yusuphfrancis
JF-Expert Member
- Oct 26, 2016
- 433
- 361
Wakuu poleni na majukumu, Mimi ni mmoja wa wafuatiliaji wa kesi ya akina Abdalah Zombe na mwenzake Christopher Bageni waliotenda kosa la kuwa ua wafanyabiashara wa Madini ya rubbi katika msitu wa pande mnamo tarehe 14 January 2006.katika kesi hiyo mwaka 2009 watuhumiwa wote katika kesi hiyo walishinda kesi na kuachiliwa huru lakini mkurugenzi wa mashtaka DPP hakuridhishwa na hukumu hiyo na alikata rufaa dhidi yao mwaka huohuo na mwishoni mwa mwaka jana 16 September 2016 Christopher Bageni alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na wenzake akiwemo Zombe hawakuonekana kuwa na hatia katika kesi hiyo na hivyo kuachiwa huru. Katika kipindi hicho baada ya hukumu , wakili wa Christopher Bageni alikata rufaa kupinga hukumu hiyo ya kunyongwa hadi kufa mteja wake kwa kuiomba mahakama irejee upya kesi hiyo kwa madai kuwa mteja wake hakupewa haki sawa ya kujieleza katika kujibu rufaa hiyo. Sasa basi anayefahamu maendeleo ya kesi hiyo kuhusu kupinga hukumu ya kunyongwa kwa Christopher naomba anijuze maana kimya sana toka maombi ya kurejewa kwa kesi hiyo yaletwe mahakamani na wakili wa Christopher Bageni. Karibuni mnaofuatilia hii kesi.......