RPC Tanga: Vigodoro marufuku

RPC Tanga: Vigodoro marufuku

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
TANGA.jpg

​
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benedict Michael Wakulyamba, amepiga marufuku Vigodoro ndani ya jiji hilo kutokana na vitendo hivyo kuhamasisha uhalifu

Akiongea ofisini kwake Benedict amesema miongoni mwa viashiria vya uvunjivu wa amani ni Vigodoro, ambavyo vinatumika kukusanya vijana wenye umri mdogo wakijiandaa kufanya uhalifu.

“Miziki ya kigodoro ni miziki ambayo ukiangalia namna inavyochezwa na hata washiriki wake ni vijana ambao wanatumia kama sehemu ya maficho kwaajili ya kufanya uhalifu’’ amesema Benedict.

Hata hivyo Kamanda Benedict ameongeza kuwa hakutakuwa na ruhusa yoyote ya kufanya Vigodoro katika eneo lolote na wananchi wanatakiwa kulinda utamaduni kwa njia nzuri na sio miziki inayovunja maadili.

Chanzo: Dar24
 
Safi sana kamanda.
Tena mwenye nyumba afungwe kabisa iwe fundisho.

Wafurahi kwa njia zingine lakini sio kwa uchafu huo
 
“Miziki ya kigodoro ni miziki ambayo ukiangalia namna inavyochezwa na hata washiriki wake ni vijana ambao wanatumia kama sehemu ya maficho kwaajili ya kufanya uhalifu’’ amesema Benedict.

Hata hivyo Kamanda Benedict ameongeza kuwa hakutakuwa na ruhusa yoyote ya kufanya Vigodoro katika eneo lolote na wananchi wanatakiwa kulinda utamaduni kwa njia nzuri na sio miziki inayovunja maadili.

Mkuu;
Mbona hivi ni vitu viwili tofauti anazungumzia?? Aseme kilichomkera ni nini sio kutafuta vijisababu. Kweli huu sio utamaduni wetu kama alivyofanya mtoto wa kigogo mmoja kuchujua nguo na kubaki wazi (utupu). Wanaoangalia ni vitoto vidogo hivyo hiyo mbona ni laana? Asiseme ati ni maficho ya wahalifu, wanajificha chini ya hivi vigodoro au??
 
Nadhani RPC amekosea... Vigodoro huchezwa ndani ya club au nyumba kubwa za ukumbi au nyumba za watu wakati wa sherehe au kuburudika, mm sioni tatizo hata kidogo, waacheni watu waburudike jamani, kama kuna mtu atafanya uhalifu ndio ashughulikiwe.. Ila vigodoro ni utamaduni wa watu kama vile ngoma zilivyo au Dar kuna singeli.. Hizi ni burudani za watu, ni busara kuwaacha waburudike ila wahalifu washughulikieni..
 
Nchi hii hakuna vyombo vya Usalama kuna vyombo vya kupikia tu.
 
Nadhani RPC amekosea... Vigodoro huchezwa ndani ya club au nyumba kubwa za ukumbi au nyumba za watu wakati wa sherehe au kuburudika, mm sioni tatizo hata kidogo, waacheni watu waburudike jamani, kama kuna mtu atafanya uhalifu ndio ashughulikiwe.. Ila vigodoro ni utamaduni wa watu kama vile ngoma zilivyo au Dar kuna singeli.. Hizi ni burudani za watu, ni busara kuwaacha waburudike ila wahalifu washughulikieni..
Nadhani unazungumzia vigodoro vilivyo boreshwa ambavyo tunaona matangazo eg "Usiku wa bunyero ndani ya Club X" nk..tafsiri anayo zungumzia RPC ni zile party zisizo rasmi zinazo kesha uswahili..shughuli kama 40 ya mtoto nk! Huenda RPC akawa sahihi kwa kiwango kikubwa tu!

Ni aibu mitaani huko!
 
Kama mtoa ripoti hajakurupuka basi Rpc anatakiwa aje na convincing statement vigodoro vinaletaje uhalifu,na vijana wanajifichaje humo tofauti na hapo ntamwona kaingilia kazi ya afsa tamaduni wa mkoa
 
Back
Top Bottom