RPC simiyu kuwa makini

Supu ya kokoto

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
3,711
6,765
Katika mkoa wa simiyu Kuna tabia ya polisi kuwakamata BODABODA na kuomba rushwa ili wawaachie. Sababu za ukamataji huo zimejificha kwenye makosa makuu mawili.
1. Leseni
2. Bima
Pamoja na kuwa BODABODA hao wengi wao hawana vitu hivyo vya muhimu kisheria lakini pia jeshi la polisi haliwasaidii vijana hao kwa kuwapa elimu juu ya umuhimu wa leseni pamoja na bima.
Badala yake wamegeuza makosa hayo kuwa posho zao za kila siku kwa kujikusanyia pesa kutoka kwa maskini hao walioamua kujiajiri.

Maeneo yenye kero kubwa na usumbufu huo ni pamoja na:
1. Maswa mjini
2. Ligangabilili
3. Mwandoya
4. Lalago
5. Bariadi mjini

RPC wa mkoa wa Simiyu tunakuomba Jambo hili ulisimamie hata kwa kuwasaidia vijana Hawa ambao ni sehemu ya amani mkoani simiyu kupewa mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao pamoja na kupewa semina za usalama barabarani.
Natumai sauti hii itafika mbali.
Mungu ibariki tanzania
 
Kichwa cha habari ni Biti kwa RPC.ila kwenye maelezo kuna Maombi kwa RPC

SUBIRI KIDOGO
 
Wanakera sana hawa watu. Ila Basi tuu mie nimechoka nao
 
Back
Top Bottom