Rommy Jones amwita Gabo Zigamba mshamba

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
8,600
2,000
Hit maker wa ngoma ya bora iwe Rommy Jones ambaye amemshirikisha Baraka the prince mpenzi halali kabisa wa ex wa Mr Blue hapa namzungumzia Naj , Rommy Jones ameibua hisia za chuki kwa baadhi ya mashabiki wa Gabo Zigamba baada ya kumwita Gabo kwamba ni mshamba aliyepitwa na wakati .

Kauli hii baadhi ya wadau waiisapoti huku wengine wakiwa wamechukizwa sana na kauli hiyo na kuwambia Rommy Jones aache tabia za kike kwa kuwa haipendezi kwa mwanaume kumdhalilisha mwanaume mwenzake mbele za watu.

Rommy alimwita hivyo Gabo baada ya Wema Sepetu kupost picha akiwa na Gabo na Wema akaandika BEST ACTOR & ACTRESS 2018 , ila kutokana na pozi la kiajabu ajabu alilokuwa ameweka Gabo ambalo kwa haraka haraka ilikuwa inaonesha kama anamuogopa Wema ,Rommy hakusita kumchana Gabo kwa kuzubaa zubaa na akamuita ni mshamba sana Gabo japo kwa sasa anajifanya mtoto wa mjini.

Wadau mbalimbali mpaka sasa bado wanasubiri kuona Gabo atamjibu Rommy kutokana na kudhalilishwa na Rommy .

IMG_20180503_024731_205.jpg
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,163
2,000
Wao wameshazoea pozi za kumkumbatia kila mtu hata kama huna uhusiano naye wa kimapenzi ilimradi aonyeshe kuwa ana confidence,kumbe huo ndio ushamba,unapokuwa unajiheshimu au unajielewa mtu anayekukumbatia kijinga kama alivyofanya Wema ni lazima uonyeshe hali flani ya kutokukubali aina ya mkumbatio aliokupa,kwani wengine huchukulia hizo opportunity kukuchafua baadaye...
 

MKIKUU

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
336
500
Wao wameshazoe pozi za kumkumbatia kila mtu hata kama huna uhusiano naye wa kimapenzi ilimradi aonyeshe kuwa ana confidence,kumbe huo ndio ushamba,unapokuwa unajiheshimu au unajielewa mtu anayekukumbatia kijinga kama alivyofanya Wema ni lazima uonyehe hali flani ya kutokukubali aina ya mkumbatio aliokupa,kwani wengine huchukulia hizo opportunity kukuchafua baadaye...
Umenena ukweli mtupu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom