RPC Arusha: Tunamshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vicent, atapelekwa mahakamani

Hakuna kesi hapo ni kupoteza muda tu.....ndio maana serikali iligoma kukagua vyeti kwenye majeshi maana kwa rpc kama huyo sidhani kama angepona.

Muda wanafunzi wanapanda bus mmiliki huyo alikua nyumbani kwake sasa angeota kuwa gari yake muda huo inabeba watu wangapi...!!!!

Rpc nenda kaongeze nguvu kibiti
 
kwani hiyo gari ilivuka vizuizi vingapi vya POLISI kwa ya kupata ajali? hawkuona wingi wa abiria? je, hizo gari nyingine 2 zilikua hazijazidisha abiria?
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles Mkumbo amesema wanamshikilia mmiliki wa basi dogo aina ya Coaster ambayo ilipata ajali na kusababisha vifo kwa wanafunzi, walimu na dereva siku ya Jumamosi huko Karatu, Arusha.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles MkumboRPC Mkumbo amedai wanamshikilia mmiliki wa shule hiyo kwa kuruhusu gari yake hiyo kubeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wa gari "Siku ya tukio walikuwepo abiria 38 kwenye gari katika uchunguzi baada ya kubaini hilo tumeshachukua hatua kwa mtu aliyewezesha gari hilo kupakia hao watu.

Tumeshamkamata mmiliki wa gari ambaye ndiye mwenye shule hii, sasa hivi tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa mahakamani"alisema RPC wa Arusha Kwa mujibu wa Mkumbo anasema gari hiyo ilikuwa na kibali cha kubeba watu 30 lakini gari hiyo siku ya ajali ilikuwa na watu zaidi ya 30.

Chanzo: EATV
Mmmh haisaidiii cha msingi ni kusimamia suala zima la usalama tuu barabaran mana hata huku town macosta siyana beba hata zaid yahao 30 na inaonekana nikawaida tuu sembuse wanafunz ambao ni familia.
Mm nakumbuka shule tushawahi kupanda fuso wanafunz 140 tulikuw tukienda michezon gar lilipata ajali kama mitre 10 kutoka tulipo pandia linaaguka huku walimu wanaliona yan ndio dereva qlikuwa kaliondoa tuu hata assemble halijatoka.
 
Negligence itamfaa basi ama si unajua tena si Ma-bush lawyer (tunababia babia taaluma za watu).
** Kaimu Jaji Mkoou alimuwakilisha nan pale?
Akili zako ziko matak*n* eeeh? Huko ni sehemu ya kutolea uchafu sio kufikiri,tumia kichwa kufikiri,kujiheshimu ili uheshimiwe!
 
Fine yake naweza kuta isizid 5k.
Hamtoamini macho na masikio yenu siku hukumu ikitoka.
Kuna umuhimu na ulazima wa Ku review & upgrade sheria zetu za barabarani
 
Toka hii ajali itokee nimeshangaa sijamuona mmiliki wa shule wala kutajwa ni nani. Hii kwangu ndio habari ya kwanza inamgusia mwenye shule.
Mwenye shule anakosa gani? tatizo sisi wantazania tuna tabia yakua na chuki na mtu anae jitahidi kiuchumi bila sababu za msingi. matharani kuna mkuu wa shule, makamu, mtaaluma Mwl wazamu, driver viraja hao ndowanao ratibu shughuri za kila Siku za shule. Sasa hapo menaje au Mmiliki anaingilia wapi? shule ngekua ya Kanisa au serikali archbishop au Waziri wa elimu ndoangewekwa lockup kweli ? let us be fair to private sector
 
Hivi toka Arusha hadi Karatu njiani hamna askari wa usalama barabarani? Kama wapo hawakukagua hiyo gari ili isiendelee na safari kwa kuzidisha abiria? Kama askari wapo njiani na walikagua kwanini waliruhusu iendelee na safari? Kuna mtu mahala hakutimiza wajibu wake. Ni vema kila mtu atimize wajibu wake ili kuzuia matatizo kama haya yaliyowakuta watoto wetu.
 
Kwa hiyo mmiliki wa hiyo minibus ndo huyo huyo mmiliki wa shule?

Kwa shule nyingi binafsi wamiliki wanajihusisha moja kwa moja na mambo/shughuli za kila siku zinazoendelea hapo shuleni. Inawezekana kabisa ndiye aliyependekeza gari iliyopata ajali ndiyo ibebe watoto siku hiyo. Na katika mazingira ambapo dereva amefariki then ni vema mmliki ahojiwe ili ijulikane utaratibu wa safari hiyo ulikuwaje hasa swala la usafiri. Nadhani na mwl. Mkuu angehojia pia ili "ku-balance" story
 
Movie ndo inaanza mbona kwenye daladala tunabebwa wengi hata kwenye mwendo kasi pia hzo sinema mnaleta
Acha daradara, defender za police zina beba zaidi ya uwezo wakiwa wanaenda lindoni au wakiwa wanatoka kibaya Saudi wakiwa wamesimama au wenyewe sio binaadamu charity begins at home.
 
Mbona Daladala na mabasi ya mwendokasi yanapakia hadi kuzidisha abiria. ao mpaka ajali itokee, ndio sheria ichukuliwe??? mmmh kweli Afrika shida
 
Back
Top Bottom