Roy Hodgson ajihuzulu ukocha Uingereza..

Majighu2015

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,936
3,958
Kocha wa timu ya Uingereza Roy Hodgson amejuzulu kuwa kocha wa Uingereza baada ya timu yake kuenguliwa kwenye mashindano ya Uefa Euro 2016 dhidi ya Iceland.

Je, aistahili kujihuzulu?

Nini maoni yako?
 
35BC344700000578-0-image-m-3_1467060942398.jpg

Kocha wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Uingereza Roy Hodgson ajiuzuru rasmi baada ya mechi kati ya timu anayoifundisha dhidi ya Iceland kwa kichapo cha goli 2-1 na kutolewa kwenye hatua ya mtoano ya michuano ya Ulaya.

Uingereza wakiwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 4 lililo fungwa na mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Wayne Roone kwa njia ya penati iliyo sababishwa na mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling kukwatuliwa kwenye eneo la hatari na golikipa Hannes Thor Halldorsson wa timu ya taifa ya Iceland.
rooney-penalty-iceland.ashx

Hata hivyo goli hilo haliku dumu maana dakika ya 6 tu mchambuliaji wa timu ya taifa ya Iceland, Ragnar Sigurdsson alitia nyavuni goli la kusawazisha na kuwapa nguvu kipindi cha kwanza chote cha mchezo na baada ya dakika chache mshambuliaji mwingine Kolbeinn Sigthorsson alitia nyavuni dakika ya 18 goli la pili lililo dumu hadi mwisho wa mchezo.
maxresdefault.jpg

Huku kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya mchezo huo kocha wa Uingereza akitamka kwa majonzi kuachia ngazi kufundisha timu hiyo.
 
Kocha msaidizi wa England Gary Neville naye pia amejiuzulu nafasi hiyo baada ya kuondoshwa na Iceland EURO2016
 
Kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hogdson ametangaza kujiuzulu kuifundisha timu ya taifa England, kutokana na kupoteza mchezo wao wa 16 bora dhidi ya Iceland taifa lenye wakazi wasiozidi 330,000 huku ikiwa nafasi ya 34 kwenye viwango vya FIFA, kwa kufungwa goli 2-1, England walianza kupata goli la uongozi dakika ya 4 kwa mkwaju wa Penati kupitia kwa Wayne Rooney.

35BC53AE00000578-3662916-image-a-41_1467063156986.jpg

Dakika mbili baadae baada ya England kupata goli la uongozi, Iceland walisawazisha kupitia kwa Ragnar Sigurdsson dakika ya 6 na Kolbeinn Sigposson dakika ya 18.

Roy Hodgson ametangaza uamuzi huo wa kujiuzulu kuendelea kuifundisha England, ikiwa ni siku tatu zimebakia mkataba wake umalizike
 
England has never been among the big boys in soccer apart from 1966 where soccer was not at full blown size, sielewi ni kwa nini wanajilazimisha waonekane kama ni taifa kubwa, binafsi niliitabiria kutoka ktk makundi.
 
Huyu na Dunga hawana tofauti,ujuaji na uvichwa vigumu mwingi sana.
 
England has never been among the big boys in soccer apart from 1966 where soccer was not at full blown size, sielewi ni kwa nini wanajilazimisha waonekane kama ni taifa kubwa, binafsi niliitabiria kutoka ktk makundi.
Hawa jamaa kwenye kufuzu walikomaa,friend match walishinda nyingi. Sielewi kwa nn wamevurunda kiasi hili.
 
Huyu mzee anastahili kushitakiwa .
Hahaaaa kwa nn ashtakiwe?? Walitaka kocha muingereza ndo huyo kawafikisha hapo walipo. Jana Kevin Kegan alikiri hamna kocha mwingereza anaweza kuinoa timu hiyo na sababu kubwa ni kwamba karibu club kubwa zote UK hamna mwingereza anyezionoa.
 
Wakati naanza kupenda soka nilikuwa naweka ushabiki kwa England kwamba haichukui kombe basi ushabiki ukaendelea nikijua nayo ni timu bora kumbe ni kinda tu la robo final basi mwaka huu hata sikuwaangalia kabisa(France au German )ndio timu zangu kwa sasa.
 
Hahaaaa kwa nn ashtakiwe?? Walitaka kocha muingereza ndo huyo kawafikisha hapo walipo. Jana Kevin Kegan alikiri hamna kocha mwingereza anaweza kuinoa timu hiyo na sababu kubwa ni kwamba karibu club kubwa zote UK hamna mwingereza anyezionoa.
Amelitia hasara taifa lake , utamuachaje Vardy nje ?
 
Back
Top Bottom