Ruge Mtahabwa, Umebug men!!!!!

Ruge Mtahabwa, Umebug men!!!!!

ntamaholo

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
12,950
Reaction score
6,981
salam wakubwa.

Nimeanza na Ruge kwa kuwa ndiye meneja wa suala hili. Ni juu ya yeye na timu yake ya clouds fm, kuwaleta Black Leopard ya Africa Kusini.

Baada ya timu hiyo kucheza DSM, ikafungwa 3-1 kama sijanukuu vibaya, inakadiriwa kwa watu waliohudhuria waliaweza kupata pesa milion 70/-. Lakini ukiziweka kwenye ratio za kisoka, inasemekana walipata milion 40/- tu kitu ambacho ni hasara kubwa kwa maandalizi na gharama walizoingia kuileta na kuwalipa Yanga.

Jamaa hawakukoma, wakajipa moyo kuwa DSM wakivuruga, Mwanza watapata pesa za kufidia hasara hiyo. Hivyo matangazo kedekede yakaanza, na jana saa kumi na nusu, Yanga ilikipiga na hao wageni, na kama kawaida yanga 2, wageni 1.

Lakini ukija kwenye mapato, wamepata jumla ya milion 22, ambazo ukizigawa kwenye ratio za kisoka, wameendeleza hasara ya kufungua mwaka 2013. Kwani inasadikikika kuwa, kuwaleta Yanga na wageni wao hapa mwanza, tiketi ya ndege tu, zimekula zaidi ya milion 100/-

Nasema wamebugu kwa haya yafuatayo.

1. Kushindwa kupima upepo wa kiuchumi, kuwaleta wageni kwa gharama kubwa ukitegemea kuvuna kingi wakati unaowaletea burudani, ndo kwanza wana msongo wa mawazo vipi watamudu ada za watoto wao mashulen, vyakula havikamatiki na masuala mengine mhimu.

2. Kushindwa kuchagua siku nzuri za kuchezesha mechi hiyo, kwani Jumatano siyo siku sahihi, wengi wako kikazi zaidi, na hili limechangia pia kuwepo kwa watazamaji kiduchu uwanjani.

3. Hasira za HASARA waliyoipata, kuamua kuwasukumia wadau wengine jijini mwanza.
a) Watu waliokodiwa kwa ajili ya usafiri kwa makubaliano ya kulipwa laki, mwisho wa siku walilipwa 60,000/- kitu ambacho waligoma ikawalazimu polisi wa ulinzi kutuliza fujo hiyo, kwani mitaa ya mwanza hotel, iligeuka uwanja wa fujo, watu wakigombea hela. Mwisho wa siku, wamelipwa 80,000 na baadhi yao wamesusa kuchukua mshiko huo.
b) Polisi wenyewe pamoja na kuoneshewa dharau na timu ya clouds fm, nao waliambuliwa patupu pamoja na kuwa walifanya kazi hiyo hadi saa tano usiku. Hali hii ilizua mtafaruku, kwani baadhi ya askari waliendelea na majukum bila kula chochote tangu saa tatu hadi saa tano usiku walipotawanyika Mwanza hotel.
c) wakataji wa tiketi nao wamelambishwa hasara ya clouds fm, kwani malipo yao kwa siku, ilibidi yashuke kwa asilimia 50 ya makubaliano yaliyofikiwa,

4. Ugomvi wa kugawana mapato kiduchu yaliyopatikana. Ikumbukwe kuwa, utartibu wa kisoka, unajumlisha mwandaaji, TFF na Uongozi wa Kiwanja ukiongozwa na mzee Tegete. Makundi haya matatu mwisho wa siku walitaka kuzipiga, Puwepo wa polisi ukanusuru ugomvi huo japokuwa matusi ya nguoni na ubabe havikutiishwa na uwepo wa polisi wale. Watu waitukana, na kutaka kutunishiana misuli lakini polisi iliwaamua.

Narudia kusema, CLOUDS FM MMEVURUGA. Iweje hasira yenu wenyewe kwa kutokuwa makini mlazimishe ile na kwatu wengine wsiohusika na swaga zenu? Au kwa kuwa mmezoea kuwadhulum wasanii mbalimbali, roho hiyo mnataka muirudishe na kwa wananchi wengine?

MMEBUG, MMEVURUGA, na bado hamjakoma, kwani leo nasikia mmeandaa Simba kucheza na vibonde hivi toka kwa madiba. Kweli mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu, kuwadhulum wasanii wa nyimbo mmekuwa mkifurahia sana, lakini yamewageukia katika soka, mnatafuta wa kummeza. Nyie ni hovyo na hopeless kabisa. Naona umhimu wa ANT-VIRUS activists, Mungu awalinde wahakikishe wanaondoa unyonyaji wenu.

UPDATES:

Nini matokeo ya simba na hawa vibonde? vipi mwitikio wa wakazi wa dsm? wameingia kwa wingi na hivyo kuziba hasara waliyoipata?
 
kama wataieleza, natamani ningesikia uchambuzi wao hawa mbwiga.
 
Toka yule meneja wa creativity alipoondoka clouds imeshuka sana! Hakuna kipya na mvuto umepungua.saiv wanabebwa kwa historia ya jina(brand) waliojenga zaman...soon they will collapse!
 
Kikubwa hapa kwangu hapa ni kwamba Clouds wamepata hasara baaaaaasi!!!!!!!
 
Hivi hiyo timu kule kwao inacheza ligi daraja la sita sijui
 
mbona nimeangalia tbccm naona watu kibao au hao wametoa 3000 nini? ndo maana watu wanataka chao mapema ndio vingine vinafuata tatizo na wao waandaji wameingia mkenge kwanini wasichukue hao ndio mengine yafuate..

ngoja tuone na mnyama itapatikana shilingi ngapi..
 
Hivi hiyo timu kule kwao inacheza ligi daraja la sita sijui

hii timu iko PSL bibie sema iko mwishoni mwa msimamo wa ligi yaani ni sawa wacheze na toto afrika ua oljoro jkt hivi..
 
Ni ngumu sana. Hawawezi 'kujichambua' na kujitathmini.

wewe si unakumbuka ya shadaka (shafi dauda kajuna) kwenye DRFA kapigwa chini kasingizia alikuwa anafanya uchunguzi sasa hivi wanasema ynga na simba watajifunza jinsi ya kupata kit sponsor subiri tuwasikilizie kenye blog zao..
 
Toka yule meneja wa creativity alipoondoka clouds imeshuka sana! Hakuna kipya na mvuto umepungua.saiv wanabebwa kwa historia ya jina(brand) waliojenga zaman...soon they will collapse!

hakika, kwani taarifa nilizozipata, hata baadhi ya matamasha ya fiesta waliambulia patupu! lakini Mwosha huoshwa
 
wewe si unakumbuka ya shadaka (shafi dauda kajuna) kwenye DRFA kapigwa chini kasingizia alikuwa anafanya uchunguzi sasa hivi wanasema ynga na simba watajifunza jinsi ya kupata kit sponsor subiri tuwasikilizie kenye blog zao..

alikuwepo na tumbo lake, kifupi alikuwa mpoleeeee sana tu.
 
mbona nimeangalia tbccm naona watu kibao au hao wametoa 3000 nini? ndo maana watu wanataka chao mapema ndio vingine vinafuata tatizo na wao waandaji wameingia mkenge kwanini wasichukue hao ndio mengine yafuate..

ngoja tuone na mnyama itapatikana shilingi ngapi..

itakuwa nimwendelezo wa hasara, kwani mpaka sasa ili warudishe japo fedha yao, inatakiwa mapato ya kubaki kwao, baada ya mgao wapate zaidi ya milion 200/-. sasa kwa simba watazipata wapi? watalaamu wa michezo wanasema, Dar Yanga African, kwa dsm na nchini kote, ina mashabiki wengi zaidi ilikinganishwa na simba. so kama yanga walipata milion 70s, basi kwa simba wataambulia mil. 20/- tu ikizingatiwa timu yenyewe (black leopard) ishapoteza mvuto kwa watanzania.
 
wewe si unakumbuka ya shadaka (shafi dauda kajuna) kwenye DRFA kapigwa chini kasingizia alikuwa anafanya uchunguzi sasa hivi wanasema ynga na simba watajifunza jinsi ya kupata kit sponsor subiri tuwasikilizie kenye blog zao..
Nakumbuka sana ishu hiyo. Hawa jamaa wamezoea kuwapiga panga wanamuziki, sasa naona wameingia kwenye soka! Sugu alipokua analalamikia ubabe wao wengi walimuona ana wivu. Waandike na hii kwenye blogz zao, kwamba wamedhulumu wenye mabasi Mwanza
 
nirushie moja ya blog zao niidurusu mara moja, naweza kuta jambo huko
 
Haya bwana siye mashabiki tunachekelea ushindi tu, mengine yote watajijua wenyewe...
 
Back
Top Bottom