Rostam ni Baniani Mbaya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam ni Baniani Mbaya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jul 14, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Wahenga walinena; " Baniani mbaya, kiatu chake dawa!".

  Na kuna kisa nilipata kusimuliwa. Ni kisa cha mwandishi wa habari wa Kitanzania aliyekamatwa na makachero wa Idi Amin mpakani mwa Uganda na Tanzania. Mwandishi yule akafikishwa mpaka kwa Idi Amin mwenyewe. Masikini, alijawa na hofu kuu. Mbele yake aliyaona mauti yake yakimkodolea macho.


  Idi Amin alimwangalia kijana yule mwanahabari Mtanzania. Kisha akatamka; " Nyie waandishi wa Tanzania mnaandika mambo mabaya tu kuhusu Idi Amin. Hivi hakuna hata kitu kimoja muzuri Idi Amin amefanya?"

  Mwandishi yule Mtanzania alijibu mara moja; " Mkuu, umefanya mambo mengi mazuri".

  Idi Amin aliposikia hivyo akatamka; " Basi, nenda nyumbani Tanzania na ukaandike kitu moja tu muzuri kuhusu Idi Amin."
  Mwandishi yule Mtanzania hakuamini alichosikia. Kuwa aliachiwa huru na Idi Amin!


  Soma habari hii hapa chini kuoka Igunga iliyochapwa kwenye gazeti la Mwananchi. Je, ni yale yale ya " Baniani mbaya, au?"


  Igunga yazizima

  Fidelis Butahe, Igunga

  MJI wa Igunga na vitongoji vyake jana ulizizima, Mbunge wa Igunga Rostam Aziz alipotangaza kuachia ubunge wa jimbo hilo.Tukio hilo liliambatana na matukio kadhaa ya wananchi kuonyesha mabango yaliyokuwa na ujumbe tofauti, wengine kuzirai na mara kadhaa kumvamia ili asiendelee na uamuzi wake huo.

  Mbunge huyo aliwasili Igunga saa saba mchana na baada ya kufika akaingia katika ofisi za CCM wilaya na kuzungumza na Baraza la Vijana la Wilaya. Aliwambia vijana hao kwamba, halikuwa lengo lake kuingilia mkutano wao bali alitaka kuzungumza na wazee.

  Wakati akiingia katika mkutano huo, alipokewa na mabango yaliyokuwa na ujumbe uliosomeka kwamba "Kama wakikufukuza na sisi tutaondoka CCM", "Igunga bila Rostam hakuna maendeleo", "Rostam umeboresha huduma za kijamii Igunga", "Mbunge wetu tunakupenda sana" na "Tuna imani na wewe".

  Alitumia dakika saba kuzungumza na vijana kabla ya kukutana na viongozi wa CCM wa wilaya hiyo, akiwamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee, Kassim Ally. Akiwa na viongozi hao alizungumza nao kwa dakika 49.

  Saa nane mchana aliondoka kwenda kwenye Ukumbi wa Sakao uliopo kilomita moja kutoka jengo la CCM wilaya hiyo.

  Akiwa huko alipokewa na kisha kuanza kusoma hotuba yake ndefu ya kurasa takribani 10, lakini mara baada ya kutangaza kuachia nafasi zake ndani ya CCM huku akilengwa na machozi, baadhi ya wanachama walianza kulia huku wengine wakivamia meza kuu kumtaka mbunge huyo abadili uamuzi yake.

  Wananchi hao walikuwa wamebeba mabango yenye maneno " wao CCJ, sisi CCM", huku wakilitaja jina la Nape Nnauye, ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho.

  Kufuatia tukio hilo Rostam alilazimika kuacha kuendelea kuisoma hotuba hiyo kwa dakika 15 baada ya kuvamiwa na kundi la baadhi ya vijana waliomtaka kusitisha uamuzi wake huo na kuwasihi wasimzuie, ili amalizie hotuba hiyo na baadaye watoe maoni yao.

  Baada ya wanachama hao kutulia walipewa nafasi ya kutoa maoni yao wakasema kwamba akiendelea na uamuzi huo watarudisha kadi za CCM.

  "Hatukubali wewe kwetu ni muhimu sana umetufanyia mengi, yanayosemwa yavumulie nakuomba ubadili msimamo wako na kama hautabadili msimamo huo hatuoni haja wa kubakia ndani ya chama cha CCM," alisema Hamis Kanama.

  Watu wazirai

  Baada ya Rostam kumaliza kusoma hotuba, Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nzega, Daudi Ngutu, na Katibu wa Uchumi Kata ya Igoweko, Athuman Kanyama, walizirai na kupandishwa katika gari la Halmashauri ya kupelekwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya.

  Mjumbe wa Barala la Utekelezaji la UVCCM, Hussein Bashe, alikuwa miongoni mwa mashuhuda wa tukio la Rostam kutangaza kung'atuka. Bashe ambaye alikuwa sambamba na Rostam tangu akiwa katika ofisi za wilaya aliliambia Mwananchi kuwa uamuzi wa Rostam ni mwiba mchungu kwa wananchi wa jimo hilo.

  "Alichokifanya Rostam ni haki yake, lakini pamoja na hayo hawatendei haki wananchi wa Igunga, ila kwa kuwa ni maamuzi yake hakuna jinsi,"alisema Bashe na kusisitiza kwamba, CCM isipokuwa makini uchaguzi wa mwaka 2015 ukimalizika, utakiacha kikiwa chama cha upinzani na si chama tawala.

  "Sekretarieti ya CCM itakabidhi chama kikiwa cha upinzani Watanzania wana matatizo mengi , lakini viongozi badala ya kuangalia hayo wanaendekeza siasa za chuki na kinafiki," alisema Bashe.

  Rostam aondolewa na mabaunsa

  Wanachama wa CCM waligoma kumruhusu Rostam kutoka katika ukumbi huo mpaka abadili uamuzi wake hali iliyosababisha vurugu na kufanya Askari wa kutuliza Ghasia(FFU) kuingilia kati.

  Hata hivyo baadhi ya viongozi wa CCM walimtoa Rostam katika ukumbi huo kwa kuwatumia mabaunsa waliokuwa wanawazuia wananchi wasimzuie Rostam kuondoka.

  Wakati Rostam akiwa njiani kuondoka kwenda Dar es Salaam wanachama wengine ambao ni Katibu mwenezi kata ya Chabutwa, Athumani Mihayo, Catherine Mabula na Zainabu Athumani walizirai.

  Viongozi wa CCM waliokuwapo

  Viongozi wa CCM wengi kutoka wilaya zote za mkoa wa Tabora walihudhuria ambao ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Igunga, Katibu Tawala wa Wilaya, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tabora, wajumbe wa kamati ya siasa wa wilaya na Baraza la Wazee la Wilaya na Mbunge wa Viti Maalumu, Munde Tambwe.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Ama kweli, Banianai Mbaya Kiatu chake Dawa!

  Matukio haya ya Igunga yanatuonyesha jinsi vita ya ufisadi ilivyo ngumu. MAFISADI hawa, wana ndugu, wajomba, mashemeji, na hata wapambe wanaofaidika na bakhshishi kutokana na utajiri wao; wote hawa watampigania bwana yao katika kulinda kie kidogo wanachotupiwa.

  Hakika hii ni aina nyingine ya utumwa; na ni hulka ya watanzania wengi, kutaka pata vya bure na kwa njia za mkato. Tunasubiri vituko zaidi pale MAGAMBA wengine maarufu watapojivua.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tukiacha tofauti za Kiitikadi viatu vya Rostam kwa wanaIgunga hakuna anayeviweza! Siwezi shangaa atawaamulia nani awe Mbunge wao
   
 4. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kwa yote hayo aliyowafanyia....... wana haki ya kuzizima!
   
 5. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  bado Lowasa
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  The Dude is filthy rich....
   
 7. k

  kiloni JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wote ni tabia ya umaskini popote. Unakuwa na vibaraka wengi kwa jina la wapambe.
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,264
  Trophy Points: 280
  Kama aliweza kutuamulia Rais awe nani ni kazi rahisi kuamuwa mbunge awe nani ili halina mjadala
   
 9. mulambakao

  mulambakao Member

  #9
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Teh teh teh, Igunga, Rostam , Chama Cha magamba (CCM) Wanaendelea kufaidika sana na hiyo dhana ya utumwa wa kisasa, wanasahau kwamba kuna mambo ambayo yangewakomboa kutoka huo ugumu wao bila kumtukuza huyo dugu, na kukufuru Mungu, hakuna nafasi isiyozibika! Vueni magamba na mhakikishe hayaoti tena, acheni kuendekeza umaskini mambo leo Igunga ninyi!
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Dude I missed you! Salama?
   
 11. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  "Baada ya Rostam kumaliza kusoma hotuba, Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nzega, Daudi Ngutu, na Katibu wa Uchumi Kata ya Igoweko, Athuman Kanyama, walizirai na kupandishwa katika gari la Halmashauri ya kupelekwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya."

  "Wakati Rostam akiwa njiani kuondoka kwenda Dar es Salaam wanachama wengine ambao ni Katibu mwenezi kata ya Chabutwa, Athumani Mihayo, Catherine Mabula na Zainabu Athumani walizirai. "

  Huku ni kuzrai kwa kimaslahi binafsi zaidi ambayo ni sawa na sanaa za jukwaani.
  Muda wa kutengeneza mabango ulitoka wapi kama si walio karibu na Mbunge (aliyeshinikizwa kujiuzuru) kuwa wame-stage drama?

  Kuzirai na vilio vwa ukweli ilikuwa April 12 1984 na October 14 1999
   
 12. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Umaskini tu ndo uliwaliza hao maigunga hamna jipya
   
 13. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wavivu ndivyo walivyo si wamezoea umatonya.
   
 14. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mimi nilijua ni watanzania kumbe ombaomba hao lazima wawake moto
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ukitaka kujua kila shetani na mbuyu wake uwa jambazi halafu hudhuria mazishi uone watu wanavyozirai.
   
 16. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,264
  Trophy Points: 280
  Mkuu salama kabisa, ni mambo ya Tanesco haya yanatuathili.
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nilijua mambo yetu yaleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ya BAN
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,264
  Trophy Points: 280
  Inahusika hiyo,........ ni bora kujiunga FT family.
   
 19. Dickson Mpemba

  Dickson Mpemba JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Nafikiri umefika wakati wa kuangalia upya katiba yetu na kuruhusu mgombea binafsi ili watu wa igunga wasiporwe haki yao ya msingi ya kuwa na mwakilishi wanaemtaka .
   
 20. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Kuna watu waliwahi kulia wakoloni walipoondoka "uuuwi jamani sasa nani atatutawala?".
  Ujinga una raha zake.
   
Loading...