Kwa mujibu wa utaratibu wa uongozi wetu, masuala ya ulinzi yanasimamiwa na jeshi la polisi, jeshi la wananchi, magereza na usalama wa Taifa. Mabossi wa taasisi hizo katika mkoa wanaunda Kamati ya Ulinzi na Usalama ambayo Mwenyekiti ni Mkuu wa Mkoa. Hivyo kama suala linatambuka ktk idara hizo RC ndo atakuwa msemaji. Hata hivyo RPC amepewa nafasi kubwa ya kusemea mambo yanayohusu usalama wa rai na mali kuliko RPO, RSO, Makamanda na majeshi kwa kuwa mambo yao ni nyeti zaidi hivyo kama yanatolewa kwa wananchi yatahitaji itafaki zaidi.
Hata hivyo, binafsi huwa sioni umuhimu wa kuwa na RC wakati RAS yupo. Majukumu anayoyafanya RC yanaweza kufanywa na RAS. Hali kadhalika DC, DAS anatosha.