kijana ni muhimu ukawa umefanyia utafiti jambo unalotakasema kwa public kabla hujasema.
MUST pana aina mbili za hostels, kuna za zamani(diploma) block 6, na mpya(bachelor), block 8. Lakin hizi za zamani hukaliwa na wanafunzi wa bachelor pia ambao huchelewa kuripot kwani kule block 8 kunakuwa kumejaa.
Nichukue fursa hii kukutoa hofu kuwa vyumba vina ukubwa wa kuweza kukuaccomodate vizuri, vyumba vya block 6 ni vikubwa zaidi. Pia mzunguko wa hewa ndan ya chumba ni mzuri ukizingatia Mbeya ni mkoa wa baridi na upepo kiasi, Na pia hamna habari ya kubebana kama sehemu nyingine, kifupi ishu ya accomodation sio tatizo. Pia kuna nyumba nyingi zipo kuzunguka chuo, gharama yake kwa chumba ni kati ya 20000 had 35000.
Karibu
Daah inatia simanzi,kuna watu wanasoma kwa shida sana
Diploma ndo ipo hivyo mkuu. Degree ni watu wa-nne. Ukifika wakati gombea U-rais pale upewe chumba chako na ofisi kubwaaaa!!!
mbeya university of science and technology...nilikuwa nasoma join instruction yao hawa jamaa...nilipofika kwenye mambo ya hostel nikachoka....eti chumba watu 8. jaman ...,kama watoto wa secondary....kumbe ni watu wanaosomea shahada....
Unajua nin mkuu...wengi wetu huwa tunaongea mambo kutokana experience,mi nimetoka diploma dit...mwaka wa 3 tulikuwa tunakaa room watu 2 tu....na watu wa shahada wao kuanzia mwaka wa kwanza mpaka wa mwisho wanakaa room watu wa2 tu....kwa hyo nikiona sehemu kuna tofaut lazima nishangae...tena afadhali ingekuwa tofauti ndogo kama vile watu 3 au wa4..lkn kutoka wa2 mpaka 8...hapo nikishangaa si ajabu...
Me enyewe nmeshangaa sana baada ya kuisoma ile fom aisee !! Wa2 8 duuuuuuh
Mkuu kwa MUST kila kitu kipo poa isipokuwa kitu kimoja tu "CANTEEN"
Hii sehemu kwakweli aliye design sijui ni nani. MUST ni moja ya Chuo kizuri sana kwa hii fani ya Usanifu Majengo lakini aliyedesign hiyo Canteen siyo kabisa.
Mkuu hawajajenga nyingine?
Kuhusu room za kulala watu 8 ni sawa tu maana room ni kubwa sana hasa zile za Block 7, Block 6A and 6B. Kuhusu hizi mpya nazo room ni kubwa sana.
MUST ni sehemu nzuri sana ya kusoma kiukweli.