Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,329
- 33,139
Taarifa zilisema kuwa rubani huyo aliwahi kuwa na leseni ya kuendesha ndege ndogo ambayo pia ilikuwa imeisha muda wake na alikuwa haruhusiwi kuendesha ndege kubwa.
Tunafikiri sawasawa, maana kama angekuwa hajawahi kwenda darasa la urubani kabisa , ningeconclude kwamba he is GENIUS, naningeshauri wamwache, huyu kafanya kosa lakuto update leseni zake ila anaelimu ya urubani, tofauti na wataalamu feki wa huko bongo, maana unakuta mtu anaigiza daktari kumbe ni kuhiyo kabisa.Kama alishawahi kuwa na leseni basi haina ishu, nilidhani hajawahi hata kwenda shule ya urubani.
Sasa hawa watu nawashangaa sana. Kwani amewezaje kuendesha ndege hizo kubwa kwa miaka 13 bila madhara kutokea kama hafai? Hapa naona wanatetea kitu kilichojificha. Si wampe mtihani ili waverify cheti chake? Kama utoaji wa vyeti ni mgumu, kwa nini asitumie njia mbadala kuvipata ikiwa short cuts zipo na anaweza kuperform kuliko wenye vyeti "halali"?
Nilidhani usalama kwanza, kumbe vyeti kwanza? Ona sasa ati cheti cha ndege ndogo kimeisha muda wake, sasa ukiwa na cheti cha darasa la saba utaendelea kukitumia hata baada ya kupata cheti cha chuo kikuu?
Mizengwe katika control husababisha short cuts kibao. Ningewapongeza kama wangejali hasara aliyoileta katika miaka 13 kwa kuwa na cheti alicho nacho. Degree isiyo na reflection kwenye utendaji inafaa nini? Engeneer wa veta anaweza kuwa na tija zaidi kuliko Engeneer mwenye PhD, ndivyo ninavyoamini mimi. profesa wa Medicini anaweza kuua mgonjwa ambaye angeweza kuokolewa na Auxilliary. Sihamasishi vyeti feki, lakini huyo mtu amethibitisha kuwa anao uwezo ila systems zilitaka kumnyang'anya nafasi ya kuonyesha upevu wake. Sasa wanatafuta kazi hiyo wenye makaratasi "halali" wameamua kumtafutia skendo bwana huyu ili atoke wachukue wenyewe. Sio Bongo tu kumbe mambo haya kutokea.
Tunafikiri sawasawa, maana kama angekuwa hajawahi kwenda darasa la urubani kabisa , ningeconclude kwamba he is GENIUS, naningeshauri wamwache, huyu kafanya kosa lakuto update leseni zake ila anaelimu ya urubani, tofauti na wataalamu feki wa huko bongo, maana unakuta mtu anaigiza daktari kumbe ni kuhiyo kabisa.
Iam positively puzzled!
Miaka 13 ya kuendesha ndege, vyeti feki, bila ajali hata moja!
Huyu ni pilot makini sana, na ni hazina/lulu katika industry hii!
Huyu avalidate vyeti vyake tu, na aendelee na kazi yake!
Nina uhakika katika miaka yote hiyo amekutana na situations nyiingi sana angani ambazo zinahitaji critical decision making, na amefanya bila kuleta ajali!
Practically, this guy is a genius, let him just do the paperwork and go back enroute!
Hold on, but we are not informed kama hakuwahi kupata ajali! Au na wewe umeingia mkumbo wa kufikiri kama angekuwa amepata ajali asingekuwepo!!! Remember kwenye ajali siyo lazima watu wapoteze maisha... Mifano iko mingi tu e.g. ile ajali ya ndege ya Mwanza hivi majuzi!Iam positively puzzled!
Miaka 13 ya kuendesha ndege, vyeti feki, bila ajali hata moja!
Huyu ni pilot makini sana, na ni hazina/lulu katika industry hii!
Huyu avalidate vyeti vyake tu, na aendelee na kazi yake!
Nina uhakika katika miaka yote hiyo amekutana na situations nyiingi sana angani ambazo zinahitaji critical decision making, na amefanya bila kuleta ajali!
Practically, this guy is a genius, let him just do the paperwork and go back enroute!
Wakati anakamatwa rubani feki alikuwa akiendesha ndege kama hii ya shirika la ndege la Corendon Airlines
March 05, 2010
Maafisa wa Uholanzi wamemkamata rubani feki raia wa Sweden ambaye kwa kutumia vyeti feki vya urubani amekuwa akiendesha ndege za abiria kwa miaka 13 bila kugundulika. Rubani huyo mwenye umri wa miaka 41 alitiwa mbaroni kwenye uwanja wa ndege wa Schiphol mjini Amsterdam akijiandaa kuirusha ndege ya abiria 101 toka Uholanzi kuelekea Uturuki.
Rubani huyo mwenye makazi yake mjini Milan nchini Italia kwa miaka 13 alitumia vyeti feki na kufanikiwa kuendesha ndege za abiria za mashirika ya ndege ya Uingereza, Italia na Ubelgiji.
Kufuatia taarifa waliyotonywa na maafisa wa Sweden, maafisa wa Uholanzi walimnyanyua rubani huyo toka kwenye kiti cha rubani wakati akijiandaa kuanza safari ya kuelekea Uturuki akiwa na abiria 101 kwenye ndege aina ya Boeing 737.
Taarifa zilisema kuwa rubani huyo aliwahi kuwa na leseni ya kuendesha ndege ndogo ambayo pia ilikuwa imeisha muda wake na alikuwa haruhusiwi kuendesha ndege kubwa.
Wakati anakamatwa rubani huyo ambaye jina lake liliwekwa kapuni alikuwa akiendesha ndege ya shirika la Uturuki la Corendon Airlines.
Rubani huyo amewekwa mahabusu mjini Amsterdam akisubiria kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kufoji vyeti na kuendesha ndege bila leseni.