Rostam bado mbunge!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam bado mbunge!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyambala, Jul 21, 2011.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading"]Makinda asubiri barua ya Rostam CCM[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 20 July 2011 21:13[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]
  Spika wa Bunge,Anne Makinda​
  Leon Bahati, Dodoma, Elizabeth Ernest, Dar

  UAMUZI wa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya CCM, unaonekana kukitesa chama hicho kutokana uongozi wake hadi sasa kushindwa kuandika barua Ofisi ya Bunge kumjulisha hatua ya mbunge wake huyo.

  Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliliambia gazeti hili jana kuwa ofisi yake haikuwa imepata barua ya CCM hadi jana na kuongeza, "Sisi tungepata tungetangaza mara moja bungeni na kisha tungeiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)".

  Kwa mujibu wa Makinda, kiutaratibu mbunge anapojiuzulu, chama chake ndicho kinachopaswa kumjulisha Spika kwamba, kiti cha ubunge katika jimbo husika kiko wazi.Spika Makinda alikiri kupata barua ya Rostam, lakini hiyo haiwezi kuwa kigezo cha kutangaza kiti hicho kuwa kiko wazi kwani katiba inataja chama kuwa ndicho kinachopaswa kuliarifu Bunge.

  Awali Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, alisema, "Ofisi yangu bado haijapata taarifa rasmi za maandishi kuwa amejiuzulu (Rostam)! Hiyo ina maana bado tunamtambua kuwa ni mbunge." Joel alisema kwa mazingira hayo, Rostam bado anapata haki zake za kiubunge ikiwa ni pamoja na mshahara.

  Alifafanua kwamba hata angefika bungeni na kusaini mahudhurio, angepatiwa posho kama ilivyo kwa wabunge wengine.Kwa mujibu wa Joel, Ibara ya 71(f) ya Katibu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaeleza kuwa mbunge atakuwa amepoteza nafasi hiyo iwapo ataacha uanachama wa chama kilichompa kofia hiyo.

  Lakini ibara hiyo hiyo kifungu cha (C) kinalipa Bunge madaraka ya kumuengua mbunge kwenye nafasi hiyo iwapo hatahudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo bila ruhusa ya Spika."Ibara hiyo hiyo kipengele cha (g) kinazungumzia kuhusu nafasi kuwa wazi iwapo mbunge amefariki au kujiuzulu," alisema Joel.

  Lakini, suala la kujiuzulu kama lilivyoelezewa kwenye kipengele hicho halijafafanuliwa kwa undani hivyo ofisi ya Bunge lazima itumie busara za kisheria katika kuamua.

  CCM wapata ganzi kulijulisha Bunge

  Sekretarieti ya CCM imepata ganzi kuandika barua hiyo huku viongozi wake wakirushiana mpira katika kuzungumzia suala hilo.Jana Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, alishindwa kuzungumzia suala hilo alipotafuta na gazeti hili akieleza kuwa alikuwa kwenye kikao.Mukama alitoa sababu hiyo hata baada ya kupigiwa simu kwa zaidi ya saa tano.

  Hii si mara ya kwanza kwa Mukama kukata simu punde anapoulizwa kuhusu suala la Rostam kujiuzulu ubunge na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec).Majira ya asubuhi jana, mwandishi wa gazeti hili aliyefika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Dar es Salaam, alizuiwa na katibu muhutasi kukutana na Mukama.

  "Wewe na mhariri wako mnaonekana hamjui suala hili mtalifuatilia wapi, hii sio sehemu husika ya kufuatilia barua ya Rostam,"alisema Ramadhani Gabriel, katibu muhutasi wa Mukama.

  Nape akwepa jukumu
  Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, alipopigiwa simu kuulizwa juu ya suala hilo, alisema "Ndio naingia ofisini nitakupa majibu baadaye nitakapopata taarifa hizi."

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Kapteni John Chiligati alisema, "Katibu Mkuu alishatoa tamko kwamba amepokea barua ya Rostam."

  Hata hivyo, Chiligati alipotakiwa kueleza lini barua hiyo itapelekwa kwa Spika wa Bunge alijibu,"taarifa hizo aulizwa Katibu Mkuu mwenyewe."

  Habari za ndani zimeeleza kuwa CCM imechelewa kutoa taarifa hiyo kwa spika kwa sababu ilipata mshituko kutokana na hatua ya Rostam kuachia ujumbe wa Nec hadi ubunge.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, CCM ilitegemea Rostam angejiuzulu ujumbe wa Nec pekee, lakini hatua yake ya kujiuzulu na ubunge imekishtua chama hicho na hivyo kulazimika kuhaha kunusuru hali hiyo kwani kuna uwezekano Jimbo la Igunga likawa na upinzani mkubwa uchaguzi mdogo utapoitishwa.

  My Take:
  Ina maana chama au CCM for this matter wakaamua kusikilizia au kuuchuna bila kupeleka barua hiyo basi watu wa Igunga watakaa bila mbunge mpaka 2015?? Kweli amani na utulivu have made us really dumb!!

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,739
  Likes Received: 82,676
  Trophy Points: 280
  Duh! Huu ni ufisadi wa hali ya juu!!! Mtu katangaza rasmi kwamba kajiuzulu lakini bado analipwa mshahara na marupurupu mengine!!!! Kweli huu ni uthibitisho mwingine unaoonyesha kwamba hii Serikali ni ya mataahira!!!!
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema Rostam bado ni mbunge kwa kuwa hadi jana ofisi yake haikuwa imepata barua ya CCM ya kujiuzulu kwake na kuongeza, "Sisi tungepata tungetangaza mara moja bungeni na kisha tungeiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)". Hata hivyo Spika Makinda alikiri kupata barua ya Rostam, lakini akasema hiyo haiwezi kuwa kigezo cha kutangaza kiti hicho kuwa kiko wazi kwani katiba inataja chama kuwa ndicho kinachopaswa kuliarifu Bunge.

  Naye Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel amesema "Ofisi yangu bado haijapata taarifa rasmi za maandishi kuwa amejiuzulu (Rostam)! Hiyo ina maana bado tunamtambua kuwa ni mbunge." Joel alisema kwa mazingira hayo, Rostam bado anapata haki zake za kiubunge ikiwa ni pamoja na mshahara. Alifafanua kwamba hata angefika bungeni na kusaini mahudhurio, angepatiwa posho kama ilivyo kwa wabunge wengine.

  Habari za ndani ya CCM zimeeleza kuwa CCM imechelewa kutoa taarifa hiyo kwa spika kwa sababu ilipata mshituko kutokana na hatua ya Rostam kuachia ujumbe wa Nec hadi ubunge ilitegemewa Rostam angeachia ujumbe wa Nec pekee.

  Mwananchi
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani mkuu mpaka inachosha!!!!!
   
 5. g

  geophysics JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama ni hivi tutatoana ngeu sasa, mtu tajiri ana kila uwezo na amekuwa akiyumbisha uchumi kwa biashara zake haramu kupitia vyeo katika chama na ubunge iweje leo ajitoe harafu eti bunge liendelee kumlipa.... Hizo pesa si zingeokoa maisha ya watu watatu mpaka kumi hospitali ya Muhimbili..... Hapa sasa mnatafuta wananchi ubaya jamani.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Halafu wanakwambia hii ni serikali makini!!!!!!! Tanzania kweli ni zaidi ya uijuavyo!
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  sasa waliimba taarab watamvua gamba sijui kufanyajekufanyaje! kajivua mwenyewe wanaona aibu kumjibu? hii sumu ya barua za serikali ku-take forever kujibiwa kumbe inaanzia ccm?
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Umeona eeh!!!!!!, lakini najua tatizo la CCM, hwanasubiri kwanza msimamo wa mwenyekiti!!!!!!!!!!!! si wanafahamu kwamba yeye na RA ni washikaji, hivyo kila mtu anaogopa kufanya maamuzi rahisi kabisa kama hilo la barua. Huku ndipo CCM ilipotufikisha
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,469
  Likes Received: 19,854
  Trophy Points: 280
  muongo huyu makinda
   
 10. D

  Daty Senior Member

  #10
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kujiuzulu naona imekuwa fashion kwa viongoz wetu. Dah hii nchi yetu . Lini watachukuliwa sheria?
   
 11. Jilanga

  Jilanga JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  CCM lazima wapate mshtuko/kigugumizi, Mchango wa Rostam kui-finance Ccm hukuwa mdogo! Wote wanatambua fika uchaguzi mkuu 2005 mchango wake kwa kulipa fadhila ya kumpa udhabun wa kufua umeme wa zarura na compuny fake {Richmond}
  Napenda sana mfumo wa China!
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nadhani hili ndilo linalowahangaisha
   
 13. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Makinda asubiri barua ya Rostam CCM [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  UAMUZI wa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya CCM, unaonekana kukitesa chama hicho kutokana uongozi wake hadi sasa kushindwa kuandika barua Ofisi ya Bunge kumjulisha hatua ya mbunge wake huyo.

  Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliliambia gazeti hili jana kuwa ofisi yake haikuwa imepata barua ya CCM hadi jana na kuongeza, "Sisi tungepata tungetangaza mara moja bungeni na kisha tungeiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)".

  Kwa mujibu wa Makinda, kiutaratibu mbunge anapojiuzulu, chama chake ndicho kinachopaswa kumjulisha Spika kwamba, kiti cha ubunge katika jimbo husika kiko wazi.Spika Makinda alikiri kupata barua ya Rostam, lakini hiyo haiwezi kuwa kigezo cha kutangaza kiti hicho kuwa kiko wazi kwani katiba inataja chama kuwa ndicho kinachopaswa kuliarifu Bunge.

  Awali Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, alisema, "Ofisi yangu bado haijapata taarifa rasmi za maandishi kuwa amejiuzulu (Rostam)! Hiyo ina maana bado tunamtambua kuwa ni mbunge." Joel alisema kwa mazingira hayo, Rostam bado anapata haki zake za kiubunge ikiwa ni pamoja na mshahara.

  Alifafanua kwamba hata angefika bungeni na kusaini mahudhurio, angepatiwa posho kama ilivyo kwa wabunge wengine.Kwa mujibu wa Joel, Ibara ya 71(f) ya Katibu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaeleza kuwa mbunge atakuwa amepoteza nafasi hiyo iwapo ataacha uanachama wa chama kilichompa kofia hiyo.

  Lakini ibara hiyo hiyo kifungu cha (C) kinalipa Bunge madaraka ya kumuengua mbunge kwenye nafasi hiyo iwapo hatahudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo bila ruhusa ya Spika."Ibara hiyo hiyo kipengele cha (g) kinazungumzia kuhusu nafasi kuwa wazi iwapo mbunge amefariki au kujiuzulu," alisema Joel.

  Lakini, suala la kujiuzulu kama lilivyoelezewa kwenye kipengele hicho halijafafanuliwa kwa undani hivyo ofisi ya Bunge lazima itumie busara za kisheria katika kuamua.

  CCM wapata ganzi kulijulisha Bunge

  Sekretarieti ya CCM imepata ganzi kuandika barua hiyo huku viongozi wake wakirushiana mpira katika kuzungumzia suala hilo.Jana Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, alishindwa kuzungumzia suala hilo alipotafuta na gazeti hili akieleza kuwa alikuwa kwenye kikao.Mukama alitoa sababu hiyo hata baada ya kupigiwa simu kwa zaidi ya saa tano.

  Hii si mara ya kwanza kwa Mukama kukata simu punde anapoulizwa kuhusu suala la Rostam kujiuzulu ubunge na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec).Majira ya asubuhi jana, mwandishi wa gazeti hili aliyefika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Dar es Salaam, alizuiwa na katibu muhutasi kukutana na Mukama.

  “Wewe na mhariri wako mnaonekana hamjui suala hili mtalifuatilia wapi, hii sio sehemu husika ya kufuatilia barua ya Rostam,”alisema Ramadhani Gabriel, katibu muhutasi wa Mukama.

  Nape akwepa jukumu
  Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, alipopigiwa simu kuulizwa juu ya suala hilo, alisema “Ndio naingia ofisini nitakupa majibu baadaye nitakapopata taarifa hizi.”

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Kapteni John Chiligati alisema, "Katibu Mkuu alishatoa tamko kwamba amepokea barua ya Rostam."

  Hata hivyo, Chiligati alipotakiwa kueleza lini barua hiyo itapelekwa kwa Spika wa Bunge alijibu,"taarifa hizo aulizwa Katibu Mkuu mwenyewe."

  Habari za ndani zimeeleza kuwa CCM imechelewa kutoa taarifa hiyo kwa spika kwa sababu ilipata mshituko kutokana na hatua ya Rostam kuachia ujumbe wa Nec hadi ubunge.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, CCM ilitegemea Rostam angejiuzulu ujumbe wa Nec pekee, lakini hatua yake ya kujiuzulu na ubunge imekishtua chama hicho na hivyo kulazimika kuhaha kunusuru hali hiyo kwani kuna uwezekano Jimbo la Igunga likawa na upinzani mkubwa uchaguzi mdogo utapoitishwa.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 14. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Mkuu taarifa ndogo hapo penye red, Ilikuwa nadra sana RA kumkuta akisaini posho ya Ubunge bali alikuwa akiitoa kwa wabunge viherehere kama hongo isiyo rasmi na ndio waliokuwa wanasaini hizo posho, jiulize kwanza mtu mwenyewe alikuwa anaonekana Dodoma kwenye ufunguzi na pengine kwenye kufunga Bunge tu then huo muda wa kufuatilia posho angeupata wapi?

  Posho kwake haikuwa dili mzee bali aliitumia kulainisha viherehere
  [​IMG]
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Spika wetu naye! Kifungu cha 149(1)(d) cha KATIBA yetu ya JMT kinasema taarifa ya Mbunge kujiuzulu anapelekewa Spika hayo ya chama anayatoa wapi kama sio kulewa enzi hizo za mfumo wa chama dola?
   
Loading...