Ruhusa Kwa Wafanyakazi wa Serikali kusafiri Nje ya Nchi

Sumba-Wanga

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
5,349
1,224
Kuanzia sasa kila mtumishi wa serikali anayetaka kusafiri nje ya nchi, anatakiwa kupata kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, ofisi ya Rais, Ikulu, kupata fomu "TFN 773", maombi hayo yawe yamemfikia wiki moja kabla ya safari.

Mtumishi wa serikali atakayesafiri nje ya nchi bila kupata kibali na kuwa retrospective approval" kitatolewa kama kuna dharura na kinaweza kutolewa kwa njia ya simu.
Pia maombi yatapelekwa kwake sio kama formality, bali yatahitaji maamuzi kabla ya kibali kutolewa.

My Take:

1) Chief Secretary wa Ikulu ataweza ku deal na maombi yote ya Wafanyakazi wa Serikali ili wapate majibu katika wiki moja kama anavyosema? Sina hakika kama hili litawezekana hasa ukizingatia kwamba serikali imesambaa kutoka Kasulu hadi Nyasa!

2) Swala la kutoa vibali kusafiri nje ni priority kiasi hicho hadi liende kwa Katibu Mkuu? Hakuna mambo mengine ya maana zaidi katika kipindi hiki ambacho nchi ina lundo la matatizo?

3) Zoezi hili linakusudia kuwabana wafanyakazi wa ngazi ipi? Ni wazi kwamba wanaosafiri zaidi ni wakubwa wenyewe, kwa nini linawabe hata wadogo wanaosaffiri mara moja kwa Mwaka?

4)....

5)
 
na bado utawaona watu wamevaa nguo za kijani na yellow! huwa siwaelewi kabisaaaaaaaa, ni bora kuvaa nyeusi, kuonyesha msiba tulionao nchini mwetu, mpaka 2015, tutakuwa tumemaliza kukaa matanga!
 
Kwlei kabisa, badala ya kutatua matatizo ya muhimu yanayowakabili wafanyakazi, tumekuwa busy kuwakandamiza zaidi!
 
Mbona ilikuwepo hilo tangu zamani kwenye standing order ya mwaka 2009? Ruhusa lazimaupate kwa katibu mkuu utumishi, au labda sijakuelewa.

Mkuu ni Katibu Mkuu Kiongozi (chief Secretary) wa Ikulu!
 
Ina maana mkulu naye anatakiwa kupewa hiyo ruhusa au yeye akiamua kuondoka hana haja ya kufanya hivyo? Kuna watu wengine huko serikalini ambao wao kwenda nje ni kugusa tu na kwa maana hiyo nahisis kama katibu mkuu anaweza kujikuta akishughulikia maombi ya watu wale wale kila siku. Sasa sijui haya ya wengine nani atayafanyia kazi!!
 
Jambo la kujiuliza ni kwamba hii ina lenga kumbana nani???
 
SERIOUSLY???? this is very funny, ha! unaripoti kwa kipi hasa au wantaka kuwabana wezi wao?? manake mi sio tatizo ukienda nje ya nchi kwa private issue zako then uripoti ikulu???? kweli serikali inko na pesa, ina maana ataajiriwa mtu wa kuhakiki hivyo vibali tena sio mtu watu, upande mwingine wa shilingi watu wanalia ajira then wengine wanatafuta mwanya kupean.... aha Tanzania nchi yangu na kupenda weeeeee!
 
Serikalini utaratibu huo upo toka tupate uhuru! Hata kwenda kwenye mikutano ya ujirani mwema kwa baadhi ya mikoa inabidi kupata kibali toka ikulu au mambo ya nje. Sema kwasababu ya udhaifu, watumishi wengi wanavuka mipaka na kwenda nchi jirani kufanya shopping bila ya hivyo vibali!
 
Wafanyakazi wote waombe kibali kwa Ikulu?
KWa chief Secretary.
 
Kuanzia sasa kila mtumishi wa serikali anayetaka kusafiri nje ya nchi, anatakiwa kupata kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, ...............ofisi ya Rais, Ikulu, kupata fomu "TFN 773", maombi hayo yawe.................

Pls fafanua; safari zipi?
Za kikazi ? au hata personal?
 
Kuanzia sasa kila mtumishi wa serikali anayetaka kusafiri nje ya nchi, anatakiwa kupata kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, ofisi ya Rais, Ikulu, kupata fomu "TFN 773", maombi hayo yawe yamemfikia wiki moja kabla ya safari.

Mtumishi wa serikali atakayesafiri nje ya nchi bila kupata kibali na kuwa retrospective approval" kitatolewa kama kuna dharura na kinaweza kutolewa kwa njia ya simu.
Pia maombi yatapelekwa kwake sio kama formality, bali yatahitaji maamuzi kabla ya kibali kutolewa.

My Take:

1) Chief Secretary wa Ikulu ataweza ku deal na maombi yote ya Wafanyakazi wa Serikali ili wapate majibu katika wiki moja kama anavyosema? Sina hakika kama hili litawezekana hasa ukizingatia kwamba serikali imesambaa kutoka Kasulu hadi Nyasa!

2) Swala la kutoa vibali kusafiri nje ni priority kiasi hicho hadi liende kwa Katibu Mkuu? Hakuna mambo mengine ya maana zaidi katika kipindi hiki ambacho nchi ina lundo la matatizo?

3) Zoezi hili linakusudia kuwabana wafanyakazi wa ngazi ipi? Ni wazi kwamba wanaosafiri zaidi ni wakubwa wenyewe, kwa nini linawabe hata wadogo wanaosaffiri mara moja kwa Mwaka?

4)....

5)
Too much big goverment.control how people live their lives.Thats why I'm proud republican small government is the solution .mambo ya Nyerere hayo yanarudi
 
jamani huu ndio utaratibu toka zamani ni lazima ujaze kipi kipya hapo?
OK, huyo wa sasa ndiye mpya, sababu hata kama yalikuwapo hayo ilikuwa ni wajibu wa serikali kuoa pesa ya kukusaidia ukiwa ugenini. Wapo waliopata lakini wengi nikiwamo mimi sijawahi kupata kwa kuwa sina mjomba huko. Hata majibu ya form ile niliyoijaza sina majibu mpaka leo miaka 16 imepita. Waliopata waliniambia walipata kiulaini tu ila majina yao ni makubwa. Hata niliporudi waliendelea kunirusha kichura sitambuliwi na hata nilichokileta hawakitambui hadi leo.
My take: wanatafuta fursa nyingine ya rushwa maana sasa wamegundua watu hawaendi kukata kitu kidogo kule. Na mbado.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom