Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

BAKOI

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
1,213
2,326
Nimeisikiliza wimbo mpya wa Roma mkatoliki Leo
Nimependa pale anaposema ""Mungu wa daudi mungu wa Paulo na mungu wa yohana""""
Hio sentensi hapo naona inamajibu karibu yote ya kutekwa.

Rapa Roma Mkatoliki ameachia video ya wimbo wake ‘Zimbabwe’ ukiwa ni wimbo wake wa kwanza tangu alipotekwa na kuteswa kwa siku tatu.
Kupitia ‘Zimbabwe’ Roma amesimulia tukio la utekaji wake, watu anaoamini walimteka na sababu za kuamua kutoendelea kufuatilia jarada la upelelezi wa tukio hilo.

Mkali huyo pia amezungumzia kitendo cha baadhi ya wasanii wenzake kutomtembelea alipokuwa anauguza majeraha ya mijeredi ya watesi wake.
Pia, rapa huyo amezungumzia kauli ya Mbunge aliyedai bungeni kuwa amemtukana mkuu wa nchi.

Mkali huyo wa mashairi yenye mvuto wa maajabu (Rhymes of Magic Attraction) amekanusha tetesi kuwa watekaji wake walikuja na Noah huku akiwachana kuwa waachane na tabia za kutekana na kutumia silaha bali washindane kwa hoja.




https://www.jamiiforums.com/attachments/roma-zimbabwe-mp3.563185/

Mashairi ya Wimbo

Wengi mlijiuliza walionteka ni maaskari?
Mkanitafuta vituo vyote central hadi stakishari
Wakasema… hawajui nilipo mama alienda hadi mochwari
Dah.....
Ya Kaisari mwachie Kaisari
Machozi yenu yatalipwa mimi nafunga na kusali

IMBA ROMA IMBA X3

Mungu wa Paulo… ndio Mungu wa daudi
Na ndio Mungu wa John mnayemuita Yohana Wayahudi
Mwanangu alimuuliza, mama baba lini atarudi?
Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru sinabudi

Fahamu yakuwa..

Me sio tu rappa pia ni baba wa familia
Na watoto mahitaji nawapa kama isemavyo biblia

Kipi bora?..

Nife museme nilikufa kiharakati?
Siogopi kufa… ila nnawaachaje waliobaki?

Je?..

Nani katiyenu mwanangu atampa malezi?
Wapi atapata mahitaji?
Wapi atapata mapenzi?
Mama naye?..
Wapi atapata mahitaj na malezi?
Na report ya upelelezi
Vipi akiteka mtekaji?

Je?…

Kaburi langu mtalipalilia majani?
Nimeumwa hamjakuja kuniona
Mnangoja mje msibani?
Nlipokuwepo skuwa nnajua hii saa nne hii saa nane
Nlichohitaji… nitoke mzima na ndugu zangu tuonane

Nimechapwa mijeledi
Nimevunjwa bila huruma
Ahsante mliopaza sauti
Nimeiona nguvu ya umma
Siku tatu nimefumbwa macho
Mikono nimefungwa nyuma....

NAKWENDAA ZIMBABWE ZIMBOBWO YELELE MAMA WEE X4

IMBA ROMA IMBAA...SEMA BABA WEEEE

Nasimama na nnaunga hoja kwenye uchumi wa viwanda
Nanasi linaoza msoga kibiti linaoza shamba
Walioniteka hawakuja na noah… ni uvumi na visanga
Ila KUTEKANATEKANA Ni uhuni wa kishamba…
Weka bunduki chini si tubishane kwa hoja
Maana sote lengo letu ni kuijenga Tanzania moja
Me skuona nyota kwa shoulder ila najua we ni soja

Inshaalah..

Ulikuja mwenyewe ama ulipewa order?

Ewalah..

Aminini siku hazigandi
We ni yanga me ni samba kuwa mpinzani sio dhambi
Ipo siku mtawala atakuwa mpinzani
Samba akichukua kombe sijui atapona nani?

Na kuna Mbunge alisema eti nimemtukana mkuu
Utahukumiwa na mkono wa Mungu… namshtakia aliye juu

Kwanza lini?
Na kwanini?
Me nimtukane mjomba?
Umepewa gari ya wagonjwa mimi Tanga najengewa bomba

Me mbarikiwa na nikifa kuume kwa baba ntaketi
Na mtu wa watu.. that’s why lilisimama bunge la
bajeti Kunijadili mtanzania kuwa MAKINI PIA MAKINIKIA
NAYATUNGIA MAPINI PIA

Me nlitabiri utakuwa rais kipindi unaitwa waziri
Japo maisha sio rahisi ila pongezi unastahili
Waliosadiki Roma ataonekana kabla ya Jumapili
God bless imetimia injili niliyoitabiri

NAKWENDAA ZIMBABWE ZIMBOBWO YELELE MAMA WEE X4

IMBA ROMA IMBAA
SEMA BABA WEEEE
 
Nilitabiri utakuwa rais/ukiwa unaitwa waziri japo maisha sio marahisi/Ila unahitaji pongezi /

Track itakuwa stori ya town kwa mwezi huu.


Ameitumia fasihi kwa kiwango kikubwa saaana kufikisha ujumbe.

Neno ---- zimbabwe
---------Dr anayetibu
--------'Mwalimu anayefundisha

Na lyrics zingine nyingi.

Huu ndio muziki wa Roma sasa.
 

Attachments

  • Roma - Zimbabwe [Official Music VIdeo]_high_quality.mp3
    6.8 MB · Views: 442
Nimeisikiliza wimbo mpya wa Roma mkatoliki Leo
Nimependa pale anaposema ""Mungu wa daudi mungu wa Paulo na mungu wa yohana""""
Hio sentensi hapo naona inamajibu karibu yote ya kutekwa


Ambayo anayo atuwekee hapa
kitu pekee ambacho nimekuwa nikimuombea uyu dogo ni kwamba, awe alitekwa lakini walimhurumia kumtatua rinda. kama atakuwa amepoteza rinda hapo sasa, sijui atafanyeje. ila kwa trauma ile aliyokuwa nayo wiki lile, aisee kuna siku Mungu atawalipa watesi wake tu.
 
Nimeisikiliza wimbo mpya wa Roma mkatoliki Leo
Nimependa pale anaposema ""Mungu wa daudi mungu wa Paulo na mungu wa yohana""""
Hio sentensi hapo naona inamajibu karibu yote ya kutekwa


Ambayo anayo atuwekee hapa
 
uyu dogo atatekwa tena muda si mrefu. tuwe tu makini tumsaidie atoke tena akiwa mzima. mungu wa paulo, mungu wa john, mungu wa daudi? dah? waliosema nitaonekana hada jmosi sijui jpili haitafika ilitimia vilevile? who was that? nilitabiri ukiwa waziri utakuwa rais?, mbunge uliyesema mimi nimemtukana nimekushitakiwa kwa mungu?...hahaha, aisee dogo bado ana kinyongo na Mungu atamsaidia kuwalipa watesi wake sawasawa na walivyomtenda. one day yes.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom