Rufaa dhidi ya Oscar Pistorius

Rufaa dhidi ya Oscar Pistorius

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
Mahakama Afrika Kusini inatarajiwa kuamua ikiwa viongozi wa Mashtaka wanaweza kukata rufaa kwa kifungo cha miaka 5 alichopewa Oscar Pistorius kwa kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeeva Steenkamp leo hii.


Oscar Pistorius alipewa hukumu hiyo mwezi Oktoba baada ya kupatikana na kosa hilo la mauaji bila kukusudia.

attachment.php



Viongozi wa Mashtaka walionesha kutoridishwa kwao na hukumu aliyopewa Pistorius na kusema watakata rufaa ili mwanaridha huyo Mlemavu apewe kifungo kikali zaidi.

Mbali na kifungo hicho cha miaka mitano, viongozi hao wa Mashtaka wanataka kukata rufaa pia kupinga kwa kosa la mauji bila kukusudia na kumshtaki kwa kosa la kuua kwa kukusudia.

Viongozi wa Mashtaka wakiongozwa na Gerrie Nel wanataka Pistorius apewe kifungo cha miaka 15 kwa kuua kwa kukusudia.


Jaji Thokozile Masipe aliyetoa hukumu dhidi ya Pistorius ndiye atakayetoa hukumu leo Jumatano ikiwa viongozi wa Mashtaka wakate rufaa au la.

Viongozi wa Mashtaka wanasema, Jaji Masipa alitafsiri visivyo sheria kuhusu mauaji na kesi hiyo inastahili kuendelea katika Mahakama ya rufaa.

Hadi uamuzi huo utakapotolewa, Pistorius anaendelea kukitumia kifingo cha miaka mitano jela katika jela ya KGOSI Mampuru.
 

Attachments

  • Pist.jpg
    Pist.jpg
    30.5 KB · Views: 155
Mahakama hiyo hiyo imemruhusu kiongozi wa mashitaka kukata rufaa dhidi ya kosa alilopatikana nalo hatia Oscar Pistorius la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Imeelezwa kuwa kesi hiyo, sasa itaanza kusikilizwa katika mahakama ya juu zaidi upande wa mashitaka ukitaka Pistorius ahukumiwe kwa kumuua mpenzi wake kwa kusudi.

Jaji Thokozile Masipa, alisema hataruhusu rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa ya miaka mitano dhidi ya Oscar mwezi Oktoba.

Kiongozi wa mashitaka Gerrie Nel aliiambia mahakama kuwa hukumu hio ni ndogo sana ikilinganishwa na kosa la Oscar.
 
Back
Top Bottom