Rostam ajipanga kuikimbia Tanzania; kutimkia Malaysia

Anyang'anywe passport mapema kabla na apandishwe kizimbani kujibu tuhuma kama anazo.
 
Shamba la bibi hili. Mwacheni achume mpaka achoke, sisi wa TZ kazi yetu ni kupiga kelele...
 
Aende yeye mwenyewe kama alivyokuja TZ, fedha zetu asiruhusiwe kwenda nazo!!
 
Inawezekana kabisa kuwa pesa aliyonayo ni nyingi kiasi kwamba benki hizo zilikuwa zinategemea pesa hizo katika mzunguko mzima wa biashara ndio maana wanataka kwanza wakae wajue cha kufanya.
Ningekuwa na uwezo nikazitaifisha pesa zote na kumuacha aende zake tu maana ni tishio kwa maendeleo ya nchi na wananchi wake.
 
Teh teh teh teh teh tumwombe msamaha maana akiondo anaondoka na robo tatu ya pesa zote nchini. Lol !
 
Du, CRDB Bank PLC ilifungua account ya yale makampuni yaliyohamishiwa pesa iliyokwapuliwa kwenye akaunti ya EPA kule BOT!

Nasikia aliyedhamini ufunguzi wa akaunti hizo ni Yusufu Manji.
 
Tuseme ukweli kwa mtu makini kama Rostam hilo angelistukia leo? kwamba agizo la BOT lilivyotoka naye akaanza pilika za kufunga akaunti zake..sikubali kirahisi.Kwa sababu yeye mwenyewe ana makampuni kadhaa yanayo-operate hapa nchini na inawezekana kabisa anazo fedha kiasi kidogo (kwa viwango vyake) kwa ajili ya kuendeleza shughuli zake - hawezi kuzihamisha.

Hawezi kuwa amestuka leo,kama ni kuzihamisha tayari alishazihamisha siku nyingi kama alivyohamisha hisa za Vodacom kwenda South africa.Tusisahau alipokuwa anaongea na waandishi wa habari 2010 kumjibu Mengi kuhusu tuhuma za kuwa na account nje ya nchi - alisemaje? "Nampa changamoto Mengi aseme na yeye kama hana akaunti nje ya nchi"
 
Kuna mzee mmoja ni maarufu sana siwezi kumtaja (ni mmoja wa maafisa wa Usalama wa Taifa) kwa usalama wangu maana natumia ID yangu orginal pamoja na Avatar ya picha yangu halisi..... alichoniambia kwamba Rostam Aziz ni Jasusi la CIA na yuko very protected, alikuja hapa kwa lengo maalum na kazi aliyoifanya ameshaimaliza na aliletwa na Marehemu Kambona....
siwezi endelea zaidi............
 

Mkuu, JF sio sehemu ya porojo wala kijiwe cha mbege! Kwa hiyo unapoleta data zako humu JF kwa Great Thinkers lazima uwe na facts za kutosha.

Sio kuokota maneno mitaani na kwenye magazeti ya udaku ndio ushahidi wako..

Ebu weka hiyo barua ya Rostam Aziz, humu JF tuione ndio tujadili zaidi ya hapo tutakuwa tunajadili umbeya!
 
yaani jamaa na mchuzi mpaka benki zinajishauri? huyu jamaa kweli ametushika...
 

sema yote kuwa

1. theluthi ya fedha zilizoko uko benki ni za Rostam
2. kuwa akine kimei walifunga safari kumfuata ughaibuni kumuomba abadilishe uamuzi wake akakataa
3. alichowasadia ni kuwa atazitoa fedha kwa awamu
4. anai-ondoa na kampuni yake ya caspian ambayo makao yakemakuu ni uarabuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…