Royal Tour: Wacheni Tuseme Ukweli

Acha maneno tulia tuone matokeo kwanza
 
Je ulimuona mtu gani wa kariba ya umaarufu wa kimataifa katika uzinduzi ule?
Sikuangalia uzinduzi,haihitaji mtu maarufu kuja kwenye uzinduzi,nasikia umepata views 3m...hayo ni mafanikio makubwa
 
Very good analysis.
 
Huyo muongozaji ni mshidi wa tuzo za filamu,siyo mtu mdogo kwenye tasnia,huwezi rusha filamu BBC,CNN,Fox news...
Ni kweli mhusika anajulikana kwenye ulingo wa filamu, lakini tujiulize lengo kuu la filamu ni nini? Lengo halikuwakutengeneza pesa kupitia hiyo filamu, bali kutangaza biashara ya utalii Tanzania. Itakuwa ajabu tangazo la biashara kulipiwa kuliona. Naunga mkono kama hii ingewahusiaha National Geographic ingepata coverage kubwa, sasa hivi itaoozea Amazon. Juu ya yote filamu iliyotengenezwa na pesa ya mlipa kodi inatumika kumtajrisha SSH, Greenberg, na Amazon.
 
Nadhani ungekuja na argument ya kuikataa The Royal Tour concept ingekua na maana zaidi kuliko kukataa ushiriki wa Mh. Rais. Soma kidogo kuhusu Royal Tour concept before ya kucriticise. Mhusika mkuu katika Royal Tour ni kiongozi wa nchi angalia hii Screenshot toka website yao



Tukiongelea kuhusu Rwanda wanavyojutangaza ile kutumia Arsenal na PSG ni different approach katika kujitangaza ila katika The Royal Tour Kagame alikua front kama ilivyo kwa Samia. Angalia hiyo link hapo chini

 
Sasa kama mleta mada ameweza kujua haya yote Raisi na taasisi zake wameshindwaje kujua?

Kusema at least Mama kajaribu haitoshi,Hili ni suala la kitaifa linapofanyika lifanyike kwa ukamilifu kwa sababu linabeba taifa na tuna taasisi nyingi ambazo zingeweza kufanya utafiti na kumshauri zaidi hata ya aliyosema mleta mada.

Nachokiona hapa ni watu wachache kujifanya wajuaji ndio maana kila mara nchi inapigwa na wajanja tu
 
Wavimba macho kujitia ujuaji hata kwenye fani wasio na utaalamu nayo.
Mleta mada aweke qualifications zake kwenye film industry. Na madai mengi kuhusu wakuu wa Nchi kama ndio kwanza imefanyika Tanzania.
 
Si umeona tayari Rostam Aziz ameibukia huko akisaini mikataba yake ya Dola milioni 500!
 
Wavimba macho kujitia ujuaji hata kwenye fani wasio na utaalamu nayo.
Mleta mada aweke qualifications zake kwenye film industry. Na madai mengi kuhusu wakuu wa Nchi kama ndio kwanza imefanyika Tanzania.
Je filamu hii imelenga wakuu wa nchi au wananchi wa kawaida wa nchi zao?

Je hao wakuu wa nchi huwa wanao mvuto wowote kwenye ushawishi wa masoko ya kibiashara Duniani?

Je hao wakuu wa nchi huwa wanapita bila kupingwa baada ya kurekodi filamu na Peter Greenbag?

Ebu niambie kwenye uzinduzi huo ni watu maarufu wangapi uliowaona wakijumuika na Greenbag kuja kuizindua hiyo filamu?

Halafu njoo ujibu na maswali mengine ya Gharama zake na umiliki pamoja na utitiri wa msafara na gharama za kukaa huko.
Huku mitaani watu wakipambana na mifumko ya bei.

Maswali niliyoyauliza hayahitaji taaluma maana ni ya kawaida kabisa.
 
Inahusika vipi na Royal Tour.Royal Tour ndio mada inayojadiliwa.
Tunaongelea ukubwa wa msafara wa uzinduzi na kilichoko nyuma ya pazia pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…