Rombo: Viongozi wa Kanisa Katoliki kufunga siku 9 kuomba Mungu aponye jamii na ulevi

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
776
1,330
Viongozi wa Kanisa Katoliki wilayani Rombo wameanza kufunga kwa siku tisa kumuomba Mungu aiepushe jamii wilayani humo na tabia ya ulevi uliopindukia hususan kwa vijana.

Kwa mujibu wa viongozi hao, vijana wengi wanashindwa kuoa kutokana na ulevi.

Mkuu wa Vikarieti ya Rombo na paroko wa Usseri, Padri Emmanuel Lyimo alisema wameamua kufunga ili kukisaidia kizazi hicho kiweze kupenda kazi kuliko unywaji pombe.

Alisema Tanzania inapoteza vijana wanaotegemewa kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa uchumi wa Taifa.

Paroko huyo alisema kukithiri kwa unywaji wa pombe haramu katika wilaya hiyo kunatokana na vijana wengi kutokuwa na kazi za kufanya, badala yake wanaishia kwenye vilabu vya pombe na hatimaye kushiriki katika matukio mbalimbali ya uhalifu.

Kiongozi huyo wa dini aliiomba Serikali kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili kupunguza uzururaji wa vijana pamoja na vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji.

“Ni lini Serikali itakomesha unywaji wa pombe haramu pamoja na mauaji yasiyo na hatia Rombo?” alihoji paroko huyo.

“Serikali endapo itaanzisha vikundi vya ujasiriamali, haya matukio ambayo yanaendelea kwa sasa hayatakuwepo, kanisa tupo tayari kupitia jumuiya ndogo ndogo kuwakusanya vijana ili iwe rahisi kuwafikia walengwa.”

Alisema, “yapo makundi mbalimbali ya vijana yameibuka katika wilaya hii, wanavunja na kuchoma nyumba za watu, kupora pamoja na kuua. Hii hali kiukweli inasikitisha.”

Padri Lyimo alisema kutokana na hali hiyo waumini wa kanisa hilo wameamua kufunga na kuomba ili Mungu ainusuru jamii na matukio ya kihalifu yanayotokea.

Kiongozi wa jumuiya ya kanisa hilo, Athanas Joseph alisema wameamua kufunga baada ya kuchoshwa na matukio ya kihalifu yanayosukumwa na ulevi kupindukia miongoni mwa vijana.

“Sasa hivi hakuna vijana wanaooa, wengi wameishia kunywa pombe haramu, vijana wengi unakuta wanakunywa pombe aina ya gongo na mbundimbundi ambazo zinawamaliza nguvu kabisa,” alisema.

“Hapa kuoa hawawezi kabisa na mwisho wake baada ya muda kijana wa miaka 20 utafikiri ni mzee wa miaka 60.”

Aliitaka Serikali kuangalia namna ya kuwanusuru vijana wilayani humo kwa sababu wanaangamia.

“Kizazi kijacho hatutakuwa na vijana imara katika wilaya hii, tunaomba Serikali itusaidie kuwapatia vijana hawa mtaji angalau wajiingize katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali,” alisema Joseph.

Kwa mujibu wa wakazi wa wilaya hiyo, kuna zaidi ya aina 52 za pombe za kienyeji zinazonywewa wilayani humo.

Mmoja wa wakazi hao, Alfred Martin aliliambia Mwananchi kuwa kutokana na wingi wa pombe hizo na jamii kutokuwa na mbinu madhubuti za kudhibiti unywaji kupita kiasi, inakuwa rahisi kwa vijana kujiingiza katika tabia hiyo.

“Labda tu itokee kwamba kuna mkakati maalumu, lakini vinginevyo iwe ni maombi na ibada ili Mungu atusaidie,” alisema.
 
Serikali inabidi iunde kikosi kazi cha vijana wenye nguvu wakawasaidie kima mama na wanawake wa Rombo kutokana na wanaume wa Rombo kutojishughulisha kabisa na mambo ya chumbani zaidi ya pombe, ugwadu utawaua wamama wa Rombo, au serikali inataka waanze kukodi wanaume kutoka Kenya tena, tupate aibu tena ya kuimport wanaume kutoka nchi jirani?

Serikali iunde kikosi kazi cha vijana wenye nguvu, wapelekwe Rombo, vijana 10 wanapewa kata moja kushughulikia, kazi yao kuanzia asubuhi hadi jioni ni kutoa huduma. Ile aibu ya miaka ile sitaki tena itupate, bado hii nchi ina vijana wenye nguvu kuweza kuokoa jahazi na kuwatunzia heshima wanaume wenzetu wa Rombo.
 
Viongozi wa Kanisa Katoliki wilayani Rombo wameanza kufunga kwa siku tisa kumuomba Mungu aiepushe jamii wilayani humo na tabia ya ulevi uliopindukia hususan kwa vijana.

Kwa mujibu wa viongozi hao, vijana wengi wanashindwa kuoa kutokana na ulevi.

Mkuu wa Vikarieti ya Rombo na paroko wa Usseri, Padri Emmanuel Lyimo alisema wameamua kufunga ili kukisaidia kizazi hicho kiweze kupenda kazi kuliko unywaji pombe.

Alisema Tanzania inapoteza vijana wanaotegemewa kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa uchumi wa Taifa.

Paroko huyo alisema kukithiri kwa unywaji wa pombe haramu katika wilaya hiyo kunatokana na vijana wengi kutokuwa na kazi za kufanya, badala yake wanaishia kwenye vilabu vya pombe na hatimaye kushiriki katika matukio mbalimbali ya uhalifu.

Kiongozi huyo wa dini aliiomba Serikali kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili kupunguza uzururaji wa vijana pamoja na vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji.

“Ni lini Serikali itakomesha unywaji wa pombe haramu pamoja na mauaji yasiyo na hatia Rombo?” alihoji paroko huyo.

“Serikali endapo itaanzisha vikundi vya ujasiriamali, haya matukio ambayo yanaendelea kwa sasa hayatakuwepo, kanisa tupo tayari kupitia jumuiya ndogo ndogo kuwakusanya vijana ili iwe rahisi kuwafikia walengwa.”

Alisema, “yapo makundi mbalimbali ya vijana yameibuka katika wilaya hii, wanavunja na kuchoma nyumba za watu, kupora pamoja na kuua. Hii hali kiukweli inasikitisha.”

Padri Lyimo alisema kutokana na hali hiyo waumini wa kanisa hilo wameamua kufunga na kuomba ili Mungu ainusuru jamii na matukio ya kihalifu yanayotokea.

Kiongozi wa jumuiya ya kanisa hilo, Athanas Joseph alisema wameamua kufunga baada ya kuchoshwa na matukio ya kihalifu yanayosukumwa na ulevi kupindukia miongoni mwa vijana.

“Sasa hivi hakuna vijana wanaooa, wengi wameishia kunywa pombe haramu, vijana wengi unakuta wanakunywa pombe aina ya gongo na mbundimbundi ambazo zinawamaliza nguvu kabisa,” alisema.

“Hapa kuoa hawawezi kabisa na mwisho wake baada ya muda kijana wa miaka 20 utafikiri ni mzee wa miaka 60.”

Aliitaka Serikali kuangalia namna ya kuwanusuru vijana wilayani humo kwa sababu wanaangamia.

“Kizazi kijacho hatutakuwa na vijana imara katika wilaya hii, tunaomba Serikali itusaidie kuwapatia vijana hawa mtaji angalau wajiingize katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali,” alisema Joseph.

Kwa mujibu wa wakazi wa wilaya hiyo, kuna zaidi ya aina 52 za pombe za kienyeji zinazonywewa wilayani humo.

Mmoja wa wakazi hao, Alfred Martin aliliambia Mwananchi kuwa kutokana na wingi wa pombe hizo na jamii kutokuwa na mbinu madhubuti za kudhibiti unywaji kupita kiasi, inakuwa rahisi kwa vijana kujiingiza katika tabia hiyo.

“Labda tu itokee kwamba kuna mkakati maalumu, lakini vinginevyo iwe ni maombi na ibada ili Mungu atusaidie,” alisema.
Huo ndio unaitwa unafiki. Kanisa linafundisha na kuruhusu watu kunywa pombe halafu leo linawaombea.
Shenzi zao
Habakuki. 25:15
Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
 
Waombe kupinga ulevi, wakati kanisa lao linaruhusu kunywa pombe

Pumbaff

'When you’ve been an Arsenal fan as a kid, you will be one your whole life in some way.” David Alaba
Pombe haijakatazwa, kilichokatazwa ni ULEVI ambao ni zao la kunywa kupita kiasi, kama ilivyo kwenye kula, ukila kupita kiasi (ulafi) ni dhambi vile vile. Kwani umeambiwa wanaokunywa pombe huko rombo ni wakatoliki pekee?
 
Jibu hoja mkuu acha kunanga wachangiaji
Hawakufundishwa na kanisa katoliki kuwa walevi wa kutupwa. Wanywe kwa afya. Sasa tabia yao ya ulevi uliopindukia ndiyo kanisa katoliki litwezwe, kutukanwa na kufanyiwa dharau? Haiwezekani kosa afanye mtu fulani adhabu abebeshwe asiyehusika. Halafu :Hakuna aliyelazimishwa kubugia kilevi. Ni mtu akiwa na akili zake timamu anabugia kilevi.
 
Rombo kwa zaidi ya asilimia 90 ni wakatoliki.
Iweje sasa wakatoliki wamwombe Mungu kuwaepusha na asili yao?
Ili parokia ikamilike ni lazima wawe na duka la vilevi. Kuna bar moja huko Moshi eneo la mji mdogo Himo, ina bar inayoitwa Kilacha. Hii bar ni maarufu kwa mapadre na masista kupombeka. Tena inamilikiwa na kanisa.
Shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake ati...........!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna ulevi bila unywaji.
Mama wa ulevi ni unywaji.
Mlevi ni mtoto wa mnywaji.

Unatumia Biblia ipi mkuu?
Habakuki 25:15
''Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!

Biblia inasemaje kuhusu Pombe?

“Mtu akienda kwa roho ya uongo, akinena maneno ya uongo, akisema, Nitakutabiria habari ya mvinyo na kileo; mtu huyu atakuwa nabii wao watu hawa!” Mika 2:11. Umewahi kuwasikia watu wanapohaha namna ya kuhalalisha unywaji pombe kwa kusema, “Biblia haisemi Usinywe Pombe?” Hivi,kwanini siku hizi watu wanataka kuwa wema tu? Kuwa msamaria mwema tu? Hivi ni kwa nini wengi hupenda kujiingiza katika hali zisizo bora? Siku hizi sisi wakristo lazima tutambue kwamba kuwa mwema si bora. Na lazima tuwe tayari kujitahidi kuwa bora kwa ajili ya Bwana. Kama vile jana nilivyosikia katika hotuba, “kuwa mwema huififisha haki yetu ya ubora.” Na wakolosai 1:18 yafundisha, Yesu ni mtangulizi katika yote. Nakumbushwa juu ya simulizi inayowahusu Mariamu na Martha katika Luka 10:38-42. Martha alikuwa anahangaika ili kuwahudumia wageni wake wote, jambo ambalo ni jema. Walakini, Martha alipomtaka Yesu amkaripie Mariamu kwa sababu ya kutomsaidia kuwahudumia wageni, badala yake Yesu alimkaripia Martha kwa kufanya lililo jema. Alimkaripia Martha kwa sababu Mariamu alikuwa anafanya jambo bora. Alikuwa anamsikiliza Yesu. La msingi ni kwamba, katika kila hali kunakuwapo jema na bora. Je, unadhani Yesu anapendelea nini kutoka kwetu linapokuja suala la pombe? Najua wengine hudhani ni njema, lakini, hivi kweli pombe ni bora? Kwanza, “Yesu alitengeneza divai ili kuhalalisha unywaji pombe?”. Sote tumepata kusikia hoja hii kutoka kwa walimwengu. Natambua wenye dhambi hujaribu kuhalalisha hamu yao ya pombe. Hakuna anayetaka kuitwa mpotofu. Hata ingawa hoja hii inanikera, hainikeri kwa kiwango kikubwa kama ninapomwona mkristo anaanza kutumia hoja hii hii ya kale iliyochakaa. Naam, Naam, Naam, Yohana 2:1-11 panasema Yesu alitengeneza divai. 1. Tunatakiwa kulielewa vizuri jabo hili, kwani kama Yesu alimpa pombe mkuu wa meza ili wanywe, basi Yesu alitenda dhambi!!!! Habakuki 2:15 yasema “Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo” 2. Neno la Kiyunani lililotumika kuzungumzia divai katika Biblia ni neno la kiujumla, laweza kumaanisha divai au mvinyo ilevyayo. Na tunaacha fungu hili la maandiko liamue ni aina gani ya kinywaji kilichokuwa kinaongelewa. Isaya 16:10 “Akanyagaye hakanyagi divai katika mashinikizo; nimeikomesha sauti ya furaha yake akanyagaye”. Sasa kwenye mashinikizo kunatoka nini? Inatoka mvinyo au divai? Na bado Biblia ya kiingereza imetafsiri kuwa kinachotoka kwenye shinikizo kuwa mvinyo (wine). Wakati huo huo twajua ya kuwa maji yanayokamuliwa kutoka kwenye zabibu ni divai. Ushahidi ni hapa jinsi neno hili lilivyotumika kiujumla, limeingizwa katika lugha ya Kiingereza kama mvinyo, na lazima tuache fungu la maandiko kuamua kama kinachokusudiwa ni mvinyo au divai. Unaweza kuona hali hiyo hiyo katika Yoeli 2:24 Pili, tena nimewahi kusikia hoja kwamba “Mungu hakusema usinywe pombe.” 1. Mtazamo huu juu ya Biblia ni potofu. Biblia inatufundisha “Kwa maana tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; {Kumbuka kweli imefunuliwa wapi? Roho Mtakatifu}. Mkihakiki ni nini impendezayo Bwana. Wala msishirikiane na matendo yesiyozaa ya giza, bali myakemee; kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena,” Waefeso 5:9- 12. Namna sahihi ni “hakiki ni nini impendezayo Bwana”. Kiukweli, si kazi yangu kukosoa na silazimiki kukuonyesha kwamba unywaji pombe ni kosa. Mbinu ya kutumia inapaswa kuwa, kwenye pombe kuna ubora gani? Kwenye unywaji pombe kuna ubora gani? Sisi kama wakristo, tunatakiwa kutia muhuri wa kukubali juu ya mambo yenye ubora. “Mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi; bila kosa, mpaka siku ya Kristo.” Wafilipi 1:10 Halafu tena, hivi Mungu hajawahi kumwambia mwanadamu “Usinywe kileo?” Um, Walawi 10:9, “Usinywe divai wala kileo chochote.” Mstari huu waliandikiwa makuhani. Hivi sisi siyo makuhani? “ Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme….” 1 Petro 2:9. Hesabu 6:3 panaeleza kwamba waliokuwa wanadhiri hawakuruhusiwa kunywa vileo. Katika Kumbukumbu 29:6 Wana wa Israeli walijiepusha na vileo ili kwamba wapate kushika maarifa sahihi ya Mungu. Katika Mithali 20:1 mwenye hekima aliandika “Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi. Na akosaye katika vitu hivyo hana hekima.” Mithali 31:4 Panasema kwamba kunywa mvinyo hakuwafai wafalme na wakuu. Tena, Wana wa Mungu si wafalme na wakuu? Ufunuo 1:6? Isaya 24:9 panasema, “hawatakunywa divai pamoja na nyimbo.” Isaya 28:7 yasema “ Hawa nao wamekosa kwa divai; wamepotea kwa kileo.” 2. Biblia inatufundisha kwelikweli kwamba tusinywe pombe. Nadhani swali linalobaki ni kwamba, tuko tayari kumpa Mungu yaliyo bora?yenye ubora naya kwanza? Hivi ni lini unywaji pombe ukawa ndiyo jambo bora la kumpa Mungu? Najua kwamba yapo mafungu mengi katika Agano la Kale na Agano ambayo tungetakiwa kuyaangalia. Kuna hoja nyingi nzito na muhimu ambazo zingejitokeza. Lakini mtu anayejitahidi kwa kadri awezavyo kwa ajili ya Mungu ataona dhahiri ambacho mafungu haya yanafundisha. 1) Yesu asingetengeneza pombe na kumpa mwanadamu. Kufanya hivyo kungekuwa ni uvunjifu wa wazi kabisa wa Habakuki 2:15. 2) Mungu anasema, “Msinywe divai, wala kileo.” 3) Mungu anajua kuwa watu watataka kunywa pombe hadi watafikia hatua ya kutafuta waalimu wa uongo,ambao Mungu anawaita “wadanganyifu” ili wawambie kuwa ni halali kunywa vileo, Mika 2:11 Na kwa kuhitimisha nawasihi tutafakari Mika 2:11. Hapa Mungu anaelezea “furushi la uongo livumalo” na jinsi watoto wake waliopotoka walivyowapenda wahubiri wa namna hii. Mika anasema “mtu akienda kwa roho ya uongo , akinena maneno ya uongo, akisema, nitakutabiria habari ya mvinyo na kileo; mtu huyu atakuwa nabii wao watu hawa.” Maana ya Mungu iko wazi katika mistari ya 7-11. Yaani, wasioipenda kweli watampenda na kumfuata haraka mtu anayesema ni halali kunywa pombe. Paulo alisema hivyo hivyo katika 2 Timotheo 4:3 “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe wataipatia waalimu makindi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti.” Lakini kumbuka, Mungu anasema mwalimu huyo “anadanganya,” Mika 2:11
 
Huo ndio unaitwa unafiki. Kanisa linafundisha na kuruhusu watu kunywa pombe halafu leo linawaombea.
Shenzi zao
Habakuki. 25:15
Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Kuna imani inaruhusu wanaume kuoa wake hadi wanne lakini kwa kutimiza wajibu na kuwa na uwezo. Halafu wizara ya afya na taasisi mbalimbali zinasisitiza kuwa na mpenzi /mke /mume mmoja. Sasa ikitokea aliyeoa wake wengi akafa kwa UKIMWI (Mola apishilie mbali) tutawalaumu viongozi wa imani hiyo kwa kufundisha kuoa wake wengi?
 
Rombo kwa zaidi ya asilimia 90 ni wakatoliki.
Iweje sasa wakatoliki wamwombe Mungu kuwaepusha na asili yao?
Ili parokia ikamilike ni lazima wawe na duka la vilevi. Kuna bar moja huko Moshi eneo la mji mdogo Himo, ina bar inayoitwa Kilacha. Hii bar ni maarufu kwa mapadre na masista kupombeka. Tena inamilikiwa na kanisa.
Shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake ati...........!

Sent using Jamii Forums mobile app
Uliwahesabu? OK. Tuache hilo la takwimu ambazo hauna ila unahisi. Je, mapadre wamesema watawaombea wakatoliki tu?
 
Huo ndio unaitwa unafiki. Kanisa linafundisha na kuruhusu watu kunywa pombe halafu leo linawaombea.
Shenzi zao
Habakuki. 25:15
Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Kwahiyo sababu ajali kukidhiri tupige marufuku magari? Hao wanakemea ulevi tena kwa Rombo umekithiri na si unywaji pombe.

Uendeshe gari kizembe ulaumu gari badala nafsi yako, ufanye zinaa badala ya kulaumu nafsi yako ulaumu viungo vyako vya siri! Nyie bado mnaishi zama za sheria, usiguse, usinywe, usile n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakihamia CCM watapona
That’s all
That’s the cure walahi
 
Hakuna ulevi bila unywaji.
Mama wa ulevi ni unywaji.
Mlevi ni mtoto wa mnywaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiasi ndicho husisitizwa. Hata ukila chakula kupitiliza utavimbiwa.Kwa hiyo unataka kanisa liwawekee mita za kupima ujazo wa vilevi sambamba na midomo yao? Hizo lawama za kuhusu ulevi wa watu wapewe wenyewe. Msifanye kuhamisha lawama.Escapism ya jambo si dawa.
 
Back
Top Bottom