Rombo: Viongozi wa Kanisa Katoliki kufunga siku 9 kuomba Mungu aponye jamii na ulevi

tyina

Member
Jul 11, 2017
94
125
Pombe haijakatazwa, kilichokatazwa ni ULEVI ambao ni zao la kunywa kupita kiasi, kama ilivyo kwenye kula, ukila kupita kiasi (ulafi) ni dhambi vile vile. Kwani umeambiwa wanaokunywa pombe huko rombo ni wakatoliki pekee?
C ndo hapo sasa maana mpka madhehebu mengine yanakunywa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,935
2,000
Waombe kupinga ulevi, wakati kanisa lao linaruhusu kunywa pombe

Pumbaff

'When you’ve been an Arsenal fan as a kid, you will be one your whole life in some way.” David Alaba
Hii chuki yako juu ya wakatoliki ina mavuno yake

Kristu ndiye Tumaini letu
 
Dindira

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
2,923
2,000
Mpeleke Ali Heppy awe mkuu wa wilaya ya Rombo. Atakomesha unuwaji pombe usio na mpango ili hawa ma padre wafunge na kuwaombea mapdre wa kizungu huko majuu wasiharibu watoto wa kiume kwa kuwaingilia kinyume ma maadili
 
kunguru2016

JF-Expert Member
Aug 4, 2016
295
250
Rombo kwa zaidi ya asilimia 90 ni wakatoliki.
Iweje sasa wakatoliki wamwombe Mungu kuwaepusha na asili yao?
Ili parokia ikamilike ni lazima wawe na duka la vilevi. Kuna bar moja huko Moshi eneo la mji mdogo Himo, ina bar inayoitwa Kilacha. Hii bar ni maarufu kwa mapadre na masista kupombeka. Tena inamilikiwa na kanisa.
Shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake ati...........!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ati nini!bado cjakusoma hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,715
2,000
Rombo kwa zaidi ya asilimia 90 ni wakatoliki.
Iweje sasa wakatoliki wamwombe Mungu kuwaepusha na asili yao?
Ili parokia ikamilike ni lazima wawe na duka la vilevi. Kuna bar moja huko Moshi eneo la mji mdogo Himo, ina bar inayoitwa Kilacha. Hii bar ni maarufu kwa mapadre na masista kupombeka. Tena inamilikiwa na kanisa.
Shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake ati...........!

Sent using Jamii Forums mobile app

Huo ndio unaitwa unafiki. Kanisa linafundisha na kuruhusu watu kunywa pombe halafu leo linawaombea.
Shenzi zao
Habakuki. 25:15
Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!

Hoja hapa ni ulevi nyie mang'aa....!
Leteni hayo mafundisho yanayosema watu wanywe pombe haramu walewe....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,444
2,000
Pombe haina dini ni mapenzi ya mtu. Rombo zaman ilikuepo mbege nzuri sana hakukua na ulevi. Baada ya watu kuanza kupika Busaa au Dadiii ulevi ukaanza taratibu
Badae serikali ikaruhusu viwanda kama kimorali nk ulevi ukaenea zaidi
Kwa sasa nguvu kazi hakuna tena rombo hata nguvu za kuzaa hawana.
Mapadre wamechoka wakaamua kufuatilia chanzo cha ulevi nk
Sijaona sehemu imeandikwa ati kanisa katoliki linaruhusu pombe na wala hakuna maandiko yanayokataza kunywa mvinyo au pombe biblia inakataza ulevi haikatazi kunywa. Kuna kunywa na kulewa. Acheni kupotosha. Hao hao mnaotuaminisha biblia inakataza ulevi jaribuni kuuliza wanaoishi ulaya au marekana. Hao mnaowaona wasabato au walokole wanakunywa wine sana before na after meals. Huku africa jidanganyeni tu ati maandiko yanakataza pombe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pye Chang shen

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
6,640
2,000
Sijui kuhusu dini hiyo kuruhusu ulevi ila hili jambo la kuomba kwa mungu kupitia swaumu ni jema Sana tena kumuomba kuondoa uovu naomba mungu awakubalie
 
Nyox official

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
599
500
Viongozi wa Kanisa Katoliki wilayani Rombo wameanza kufunga kwa siku tisa kumuomba Mungu aiepushe jamii wilayani humo na tabia ya ulevi uliopindukia hususan kwa vijana.

Kwa mujibu wa viongozi hao, vijana wengi wanashindwa kuoa kutokana na ulevi.

Mkuu wa Vikarieti ya Rombo na paroko wa Usseri, Padri Emmanuel Lyimo alisema wameamua kufunga ili kukisaidia kizazi hicho kiweze kupenda kazi kuliko unywaji pombe.

Alisema Tanzania inapoteza vijana wanaotegemewa kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa uchumi wa Taifa.

Paroko huyo alisema kukithiri kwa unywaji wa pombe haramu katika wilaya hiyo kunatokana na vijana wengi kutokuwa na kazi za kufanya, badala yake wanaishia kwenye vilabu vya pombe na hatimaye kushiriki katika matukio mbalimbali ya uhalifu.

Kiongozi huyo wa dini aliiomba Serikali kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili kupunguza uzururaji wa vijana pamoja na vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji.

“Ni lini Serikali itakomesha unywaji wa pombe haramu pamoja na mauaji yasiyo na hatia Rombo?” alihoji paroko huyo.

“Serikali endapo itaanzisha vikundi vya ujasiriamali, haya matukio ambayo yanaendelea kwa sasa hayatakuwepo, kanisa tupo tayari kupitia jumuiya ndogo ndogo kuwakusanya vijana ili iwe rahisi kuwafikia walengwa.”

Alisema, “yapo makundi mbalimbali ya vijana yameibuka katika wilaya hii, wanavunja na kuchoma nyumba za watu, kupora pamoja na kuua. Hii hali kiukweli inasikitisha.”

Padri Lyimo alisema kutokana na hali hiyo waumini wa kanisa hilo wameamua kufunga na kuomba ili Mungu ainusuru jamii na matukio ya kihalifu yanayotokea.

Kiongozi wa jumuiya ya kanisa hilo, Athanas Joseph alisema wameamua kufunga baada ya kuchoshwa na matukio ya kihalifu yanayosukumwa na ulevi kupindukia miongoni mwa vijana.

“Sasa hivi hakuna vijana wanaooa, wengi wameishia kunywa pombe haramu, vijana wengi unakuta wanakunywa pombe aina ya gongo na mbundimbundi ambazo zinawamaliza nguvu kabisa,” alisema.

“Hapa kuoa hawawezi kabisa na mwisho wake baada ya muda kijana wa miaka 20 utafikiri ni mzee wa miaka 60.”

Aliitaka Serikali kuangalia namna ya kuwanusuru vijana wilayani humo kwa sababu wanaangamia.

“Kizazi kijacho hatutakuwa na vijana imara katika wilaya hii, tunaomba Serikali itusaidie kuwapatia vijana hawa mtaji angalau wajiingize katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali,” alisema Joseph.

Kwa mujibu wa wakazi wa wilaya hiyo, kuna zaidi ya aina 52 za pombe za kienyeji zinazonywewa wilayani humo.

Mmoja wa wakazi hao, Alfred Martin aliliambia Mwananchi kuwa kutokana na wingi wa pombe hizo na jamii kutokuwa na mbinu madhubuti za kudhibiti unywaji kupita kiasi, inakuwa rahisi kwa vijana kujiingiza katika tabia hiyo.

“Labda tu itokee kwamba kuna mkakati maalumu, lakini vinginevyo iwe ni maombi na ibada ili Mungu atusaidie,” alisema.
Aiseee,ma hom boy mmejakuaje?
 
sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,207
2,000
Kwanza ifahamike 80% ya Vijana wa Wilaya ya Rombo wanaishi mijini na tuna kazi zetu, tuna biashara zetu, tuna miradi yetu na tuna mchango mkubwa Kwa Taifa letu. Kule nyumbani tumeweka Vijana wachache wa kupalilia ile migomba na kutunza mashamba yetu maana ndiko tumezaliwa. Vijana walioajiriwa kufanya kazi hizo wametoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi hii.

Hivyo kusema Vijana wengi wa Rombo hatuoi kwasababu ya pombe huo ni udhalilishaji kwasababu kwanza kuoa ni uamuzi binafsi wa Mtu, lakini pili si kweli Vijana wote wa Rombo ni walevi na si kweli kwamba Vijana wengi wa Rombo hawajaoa. Wapo maprofesa hawajaoa, wengine ni walevi na wengine siyo walevi.

Ni mara ya pili hawa viongozi wetu wa kiroho kutudhalilisha Vijana wa Rombo kwenye média. Wakitaka waoe wao. Kama tatizo ni sadaka haitolewi ya kutosha, wabuni miradi kama wale wa zamani walikuwa na mashamba makubwa ya parókia, ufugaji wa Mifugo yote, biashara n. K. Watusubirie tu kipindi cha mwisho wa mwaka ndo tunakuja kuhesabiwa ndo unatoa sadaka huko ila tukiwa huku tunatoa huku huku. Na hao wachache ambao ni walevi (na ikumbukwe walevi hawapo tu Rombo hata ulaya wapo) awape elimu juu ya madhara ya ulevi wa kupindukia ili waokoe nafsi zao lakini kuwaandika kwenye magazeti, mlevi wa dadii anasoma gazeti saa ngapi?

In konki voice.
IMG-20190404-WA0003.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
104,876
2,000
Hilo litakuwa ni gazeti la ccm au vibaraka wake

In konki voice. View attachment 1062370

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we trust
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
104,876
2,000
Hadi uwache ukibaraka wako kwa ccm ndiyo tutakuelewa mjinga wewe

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom