Rough minded

Jozee mkunaji

JF-Expert Member
Jun 11, 2017
457
1,000
Just thinking with my rough mind and realized this..

Mahusiano yetu vijana siku hizi ni ya ajabu sana, leo tuko pamoja baada ya mwezi tumebwagana,, tatizo ni kwamba hisia zetu zinafanya tunakurupuka, ni kweli huwezi kuuzuia moyo kumpenda mtu lakini ili kudumisha mahusiano yetu lazima kuifunza mioyo kuwa na subira ili kujua japo mambo machache zaidi kuhusu unayehisi unahitaji kuwa na mahusiano nae..
mapenzi ni kama swimming pool unapoingia usiulize nani alietangulia kuoga

pamoja na hayo jaribu basi kuchunguza huyo aliyeoga aliacha nini ndani ya hayo maji au alipotoka alitoka na nini..yawezekana alioga akatoka salama lakini akamwaga sumu ndani ya maji au yawezekana maji yalikuwa na sumu ndio sababu akatoka..

Nini maana yangu ?...

kama kijana unapoanzisha mahusiano mdadisi mwenzio ujue ameachiwa madhara gani kichwani na mtu aliyekuwa nae kabla yako, nitatoa mfano kwa jinsi ya 'ke'..kuna mabinti waliofanywa waone kama kila mwanaume ktk dunia hii si mkweli/muaminifu ktk mahusiano..je unatarajia huyo binti atakua mkweli/muaminifu ktk mahusiano mengine ? Si rahisi yeye kuwa muaminifu kwa mwanaume bila ya kumbadilisha anachowaza juu ya wanaume..So ni vzr kujua mapema tatizo lililo kichwani kwa mwenzio na ukiona unaweza kulitatua litatue ndipo uingie kikamilifu ktk mahusiano ukiona huwezi ndugu mbio sio lazima za marathoni hata moyoni kuna mbio kimbia muache kama alivyo

Usianzishe mahusiano eti kisa tu unahisia za upendo o mapenzi ya dhati kwake..kumbuka mahusiano hayajengwi na mapenzi ya dhati tu mahusiano yanajengwa kwa kila mmoja kumuelewa mwenzake vyema na ndio sababu hata waliovunja mahusiano ukiwachunguza utagundua bado wanapendana lakini nguvu ya mapenzi baina yao bado imeshindwa kuwaweka ktk mahusiano

Daaah ndefu hadi inaboa ila isome tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom