RPC Arusha: Tunamshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vicent, atapelekwa mahakamani

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,387
24,946
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles Mkumbo amesema wanamshikilia mmiliki wa basi dogo aina ya Coaster ambayo ilipata ajali na kusababisha vifo kwa wanafunzi, walimu na dereva siku ya Jumamosi huko Karatu, Arusha.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles MkumboRPC Mkumbo amedai wanamshikilia mmiliki wa shule hiyo kwa kuruhusu gari yake hiyo kubeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wa gari "Siku ya tukio walikuwepo abiria 38 kwenye gari katika uchunguzi baada ya kubaini hilo tumeshachukua hatua kwa mtu aliyewezesha gari hilo kupakia hao watu.

Tumeshamkamata mmiliki wa gari ambaye ndiye mwenye shule hii, sasa hivi tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa mahakamani"alisema RPC wa Arusha Kwa mujibu wa Mkumbo anasema gari hiyo ilikuwa na kibali cha kubeba watu 30 lakini gari hiyo siku ya ajali ilikuwa na watu zaidi ya 30.

Chanzo: EATV
 
Ni sawa kumkamata na kumshitaki lakini haisaidii kurudisha roho zilizopotea...inahuzunisha aisee
Lengo si kurudisha roho za marehemu bali kuadhibu uzembe ili na wengine wajifunze. Jitu linaanzisha shule kama linaanzisha gesti bubu, linaenda kuokota mibasi mibovu ndo inabebea watoto wetu na wazazi wanaona wanakenua meno tu na vitambi vyao. funga wote wazembe. Kuna ugumu gani wa.kununua mabasi imara?
Kakope benki, nunua basi jipya
 
Haya ndio ambayo wamiliki wa vyombo vya usafirishaji hawayataki. Kosa liwe la dereva halafu akamatwe mmiliki hii imekaaje?

Ila ngoja tusubiri kwanza tuone mwisho wa hii kesi. Ingawa inaumiza sana nyoyo za wazazi wote ila hatupendi zihaka kwenye hili.
 
Mm binafsi cthani kama kumkamata huyo bosi. Ni solution kwani haskari polisi awakwepo barabarani? Na je kukamatwa kwake kutarudisha roho za malaika wale? ishu ni Ku take care yasije kutokea kama Yale Na sio kumchukulia hatua now it's too leit.
 
Back
Top Bottom