Rombo: Viongozi wa Kanisa Katoliki kufunga siku 9 kuomba Mungu aponye jamii na ulevi

Ule muujiza wa kwanza wa Yesu kwenye ile harusi ya Kana alibadilisha maji kuwa divai, au nyie wenzetu mnafikiri ile ilikuwa juice?
Yesu hawezi kufanya huo ujinga, wa kutengeneza pombe halafu aseme walevi hawaendi mbinguni!! Unaweza kuwa unafiki wa mwaka.Hivi unajua satisfaction ya kunywa pombe ni kulewa? Kwa hiyo hakuna tofauti kati ya kunywa pombe na kulewa. Msijidanganye. Na kumbuka pombe hupunguza uwezo wa kufikiri
 
Ushauri alikuwa anapewa Mfalme Lemueli na mama yake, nimependa mama anavyo muasa mtoto wake
Mithali 31:1-10
4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?
5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.
 
Viongozi wa Kanisa Katoliki wilayani Rombo wameanza kufunga kwa siku tisa kumuomba Mungu aiepushe jamii wilayani humo na tabia ya ulevi uliopindukia hususan kwa vijana.

Kwa mujibu wa viongozi hao, vijana wengi wanashindwa kuoa kutokana na ulevi.

Mkuu wa Vikarieti ya Rombo na paroko wa Usseri, Padri Emmanuel Lyimo alisema wameamua kufunga ili kukisaidia kizazi hicho kiweze kupenda kazi kuliko unywaji pombe.

Alisema Tanzania inapoteza vijana wanaotegemewa kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa uchumi wa Taifa.

Paroko huyo alisema kukithiri kwa unywaji wa pombe haramu katika wilaya hiyo kunatokana na vijana wengi kutokuwa na kazi za kufanya, badala yake wanaishia kwenye vilabu vya pombe na hatimaye kushiriki katika matukio mbalimbali ya uhalifu.

Kiongozi huyo wa dini aliiomba Serikali kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili kupunguza uzururaji wa vijana pamoja na vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji.

“Ni lini Serikali itakomesha unywaji wa pombe haramu pamoja na mauaji yasiyo na hatia Rombo?” alihoji paroko huyo.

“Serikali endapo itaanzisha vikundi vya ujasiriamali, haya matukio ambayo yanaendelea kwa sasa hayatakuwepo, kanisa tupo tayari kupitia jumuiya ndogo ndogo kuwakusanya vijana ili iwe rahisi kuwafikia walengwa.”

Alisema, “yapo makundi mbalimbali ya vijana yameibuka katika wilaya hii, wanavunja na kuchoma nyumba za watu, kupora pamoja na kuua. Hii hali kiukweli inasikitisha.”

Padri Lyimo alisema kutokana na hali hiyo waumini wa kanisa hilo wameamua kufunga na kuomba ili Mungu ainusuru jamii na matukio ya kihalifu yanayotokea.

Kiongozi wa jumuiya ya kanisa hilo, Athanas Joseph alisema wameamua kufunga baada ya kuchoshwa na matukio ya kihalifu yanayosukumwa na ulevi kupindukia miongoni mwa vijana.

“Sasa hivi hakuna vijana wanaooa, wengi wameishia kunywa pombe haramu, vijana wengi unakuta wanakunywa pombe aina ya gongo na mbundimbundi ambazo zinawamaliza nguvu kabisa,” alisema.

“Hapa kuoa hawawezi kabisa na mwisho wake baada ya muda kijana wa miaka 20 utafikiri ni mzee wa miaka 60.”

Aliitaka Serikali kuangalia namna ya kuwanusuru vijana wilayani humo kwa sababu wanaangamia.

“Kizazi kijacho hatutakuwa na vijana imara katika wilaya hii, tunaomba Serikali itusaidie kuwapatia vijana hawa mtaji angalau wajiingize katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali,” alisema Joseph.

Kwa mujibu wa wakazi wa wilaya hiyo, kuna zaidi ya aina 52 za pombe za kienyeji zinazonywewa wilayani humo.

Mmoja wa wakazi hao, Alfred Martin aliliambia Mwananchi kuwa kutokana na wingi wa pombe hizo na jamii kutokuwa na mbinu madhubuti za kudhibiti unywaji kupita kiasi, inakuwa rahisi kwa vijana kujiingiza katika tabia hiyo.

“Labda tu itokee kwamba kuna mkakati maalumu, lakini vinginevyo iwe ni maombi na ibada ili Mungu atusaidie,” alisema.
Hawa dawa yao ni kucharazwa bakola sio maombi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba nikusahihishe, hakuna kanisa linalomiliki baa, pili ukienda baa umeenda kwa miguu yako mwenyewe na pesa unayoitoa ni pesa yako, na pombe unakunywa kwa akili yako mwenyewe, hakuna mtu anakunywesha sasa sijui kanisa linahusika vipi hapo, kwani hata mliokatazwa kunywa pombe mbona wengi wenu tunakutana baa huko, wengine wananunua wanaenda kunywa nyumbani ili wasionekane, wengine wanafanya kazi kwenye viwanda vya pombe, anzeni kuwakemea hao kwanza.

Unakaa wapi mkuu? Kama unaweza kufika kanisa la roman ukonga. Moja ya miradi yake hapo tu jirani na kanisa ni bar na zahanati
 
Yesu hawezi kufanya huo ujinga, wa kutengeneza pombe halafu aseme walevi hawaendi mbinguni!! Unaweza kuwa unafiki wa mwaka.Hivi unajua satisfaction ya kunywa pombe ni kulewa? Kwa hiyo hakuna tofauti kati ya kunywa pombe na kulewa. Msijidanganye. Na kumbuka pombe hupunguza uwezo wa kufikiri

Kwa hiyo ule muujiza ulikuwa ni wa nini mkuu. Inawezekana tunasoma vitabu tofauti, mbona kuna wengi wananidhamu ya kunywa pombe. Naona kama umeamua ku generalize kwamba wanaokunywa pombe wote ni walevi.
 
Ushauri alikuwa anapewa Mfalme Lemueli na mama yake, nimependa mama anavyo muasa mtoto wake
Mithali 31:1-10
4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?
5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.
Yes unaona maonyo juu ya ulevi na pia matumizi mazuri ya pombe. Mpinga Kristo ni yule anayefundisha mafundisho ya Yesu kinyume hata kama unafikiri lengo ni kukataza ulevi. Hekima ya Mungu yatosha tusijifanye tuna hekima kuliko Mungu mwenyewe. Tuijue kweli na tufundishe kweli watu waamue wenyewe baada ya kujua faida na hasara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii reaction yote ni kwa kuwa Kanisa limechukua hatua ya kuendesha maombi. Jambo la ajabu, wanaolishambulia kanisa wao hawajachukua hatua yoyote! Yaani wanasubiri mwingine afanye, wao waongee! Wasabato nendeni basi ninyi Rombo mkaendeshe maombi, sio kupinga tu!
 
Ushauri alikuwa anapewa Mfalme Lemueli na mama yake, nimependa mama anavyo muasa mtoto wake
Mithali 31:1-10
4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?
5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.
1 Petro 2:9
''Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu''

Je, Sisi Ni Makuhani Wa Mungu?
Mimi ni kuhani. Wewe ni kuhani kama umezaliwa tena katika ufalme wa Mungu. Kwa hiyo kama tumezaliwa tena basi sisi wote ni makuhani katika ufalme wa Mungu na Yesu Kristo ndiye Kuhani Mkuu. Kwa hiyo Biblia inatufundisha wazi kwamba wakristo wote ni makuhani. Lakini baada ya kufunguliwa ufalme wa Mungu watu walianza kufundisha kwamba kuna wakubwa tu ambayo ni makuhani. Ndiyo maana leo katika madhehebu mbali mbali wanao Makuhani na washiriki tu wa kawaida. Na wanamini ndiyo kazi tu ya Mkuhani kutoa “Sakramenti” kwa Mungu. Lakini tutaangalia leo, Makuhani ni nani na Kazi yao ni nini? Kuhani ni Nini? Neno “Kuhani” katika Agano Jipya lina maana mtoto wa mfalme au mtumishi. Na makuhani wote kwenye maandiko ni lazima wawe na madhabahu na ni lazima watoe sadaka. Na hakuna mtu kwenye maandiko alikuwa na uwezo wa kutoa sadaka kwa ajili ya watu mbele ya Mungu. Ndiyo Manabii wengi wametoa sadaka, lakini kazi ya manabii ni kutumikia Mungu kwa ajili ya watu. Lakini kazi ya Kuhani ni kutumikia Watu mbele ya Mungu. Kwa tofauti ipo. Na hata leo kama wewe ni kuhani ni lazima utoe matoleo na sadaka kwa Mungu. Kuhani Wetu Leo Kama Kanisa. Hatuwezi kusoma kuhusu Ukuhani wa Yesu mpaka kitabu cha Waebrania katika Agano Jipya. Na hapa mwandishi anamtukuza yeye kama Kuhani Mkuu wa pekee na wa milele. Yeye tu ni Kuhani Mkuu wetu na hakuna mwingine. Amekwisha mwaga damu yake kwa ajili yetu na damu yake yanafaa milele. Lakini Ukuhani wetu umetajwa kidogo sana katika kitabu cha Waebrania. Ni Ebr. 10:22 inafundisha sisi jinsi tunavyokuwa Makuhani. Na Ebr. 13:15-16, intufundisha tunahitaji kutoa matoleo gani kwa Mungu. Waebrania 13:15-16. Hapa tunaona mwandishi wa kitabu hiki anaongea kuhusu kazi ya Mkristo ambaye ni kazi ya kuhani tena. Kwa hiyo tunaona hapa kwamba sio Makuhani walionahaki ya kutoa sadaka kwa Mungu. Sio sadaka ya Wanyama bali sadaka Mungu anayohitaji siku hizi. 1 Pet. 2:5-9. Petro katika barua hii anaongea na Wakristo waliotawnyika sana. Na katika mstari wa tano Petro anasema ninyi nanyi? ______________________ na _________________________. Alikuwa ana onyesha Wakristo wa leo wanayotakiwa kuachana na dunia na kwa hiyo Wakristo sio Hekalu tu (1 Kor. 6:16-20) bali ni makuhani katika miili yao. Tena katika mstari wa tisa aliongeza kwamba sisi ni “Ukuhani wa kifalme”. Alikuwa na tukuzwa hali yetu ya kiroho na uhusiano wetu na Mungu. Na leo kwa sababu sisi ni Makuhani basi ni lazima tutoa matoleo au sadaka kama Mungu anavyotaka leo na ni laimza tukumbuke kuwa ni Makuhani tu walioamriwa kutoa sadaka. Na kama Makuhani au watu wa Mungu sisi ni mali yake, na kama tu mali yake tunakaribia kiti cha ufalme wake kupitia Kuhani Mkuu Yesu Kristo, 1 Tim. 2:5. Ufunuo 1:6. Yohana mtume aliyependwa sana na Yesu anakumbusha sisi katika mstari huu kwamba Kristo alitufanya sisi, “Kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu.” Kwa jumla sisi wote ni Ufalme wake lakini peke yetu kila moja ni kuhani katika Ufalme wake. Ndiyo, Yohana mwenyewe alitufundisha sisi kuwa ni makuhani mbele za Mungu. Hakusema walikuwa wachache ndani ya Kanisa ambao ni Makuhani lakini ni sisi wote, tena alirudia maneno yale yale katika 5:10. Warumi 12:1. Angalia maneno machache hapa: “Ndugu...Dhabihu....Ndiyo ibada yenu yenye maana.” Ndugu sio watu waliochagulia na kusoma shule fulani walikuwa na kutoa dhabihu au ibada yenye maana. Ni Wakristo wote! Kwa sababu tunajua Makuhani tu wanaweza kutoa sadaka katika Agano Jipya, mstari huu unaonyesha ndugu ni makuhani na ni lazima tutii mstari huu. Kwa hiyo ni lazima tushukuru tu kwamba sisi wote ni makuhani na hatuhitaji kupitia mtu au mwanadamu ye yote ilitufike kwa Mungu. Ni kupitia Yesu tu. Matoleo au Sadaka ya Kuhani ni Nini Leo? Tumesoma sehemu nyingi, tayari tumeona kazi nyingi ya kuhani siku hizi chini ya Agano Jipya. Kwa hiyo tuangalie oradha ya kazi tunayoweza kufanya kazi zile ni kama sadaka kwa Mungu. Imani yetu ni Sadaka. Upendo wa Mungu si
 
hatari fire,migambo inaruka na kukanyagana yenyewe
54514007_151737695858557_6904728736134249381_n.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii reaction yote ni kwa kuwa Kanisa limechukua hatua ya kuendesha maombi. Jambo la ajabu, wanaolishambulia kanisa wao hawajachukua hatua yoyote! Yaani wanasubiri mwingine afanye, wao waongee! Wasabato nendeni basi ninyi Rombo mkaendeshe maombi, sio kupinga tu!
Mkuu nadhani unaona reaction ya watu humu wanatetea pombe sasa huko ndio kwenye mizizi ya kanisa linaloruhusu kunywa pombe. Ukifanya mkutano wa injili huko, viongozi wa hilo kanisa wanazuia watu wao wasije
 
Hahah, hippocrites, wao hawaoi na hawaachi kunywa divai na pombe humo parokiani, lakini wanalaumu vijana kwa kutooa na kunywa pombe, waanze wao kuonyesha mfano, waoe na waache kunywa divai (pombe).
 
Serikali inabidi iunde kikosi kazi cha vijana wenye nguvu wakawasaidie kima mama na wanawake wa Rombo kutokana na wanaume wa Rombo kutojishughulisha kabisa na mambo ya chumbani zaidi ya pombe, ugwadu utawaua wamama wa Rombo, au serikali inataka waanze kukodi wanaume kutoka Kenya tena, tupate aibu tena ya kuimport wanaume kutoka nchi jirani?

Serikali iunde kikosi kazi cha vijana wenye nguvu, wapelekwe Rombo, vijana 10 wanapewa kata moja kushughulikia, kazi yao kuanzia asubuhi hadi jioni ni kutoa huduma. Ile aibu ya miaka ile sitaki tena itupate, bado hii nchi ina vijana wenye nguvu kuweza kuokoa jahazi na kuwatunzia heshima wanaume wenzetu wa Rombo.
Kama kulima watu walikuwa wanapelekwa mikoani kwanini wasipelekwe pia kwa hili jambo?
Ni lazima wa import kama mali ghafi?

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Rombo kwa zaidi ya asilimia 90 ni wakatoliki.
Iweje sasa wakatoliki wamwombe Mungu kuwaepusha na asili yao?
Ili parokia ikamilike ni lazima wawe na duka la vilevi. Kuna bar moja huko Moshi eneo la mji mdogo Himo, ina bar inayoitwa Kilacha. Hii bar ni maarufu kwa mapadre na masista kupombeka. Tena inamilikiwa na kanisa.
Shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake ati...........!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom