7seven
JF-Expert Member
- Mar 27, 2022
- 3,652
- 7,574
Ushangae bado tunahangaika kwenda nje kuomba msaada.Kama hilo jiwe ni bilioni 240 za kitanzania yapo mawe mangapi huwa yanatoka kwa njia kama hizi?Madini yaliyopo kwenye wilaya moja tu TANZANIA yanatosha kulipa deni la taifa na kumaliza shida za watz
Bado siamini kama lilitoka pasipo wahusika kujua hapa kuna inside job imehusika.
Madini mengi adhimu yote yapo Tanzania lakini hayaonekani kuleta tija kwenye bajeti yetu. Wabunge wanalia na bajeti barabara za majimbo yao hazipitiki wanahaha kutafuta fedha, wanalia kama sisi wananchi.
Kwanini wasiibane Serikali kwa kupitia mikataba ya madini, gesi, mafuta na utalii kuongeza mapato.? Kama wakiweza kuibana serikali vizuri hawatauumiza vichwa kuhusu utekelezaji wa ahadi katika majimbo yao.
Wengi hupigwa chini kwenye uchaguzi sababu ahadi zao huwa hazitekelezeki. Wananchi hawajui kwamba walikosa pesa ndio maana hawakutimiza ahadi zao sana sana wanawaona waongo tu.
Serikali na watendaji wana wajibu wa kufanya kuhusu rasilimali zetu. Kwamba tumegundua hiki na kile pasipo kuweka mpango madhubuti kudhibiti ubadhirifu wa hizi rasilimali tutishia kulia n kulalamika kila siku.