Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,619
Ninayoyaona:-
1. Sijaona utaratibu wa kudhibiti ukosefu wa uvumilivu wa hoja mbadala zaidi ya mfumo wa asili wa kutumia mkono wa dola. Hii itakwaza mchakato wa ukuaji demokrasia. Tutamani kufika kwenye kiwango cha ustaarabu wa kuondoa matumizi ya vikosi kwenye harakati za kukuza demokrasia yetu.
2. Makada wahanga wa chaguzi-za-machozi; za ndani ya vyama wanaenda kufanya malipizi kwa vyama vyao vilivyowatema; kwa kuendesha fitna. Kuna haja ya vyama kuwaponya majeraha hawa mapema ya mikutano hiyo kushika moto.
3. Bunge lijiandae kupokea enzi mpya ya changamoto toka upinzani 2025. Tutaanza na chaguzi ndogo kabla ya 2025 kwa majimbo na kata zitazobaki wazi kwa sababu mbalimbali. Hii inaenda kutupatia picha ya 2025.
4. Utaratibu wa vibali vya mikutano hii bado ni ule ule wa zamani uliokuwa ukilalamikiwa. (Hakuna jipya).
5. Matumizi sawia ya haki (kwa vyama vyote) ya TBC, TBC1, Daily News, Habari Leo, Habari Maelezo bado hayajaainishwa hadi sasa.
6. Namba 5 hapo juu inahusu pia viwanja vya mikutano ya hadhara.
7. Vyama vilivyoomba usajili wa kudumu vipewe ili viingie ulingoni kabla ya 2025 kama sehemu ya kukuza demokrasia yetu. Hili nalo umma hauoni kama likifanyika.
8. Ruhusa hii ni shinikizo la wafadhili au imetokana na mazingira halisi ya matakwa yetu ya ndani? Kama imetoka nje basi uhuru wetu bado uko mateka kwa wafadhili.
9. 2025 tumejiandaa kufanya uchaguzi kwa fedha za ndani 100% ili kulinda sovereignty yetu au tumejiandaa kukinga bakuli ili baadaye tuingiliwe kwenye uchaguzi na wafadhili wetu wataotaka kupenyeza maslahi yao?
10. Tumeruhusu mikutano sawa, lakini je, tumekumbuka kuhoji Katiba yetu iruhusu matokeo ya kura za rais yahojiwe kortini? Kama la, tutasemaje kuwa malengo ya vyama vya siasa ni kushika dola?
11. Namba 10 hapo juu inahusu pia wagombea binafsi.
12. Sijaona kama vyama vimeandaa agenda zaidi ya wagombea (ambao hawajajulikana) kuwa na agenda binafsi.
13. Naona wananchi wana agenda lakini siyo vyama. Na kama vyama vinavyo basi zitakuwa zinasighishana na agenda ya wapigakura.
14. Suala la Wabunge 19 wa Chadema linaning'inia kwenye usawa (hanging in the balance), Mihimili yote haina majibu yake. Majibu ya Katiba ya taifa na ya Chadema yametwezwa na kukataliwa.
Hayo yafanyiwe kazi.