Mtukutu wa Nyaigela
JF-Expert Member
- Sep 4, 2018
- 6,545
- 11,093
Yesu hawezi kufanya huo ujinga, wa kutengeneza pombe halafu aseme walevi hawaendi mbinguni!! Unaweza kuwa unafiki wa mwaka.Hivi unajua satisfaction ya kunywa pombe ni kulewa? Kwa hiyo hakuna tofauti kati ya kunywa pombe na kulewa. Msijidanganye. Na kumbuka pombe hupunguza uwezo wa kufikiriUle muujiza wa kwanza wa Yesu kwenye ile harusi ya Kana alibadilisha maji kuwa divai, au nyie wenzetu mnafikiri ile ilikuwa juice?
Hawa dawa yao ni kucharazwa bakola sio maombi.Viongozi wa Kanisa Katoliki wilayani Rombo wameanza kufunga kwa siku tisa kumuomba Mungu aiepushe jamii wilayani humo na tabia ya ulevi uliopindukia hususan kwa vijana.
Kwa mujibu wa viongozi hao, vijana wengi wanashindwa kuoa kutokana na ulevi.
Mkuu wa Vikarieti ya Rombo na paroko wa Usseri, Padri Emmanuel Lyimo alisema wameamua kufunga ili kukisaidia kizazi hicho kiweze kupenda kazi kuliko unywaji pombe.
Alisema Tanzania inapoteza vijana wanaotegemewa kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa uchumi wa Taifa.
Paroko huyo alisema kukithiri kwa unywaji wa pombe haramu katika wilaya hiyo kunatokana na vijana wengi kutokuwa na kazi za kufanya, badala yake wanaishia kwenye vilabu vya pombe na hatimaye kushiriki katika matukio mbalimbali ya uhalifu.
Kiongozi huyo wa dini aliiomba Serikali kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili kupunguza uzururaji wa vijana pamoja na vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji.
“Ni lini Serikali itakomesha unywaji wa pombe haramu pamoja na mauaji yasiyo na hatia Rombo?” alihoji paroko huyo.
“Serikali endapo itaanzisha vikundi vya ujasiriamali, haya matukio ambayo yanaendelea kwa sasa hayatakuwepo, kanisa tupo tayari kupitia jumuiya ndogo ndogo kuwakusanya vijana ili iwe rahisi kuwafikia walengwa.”
Alisema, “yapo makundi mbalimbali ya vijana yameibuka katika wilaya hii, wanavunja na kuchoma nyumba za watu, kupora pamoja na kuua. Hii hali kiukweli inasikitisha.”
Padri Lyimo alisema kutokana na hali hiyo waumini wa kanisa hilo wameamua kufunga na kuomba ili Mungu ainusuru jamii na matukio ya kihalifu yanayotokea.
Kiongozi wa jumuiya ya kanisa hilo, Athanas Joseph alisema wameamua kufunga baada ya kuchoshwa na matukio ya kihalifu yanayosukumwa na ulevi kupindukia miongoni mwa vijana.
“Sasa hivi hakuna vijana wanaooa, wengi wameishia kunywa pombe haramu, vijana wengi unakuta wanakunywa pombe aina ya gongo na mbundimbundi ambazo zinawamaliza nguvu kabisa,” alisema.
“Hapa kuoa hawawezi kabisa na mwisho wake baada ya muda kijana wa miaka 20 utafikiri ni mzee wa miaka 60.”
Aliitaka Serikali kuangalia namna ya kuwanusuru vijana wilayani humo kwa sababu wanaangamia.
“Kizazi kijacho hatutakuwa na vijana imara katika wilaya hii, tunaomba Serikali itusaidie kuwapatia vijana hawa mtaji angalau wajiingize katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali,” alisema Joseph.
Kwa mujibu wa wakazi wa wilaya hiyo, kuna zaidi ya aina 52 za pombe za kienyeji zinazonywewa wilayani humo.
Mmoja wa wakazi hao, Alfred Martin aliliambia Mwananchi kuwa kutokana na wingi wa pombe hizo na jamii kutokuwa na mbinu madhubuti za kudhibiti unywaji kupita kiasi, inakuwa rahisi kwa vijana kujiingiza katika tabia hiyo.
“Labda tu itokee kwamba kuna mkakati maalumu, lakini vinginevyo iwe ni maombi na ibada ili Mungu atusaidie,” alisema.
Naomba nikusahihishe, hakuna kanisa linalomiliki baa, pili ukienda baa umeenda kwa miguu yako mwenyewe na pesa unayoitoa ni pesa yako, na pombe unakunywa kwa akili yako mwenyewe, hakuna mtu anakunywesha sasa sijui kanisa linahusika vipi hapo, kwani hata mliokatazwa kunywa pombe mbona wengi wenu tunakutana baa huko, wengine wananunua wanaenda kunywa nyumbani ili wasionekane, wengine wanafanya kazi kwenye viwanda vya pombe, anzeni kuwakemea hao kwanza.
Yesu hawezi kufanya huo ujinga, wa kutengeneza pombe halafu aseme walevi hawaendi mbinguni!! Unaweza kuwa unafiki wa mwaka.Hivi unajua satisfaction ya kunywa pombe ni kulewa? Kwa hiyo hakuna tofauti kati ya kunywa pombe na kulewa. Msijidanganye. Na kumbuka pombe hupunguza uwezo wa kufikiri
Yes unaona maonyo juu ya ulevi na pia matumizi mazuri ya pombe. Mpinga Kristo ni yule anayefundisha mafundisho ya Yesu kinyume hata kama unafikiri lengo ni kukataza ulevi. Hekima ya Mungu yatosha tusijifanye tuna hekima kuliko Mungu mwenyewe. Tuijue kweli na tufundishe kweli watu waamue wenyewe baada ya kujua faida na hasara.Ushauri alikuwa anapewa Mfalme Lemueli na mama yake, nimependa mama anavyo muasa mtoto wake
Mithali 31:1-10
4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?
5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.
Miradi unayoiona katika eneo la kanisa sio yote ni ya kanisa, mingine inakuwa ni ya vikundi mbalimbali.Unakaa wapi mkuu? Kama unaweza kufika kanisa la roman ukonga. Moja ya miradi yake hapo tu jirani na kanisa ni bar na zahanati
1 Petro 2:9Ushauri alikuwa anapewa Mfalme Lemueli na mama yake, nimependa mama anavyo muasa mtoto wake
Mithali 31:1-10
4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?
5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.
rombo 99%ni wakatolikiPombe haijakatazwa, kilichokatazwa ni ULEVI ambao ni zao la kunywa kupita kiasi, kama ilivyo kwenye kula, ukila kupita kiasi (ulafi) ni dhambi vile vile. Kwani umeambiwa wanaokunywa pombe huko rombo ni wakatoliki pekee?
Hakuna cha afadhali. acha kudanganyika na kauli za kipadre hizoUmeambiwa wanaombewa vijana walevi.
By the way ni afadhali asiyekataza pombe, kuliko anayekataza halafu anakunywa!
Mkuu nadhani unaona reaction ya watu humu wanatetea pombe sasa huko ndio kwenye mizizi ya kanisa linaloruhusu kunywa pombe. Ukifanya mkutano wa injili huko, viongozi wa hilo kanisa wanazuia watu wao wasijeHii reaction yote ni kwa kuwa Kanisa limechukua hatua ya kuendesha maombi. Jambo la ajabu, wanaolishambulia kanisa wao hawajachukua hatua yoyote! Yaani wanasubiri mwingine afanye, wao waongee! Wasabato nendeni basi ninyi Rombo mkaendeshe maombi, sio kupinga tu!
Mkuu hii haikubaliki. Hiki kikao nami nipohatari fire,migambo inaruka na kukanyagana yenyeweView attachment 1057059
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kulima watu walikuwa wanapelekwa mikoani kwanini wasipelekwe pia kwa hili jambo?Serikali inabidi iunde kikosi kazi cha vijana wenye nguvu wakawasaidie kima mama na wanawake wa Rombo kutokana na wanaume wa Rombo kutojishughulisha kabisa na mambo ya chumbani zaidi ya pombe, ugwadu utawaua wamama wa Rombo, au serikali inataka waanze kukodi wanaume kutoka Kenya tena, tupate aibu tena ya kuimport wanaume kutoka nchi jirani?
Serikali iunde kikosi kazi cha vijana wenye nguvu, wapelekwe Rombo, vijana 10 wanapewa kata moja kushughulikia, kazi yao kuanzia asubuhi hadi jioni ni kutoa huduma. Ile aibu ya miaka ile sitaki tena itupate, bado hii nchi ina vijana wenye nguvu kuweza kuokoa jahazi na kuwatunzia heshima wanaume wenzetu wa Rombo.
KumbeRombo kwa zaidi ya asilimia 90 ni wakatoliki.
Iweje sasa wakatoliki wamwombe Mungu kuwaepusha na asili yao?
Ili parokia ikamilike ni lazima wawe na duka la vilevi. Kuna bar moja huko Moshi eneo la mji mdogo Himo, ina bar inayoitwa Kilacha. Hii bar ni maarufu kwa mapadre na masista kupombeka. Tena inamilikiwa na kanisa.
Shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake ati...........!
Sent using Jamii Forums mobile app