Rufaa ya Zombe yatinga kortini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rufaa ya Zombe yatinga kortini!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Buchanan, Oct 8, 2009.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Oct 8, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  DPP atoa sababu 11 kupinga hukumu yake!

  Na Happiness Katabazi.

  HATIMAYE Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Eliezer Feleshi, amewasilisha rufaa yake kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu na kuwaachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na wenzake wanane waliotuhumiwa kwa mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi.
  Rufaa hiyo iliwasilishwa katika Mahakama ya Rufani, jana saa 9:00 alasiri na kupewa namba 254/09 ambapo ilitiwa saini na Msajili wa Mahakama ya Rufani, Francis Mutungi.
  Katika rufaa hiyo ambayo Tanzania Daima inayo nakala yake, DPP ametoa sababu 11 za kukata rufaa.
  Kwa mujibu wa rufaa hiyo, sababu ya kwanza, DPP anadai kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Salum Massati aliyewaachilia huru Zombe na wenzake, alikosea kisheria na alijichanganya katika kuumba na kutafsiri misingi ya shitaka la mauaji lililokuwa likiwakabili washitakiwa.
  Sababu ya pili, anadai kuwa, kwa mujibu wa mazingira ya kesi hiyo, Jaji Massati alichanganya katika kutafsiri misingi ya dhamira ya pamoja kwa washitakiwa kutenda kosa hilo na kwamba anadaiwa kukosea kutoa tafsiri ya ungamo.
  Mrufani anadai kuwa Jaji Massati, alikosea kumwachia huru mshitakiwa wa kwanza, Zombe, kwa sababu kulikuwa na ushahidi wa mazingira unaombana.
  Pia alikosoa kumwachilia huru mshitakiwa wa pili, Mrakibu wa Polisi, Christopher Bageni, kwa sababu upande wa mashitaka uliwasilisha ushahidi uliomgusa katika kutenda kosa hilo.
  Aidha, alishindwa kutoa sababu za muda wa kisheria za kutomtia hatiani mshitakiwa wa tatu, ASP- Ahmed Makelle, kwa kosa la mauaji.
  "Jaji pia alikosea kumwachilia huru mshitakiwa wa nne (Jane Andrew) na saba (Koplo Abineth Sarro) kwa sababu wao ni waathirika wa kimazingira bila kufafanua na kuonyesha mazingira hayo ni yapi.
  "Sababu ya nane, Jaji alikosea kumwachilia huru mshitakiwa wa tano, Koplo Emmanuel Mabula na wa sita, Michael Shonza, kwa kuukubali ushahidi wao usioaminika uliotolewa na washitakiwa wakati wakijitetea," inaeleza sehemu ya rufaa hiyo.
  Mrufani alidai sababu ya tisa ni kwamba, Jaji Massati alikosea kumwachilia huru mshitakiwa wa nane, Koplo Rajabu Bakari, kwa sababu kulikuwa na ushahidi mzito dhidi yake.
  Sababu ya 10 iliyotolewa na mrufani ni kwamba, katika mazingira ya kesi hiyo, jaji alishindwa kumtia hatiani mshitakiwa wa kwanza (Zombe) na wa tisa (Koplo Festus Gwabisabi), kwa mujibu wa kifungu cha 300 (2) cha Sheria ya Makosa ya Jinai kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002; ambacho kinasema mshitakiwa anaweza kutiwa hatiani kwa kosa dogo.
  Alidai sababu ya 11 anadai kuwa jaji huyo alikosea kisheria kuchambua ushahidi katika kumbukumbu na kusababisha kupoteza mwelekeo wa kesi na kujichanganya alipotoa hukumu hiyo.
  Rufaa hiyo ya DPP imekuja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwaachilia huru washitakiwa hao Agosti 17, mwaka huu, pale Jaji Massati aliposema amebaini kuwa washitakiwa hao sio waliowaua marehemu na akaliagiza Jeshi la Polisi kuwatafuta waliofanya mauaji hayo. Jana, gazeti hili lilichapisha habari kubwa ambayo ilikuwa ikimnukuu Zombe ambaye alisema atishiki na rufaa itakayokatwa dhidi yake.

  Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=9243
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hakuna kitu hapo wanatapatapa tu
   
 3. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hata hivyo mahakama ilikubali pasipo shaka yeyote kwamba: -
  (1) watu waliouawa hawakuwa majambazi
  (2) waliuawa msituni (pande) siyo Sinza makaburini
  (3) walikamatwa Sinza na hapakuwepo purukushani wala kurushwa risasi
  (4) polisi hawakuwaachia au kukabidhi au kuwapeleka kituoni baada ya kuwakamata
  (5) wote waliuawa kwa kupigwa risasi sehemu inayolingana nyuma (kisigoni)
  (6) maiti zao zilipelekwa mhimbili

  Sasa iweje hapa asipatikane muuaji? Wananchi tutaielewa vipi Serikali ktk mazingira haya? Nani alipeleka maiti mhimbili mbona huyu hatajwi?
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Oct 8, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wauaji ni Polisi ambao hawakufikishwa mahakamani kwa kuwa walitoroka. Polisi hao kulingana na nakala ya hukumu ni Saad na James, ndio hasa walioshika mtutu wa bunduki na kuwafyatulia marehemu risasi na kuwaua! Rashid Lema (mshtakiwa aliyefariki) ndiye aliyepakia miili katika gari kuelekea Muhimbili. Jaji Salum Masati alidai kwamba haiwezekani kumtia hatiani aliyesaidia kutenda kosa (assesory before the fact) wakati mtenda kosa mwenyewe (principal offender) hajatiwa hatiani. Hapa mzee ni habari ya technical know how! Kesi ni ya mauaji na si ya kupakia maiti au kushuhudia watu wakiuawa au kufika eneo la tukio la mauaji! Upande wa mashtaka ulifurukuta kweli kuhusu kipengele hiki, but in vain!
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hata mimi mzee nimekosa imani kuhusu kesi hii! Sioni kama kutakuwa na conviction at the end of the day! Anyway let's wait and see! Time will tell!
   
Loading...