Ruhusa Kwa Wafanyakazi wa Serikali kusafiri Nje ya Nchi

Kuanzia sasa kila mtumishi wa serikali anayetaka kusafiri nje ya nchi, anatakiwa kupata kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, ofisi ya Rais, Ikulu, kupata fomu "TFN 773", maombi hayo yawe yamemfikia wiki moja kabla ya safari.

Mtumishi wa serikali atakayesafiri nje ya nchi bila kupata kibali na kuwa retrospective approval" kitatolewa kama kuna dharura na kinaweza kutolewa kwa njia ya simu.
Pia maombi yatapelekwa kwake sio kama formality, bali yatahitaji maamuzi kabla ya kibali kutolewa.

My Take:

1) Chief Secretary wa Ikulu ataweza ku deal na maombi yote ya Wafanyakazi wa Serikali ili wapate majibu katika wiki moja kama anavyosema? Sina hakika kama hili litawezekana hasa ukizingatia kwamba serikali imesambaa kutoka Kasulu hadi Nyasa!

2) Swala la kutoa vibali kusafiri nje ni priority kiasi hicho hadi liende kwa Katibu Mkuu? Hakuna mambo mengine ya maana zaidi katika kipindi hiki ambacho nchi ina lundo la matatizo?

3) Zoezi hili linakusudia kuwabana wafanyakazi wa ngazi ipi? Ni wazi kwamba wanaosafiri zaidi ni wakubwa wenyewe, kwa nini linawabe hata wadogo wanaosaffiri mara moja kwa Mwaka?

4)....

5)

Kwa kweli hii inashangaza sana. Kila kona ya nchi kuna wateule wa Rais kwa majina ya Mkuu wa Mkoa/Wilaya. Ukienda vyuoni kuna VC, Wizarani Makatibu wakuu nk. Jamaani wana kazi gani hawa? Kama hawana majukumu kwanini wawepo? Hivi huyo Katibu Mkuu anatoa pesa kuwasafarisha watu nje ya nchi?





Ni mbaya, umejitafutia short course kwaajili kuongeza ujuzi wa kazi. Ruhusa inasumbua. Unaenda konferensi ya siku moja Kenya kibali kwa Katibu mkuu kiongozi. Yaani nitpke Arusha niende Dar kufuata kibali wakati safari yangu ni Kenya!






Naamini Katibu Kiongozi ana mambo mengi tena yenye tija kwa nchi hii. Ni bora aachiwe hayo mengine wayafanye wateule wengine wa Rais.r
 
na wale wa apollo, lazma wafe kabla vibali havijatoka! kazi ipo!

Imagine uko Kasulu ukapata ka safari ka kwenda kuosha macho kwenye ujirani mwema huko rwanda/Burudi lazima upate ruhusu ya Ikulu? Kwani kuna haja ya kuongelea utendaji wa kazi wa serikali zetu??
 
Back
Top Bottom