambo fulani kabla ya wakati. Hakuna anayemwonea wivu mtoto wa kike aliyezaa akiwa mwanafunzi. Tunapenda kila binti ajue kuwa uzazi unaweza kusubiri.
 
Back
Top Bottom