Habari zilizoenea kwenye magazeti na mitandao ni kwamba Muimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando safari hii amemtapeliAlex Msama baada ya kupokea fedha kwa makubaliano ya kushiriki Tamasha la Krismasi kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa lakini siku ya tukio, Ijumaa iliyopita, mwanadada huyo hakutokea!
Hii ni mara ya pili, kwenye uzinduzi wa albamu ya msanii John Lisu pale Diamond Jubilee (Dar), Rose alipokea shilingi milioni moja kutoka kwa Msama lakini siku ya uzinduzi hakutokea. Kusema ukweli huu utapeli wa Rose wa kuchukua fedha za watu halafu hatokei sasa imekuwa too much. Nimesikia habari kwamba ameogopa kutokea uwanjani hapa ambako tamasha lilifanyika kwa kuhofia mimba yake kuonekana maana kwa sasa ni kubwa. Kimesema chanzo hicho cha habari
chanzo:Eatv
Kumbe huyo Msama naye hana dogo, milioni moja tu kelele kibao, si azifate akarudishiwe
Polisi case tunaletewa hapa kulishwa ugoro? Nitaamini tu pale nitakaposikia Rose apandishwa kizimbani kwa utapeli.
Yani shigongo ni mjanja sanaaa.. Tena sana. Anapiga pesa mara mbili... On your way up, anapokupandisha kwa story za kukupamba na kukusifia... And on your way down, anapiga pesa kwenye story za kukushushaa..
sijawahi kununua magazeti ya udaku,nadhani yana soko kuliko magazeti ya kawaida
Ashukuru Mungu wenye akili za maiti wanaosoma hizo takataka zake wapo vinginevyo angekufa njaa....
Shigongo anatumia ignorance ya watanzania km fursa ya ajira. Huwa namsikilizaga akisema watanzania ni wavivu kusoma, sasa ndo tusome ule uchafu wa magazeti yake? Na hizi Elimu za kata sijui tunaenda wapi? Me nliwahi kuchukua gazeti la ijumaa, nlifunua km sekunde tano hv, sikuona pakusoma kwakweli. Lakini magazeti yake yanapendwa sana uswahili kwenye watu wengi na wenye elimu ndogo na uwezo mdogo wa kupambanua mambo. Yeye anafanya biashara wala hana nia ya kuelimisha watanzania na km anataka kuwapa watu habari basi atoe habari zinazoweza kuwapa watu uwelewa wa mambo, kupitia vyombo vya habari watu wanaweza hata kupata informal education.
kwel nimeamini watz hatutambui thaman ya vipaji vyetu rose muhando anakodishwa wa 1 mil mbona ndogo kwa kazi yake