bomouwa
JF-Expert Member
- Jun 19, 2014
- 1,149
- 800
Nimekua nikisikia jinsi baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva ambao wengi hatukatai kama kampuni ya clouds media group na ile ya zamani ya prime time promotion imefanya mengi hususani katika muziki huu wa kizazi kipya na kufanya wasanii wa kitanzania kutambulika saaana ndani na hata nje ya mioaka ya nchi, kwakweli kwa hapo nawapa hongera zao saana.
Lady jaydee ni mkongwe katika mziki wa bongo na mara kwa mara alikua akisikika akisema kua ananyonywa na watu wachache lakini pia katika kipindi cha mkasi Gadna alikiri kwakusema swala la Mke wake na clouds media group lingeweza kuzungumzwa lakini kimsingi hapa ni kwamba Ladyjaydee alichoka na manyanyaso ya uongozi hapa alimzungumzia Ruge na ilifika mahali Jide aliapa kabisa kua hata akifa basi clouds wasije piga nyimbo wala kuomboleza kwa namna yoyote ile na akaongeza hata msibani Ruge asije kuzika, ukitafakari ni maneno magumu na mazito.
Nimejaribu kutafakari juu ya maneno yaliokua yanasemwa juu ya diamond katika shoo yake ya fiesta pale leaders club ambapo alizomewa saaana na mashabiki waliosemekana wametumwa na watu fulani ambao hata hivo hawakutajwa, lakini wakati huohuo Ali kiba alishangiliwa mnoo na dhahiri ilionyesha wazi kuna jambo nyuma ya pazia linaendelea ambalo watu baki hatuelewi... Watanzania tunapenda kufata mkumbo na ndo maana hata hatujui mustakabali ya yale tuyafanyayo.
Diamond amekua balozi kwa nguvu na jasho lake mwenyewe na ubunifu hata kufanya tanzania ijulikane zaidi na ndo maana hata tuzo anapata kwa wingi maana kiukweli kabisa ANAJITUMA na kwa hilo anastahili pongezi nyingi na watanzania tumpe haki yake.
CLOUDS FM wameibuka kwa kumpa promo Ally kiba ya ajabu saana yaani kila dakika 5 lazima usikie tangazo lake kimsingi si jambo baya lakini hii yote inasemekana ni juhudi za kuuzima ufalme wa kijana Diamond maana wanasema amekataa kua chini ya menejiment ya Ruge na badala yake akamkubali babu tale swala ambalo sasa clouds wameamua kumkomoa na Dj fetty kwa kipindi fulani alisema hajui kelel za kumzomea diamond zilitoka wapi lakini wenyewe kwa wenyewe wanasema "bosi hamtaki hata kumsikia".
MY TAKE
Ruge kama hela unazo na ikumbukwe tu kwa imani zetu za dini Mungu hapendi chuki wala hapendi kabisa dhuluma na kama unataka maisha ya pepo basi watendee mema kama kweli unania ya dhati ya lkuendeleza vijana hawa katika tasnia ya mziki na Mungu atakubariki.
Ieleweke mimi simtetei mtu ila mtu mwenye juhudi na asaidiwe.
Nawasilisha