Rufaa kumpinga Mnyika kusikilizwa Disemba 7

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,629
Reaction score
6,816
RUFAA ya kupinga matokeo ya ubunge katika Jimbo la Ubungo iliyokatwa na aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hawa Ng’humbi dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo John Mnyika itaanza kusikilizwa Desemba 7 mwaka huu katika Mahakama ya Rufaa.

Rufaa hiyo inatarajia kusikilizwa mbele ya jopo la Jaji Salum Massati, Jaji Nathalia Kimaro na Jaji Catherini Oriyo. Ng’humbi alifungua kesi akipinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka juzi yaliyompa ushindi Mnyika kwa madai kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu, kanuni na sheria za uchaguzi katika uchaguzi huo.

Hata hivyo Mei 24, mwaka huu, Jaji Upendo Msuya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam alitupilia mbali maombi ya Ngh’umbi na kuthibitisha Mnyika kuwa Mbunge halali wa Jimbo la Ubungo.

Katika kesi hiyo, Ng’humbi aliiomba Mahakama ibatilishe matokeo hayo kwa kuwa uchaguzi haukuwa wa haki, alikuwa na hoja tano ambazo Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za Umoja wa Wanawake (UWT) na kutumia Laptop za Mnyika kuhesabu kura.

Aidha kuingia watu wengi wa Chadema katika chumba cha kuhesabia kura, kuwepo kwa kwa kura hewa 16,000, kukosewa kwa karatasi za kujumlisha kura (form). Katika hukumu hiyo Jaji Msuya alisema Ng’humbi alishindwa kuthibitisha madai yake na kuonesha jinsi yalivyoathiri matokeo ya uchaguzi huo na kutangaza kuwa uchaguzi huo ulikuwa halali.

Alisema maombi kuwa Mahakama hiyo ibatilishe matokeo yaliyompa ushindi Mnyika yametupwa kwa kuwa hakuthibitisha madai yake na kutakiwa kulipa gharama za kesi hiyo pia mashahidi wa mdai hawakuonesha wala kuthibitisha madai yaliyowasilishwa yalitendeka vipi na ni namna gani yaliathiri matokeo ya uchaguzi.

Katika madai kuwa zaidi ya kura 14,000 alizodai hazieleweki zilitoka wapi Jaji alisema alihesabu kura hizo walizopata wagombea wa vyama 16 na kubaini ni kosa tu la kibinadamu na halina uhusiano wowote na Mnyika.

Aliongeza kuwa Fomu namba 24 b ilikuwa na dosari na ndiyo ilikuwa inabishaniwa na Ng’humbi ilikosewa kuandikwa. Kura halali Mnyika aliyetangazwa kuwa ni mshindi alipata kura 66,742 wakati Ng’humbi kura 50,544.

Wagombea wote kura ni 132496. Alisema kuwa katika ushahidi wa mdai hakuonesha ni vipi ongezeko hilo la kura liliathiri matokeo ya uchaguzi na pia mdaiwa Mnyika anahusika vipi na ongezeko hilo.

Chanzo: HabariLeo - Dec 01, 2012
 
Hiv Rwakatare upo wapi na wale blue guards wa CHADEMA ili muwahadhibu watu kama hawa wanaofungua kesi za kitoto.
 
Emu tujikumbushe mtiririko wa kesi yenyewe:-


TUMBIRI (PhD In Progree at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd [/SUP]Best Student in Form Six National Exams),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Rufaa ya Hawa Ng'umbi dhidi ya Mnyika ni kesho kutwa Disemba 7, kwa namna ambavyo Mnyika aliingia na laptop zake na kundi kubwa la watu na kulazimisha tume imeongezee kura hewa zaidi ya 14,000 hatma ya ubunge wake iko mikononi mwa jopo la majaji watatu.

....ndiyohiyo
 
Mbona unaweweseka wewe mbulula? mara unasema Ubunge wa Mnyika kukoma December 7 mara uko mikononi mwa majaji, hivi una uewelewa hata finyu wa kujuwa namna rufaa zinavyosikilizwa na kupangiwa tarehe za kusomewa Hukumu? Kilaza 100% wewe.
 

hizi gharama za kufungua kesi mnazoshindwa kwa aibu pesa huwa mnatoa wapi??
 
Nauliza sheria inasemaje kama mrufani ( hawa) hayupo dunian kesi sindio mwisho wake au ? ( kwan hawa si marehemu?????)

V
SENGEREMA
 
Hivi wana JF hebu tusaidieni hizi pesa za RUFAA za kesi za uchwara kama hizi huwa zinagharamiwa na vyama husika au ni nani? Kwa mantiki hii hizi kesi za SSM hebu sasa muamue kutumia hizi pesa za walipa kodi kwa manufaa ya watanzania. Uchafu mtupu.
 
Kwa taarifa za uhakika nilizonazo Hawa Ngumbi ameamua kuondoa rufaa yake Mahakama ya Rufaa,hivyo kusikilizwa kwa rufaa hakupo tena na bwana mdogo Mnyika anapeta mpaka 2015.
 
yule mama anapenda kusuguana mabega na dogo mnyika kwenye benchi la mahakama...hii kesi hata ukimpa nchemba aliyekunywa maji ya bendera la kijani na njano na mwenye upeo mdogo anampa ushindi kamanda mnyika!!!kwa sababu kubaka mahkama ni kawaida yenu mnaweza kumrudishia ubunge lema na kutengua kijambazi wa mnyika ili muharibu balance ya hoja nzito bungeni...sh..wa.ini
 
Rufaa ya hawa ng'umbi zidi ya john mnyika inaaza kusikilizwa kesho mahakama ya rufaa posta wanachadema wananchi na wapenda mabadiriko wote tufutilie kwa karibu rufaa hiyo.
 
Mnyika hana chake hapo kudadadeki.
watoto wa chichidodo(mang'ula)utawatambua tu(hoja mpauko kinoma)..................kamanda tupo pamoja.....mwache hawa aendelee kuhangaika.....hivi anadai nini hasa,viongozi wengine bana utumbo mtupu..............waiting for 2015
 
Hawa Ngumbi si marehemu huyu jamani? au? kwa sheria inasemaje hapo kama mrufani ni marehemu msaada kwa hiliiii pls?

V
SENGEREMA
 
Hawa Ngumbi si marehemu huyu jamani? au? kwa sheria inasemaje hapo kama mrufani ni marehemu msaada kwa hiliiii pls?

V
SENGEREMA
Mkuu umechanganya. Marehemu ni Hawa Ngulume na si Hawa Ng'humbi. Kuwa makini siku nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…